Wanasimba njoo hapa mseme ukweli

KAGAMEE

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2013
Posts
4,457
Reaction score
5,454
Hakuna kipindi mtu anasema UKWELI kama kipindi ambacho amekasirika, yaani anaweza kutaja michepuko yote mbele ya MUME/MKE wake.Wanasimba tumevurugwa kweli kweli.

Kipindi ambacho tuna hali hiyo hebu jibuni hapa haya maswali ili na mimi mwanasimba (nipate uelewa Niwe na cha kuongea mbele za watu)÷

1. Zile 20B ziliwekwa account gani?

2. Mimi sina imani na Mo nyie wenzangu mmefanywa nini kuendelea kumuamini kiasi hiki?

3. Lini mwisho wa machungu haya (uteja kwa Yanga)mbana kama hamna dalili?

4. Mnadhani hata huyo Manzoki tunayemtaka atapita mwenyewe ule ukuta wa Yanga? Huyo huyo manzoni ndo atamkaba mbaya wetu Mayele?

5.Je mnajua kama kuna adui yetu mkubwa ameongezeka pale mbele AZIZ KI?

YAANI NIMEVURUGWA HASWA
 
Huyu Mayele atatuua kwa presha.Huoni goli la pili alivyowafinya mabeki?
Kipindi cha kwanza hakuonekama kwa sababu ya viungo wote wa Yanga waliwekwa kwapani na akina Kanoute na Chama, kitendo cha kuwatoa tu, Mayele akafanya yake maana mipira ilikuwa inadondola tu kwa kwake,anaisogeza na kuangalia afungie wapi...hatari sana.
 
Haya Ina kikosi bora na kocha bora na kwa sasa wapo kwenye mfumo.

Haya maswali mengine mwulize mwekezaji au unaweza kwenda ofisi za Simba au Mo ili upate majibu.
 
Nikikumbuka enzi zile mnamkejeli kwa kumuita Aziza! Nabakia kucheka tu. 😁

Na bado wale wengine akina Gael Bigirimana, Kambole na Joyce Lomalisa! Wakianza kukinukisha mtaita maji mma kudadek!
 
Hacha
uongo man.......mayele aliwatia kamba goli la kusawazisha wakati hao makolo uliowataja wote wapo ndani ya uwanja.
 
Nikikumbuka enzi zile mnamkejeli kwa kumuita Aziza! Nabakia kucheka tu. [emoji16]

Na bado wale mwengine akina Gael Bigirimana, Kambole na Joyce Lomalisa! Wakianza kukinukisha mtaita maji mma kudadek!
Of course ni Aziza, na mwingine naye ni Joyce, au unataka kusemaje?
 
kabla ya kuingia mo Simba ilikuwaje?
Kama mnaweza kujiendesha wenyewe mbona mlishindwa?
HAKUNAA MTU ANAYEWEKA HELA ZAKE AKITEGEMEA HASARA.
Kama kuna faida moo amepata pale Simba ANASTAHILI HYO FAIDA NA ATAENDELEA KUSTAHILI
 
Tatizo ni kufungwa na Yanga au nini?

Acheni kulalamika, kila siku Simba hivi Simba , imewapasa kufahamu Yanga nao walijipanga, kupoteza derby sio kipimo Cha ubovu wa kocha!

Nenda karudie kuangalia match, first half nzima Zoran aliiweza, tactically na technically alikua good na aliwamudu yanga ( ispokuwa credit iende kwa naby aliegundua mtego wa Zoran) ,hajakaa vizur Sana na wachezaji wake kuwasoma character zao, lazima tumpe muda.

Tunatakiwa tuache malalamiko, j5 tuna Jambo letu pale estadeo de lupaso
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…