Wanasimba semeni na Frank Domayo anaweza akawaelewa au akajifunza kitu

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Mpira ni mchezo wa kiuungwana. Kitendo alichofanya Frank Domayo ni cha makusudi. Amekuwa akitumika hivi kila mara. Alishafanya kwa mchezaji wenu mwingine John Boko.

Nadhani mnapaswa mseme naye kuwa huo sio mchezo. Hii michezo ya kihuni sisi wapenda mpira wa miguu hatuitaki. Hata kama mimi si Simba, lakini naamini kuna siku mhuni mmoja atafanya hivyo kwa mchezaji wa team yangu.

Nashauri mashabiki wa Simba msiliache jambo hili kiwepesi. Semeni na Frank Domayo nadhani anaweza wasikiliza na wachezaji wengine wenye tabia za kihuni watajifunza pia.
 
Mambo ya kawaida kwny Soka japo sio fair play

Aliwah kumfanyishia hata Boko

Shomari ana bahati mbayj sana
 
Huyu ni wa kudundwa tu anazoea
 
kinachokera ktk rafu ile ni mchezo ulikuwa umemalizika na pia Domayo anamjua vizuri sana Kapombe tangu wakiwa wote Azam Kuwa ana matatizo ya goti hivyo amekusudia na anasahau kuwa TAIFA STARS ina uhaba wa namba mbili.
 
Yule anashughulikiwa kimtindo baada ya miezi miwili atakuwa shosti kama Nabii Tito
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…