Wanastahili pongezi wachezaji na benchi la ufundi

Joined
Aug 19, 2018
Posts
43
Reaction score
76
TANZANIA

Na Xavi Hernandez Alcantara

Tungeweza kuwafunga mapema tu Burundi hata kule kwenye penati tusingefika bila shaka lakini tushukuru kwa ushindi Ambao tumeupata kupitia mikwaju ya penalti. Wachezaji wa Burundi wakiondoka basi bila shaka watakuwa wakiulizana. Juma Kaseja anacheza Raja Casablanca au Tp Mazembe lakini wataambiwa yupo Kmc tu kule kinondoni.

Kocha Etiene bila shaka kuna sehemu alikosea. Kama nlivyosema tungeweza kuwafunga Burundi ndani ya Dakika 90 ni pale kibao cha Sub kilipoonesha Salum Abubakar Sureboy nje na nafasi yake kuchukuliwa na Shabani Chilunda. Etiene aliitaji goli. lakini aliuwa sehemu ambayo magoli yanazaliwa.

Burundi kuna zile Dakika waliuchukua mchezo wakashambulia sana. Tayari Jonas Mkude alibaki chini. Alafu Idd Nado acheze juu yake jambo ambalo kwa Idd halikuwezekana kirahisi. Aliendelea sana kucheza pembeni,Kushuka si kwa wakati.

Kibaya wale wa mbele hawakuwa na hata asilimia 10 ya kukaba(Msuva,Samatta,Farid Mussa) Ukiachilia mbali kazi nzuri ya Juma Kaseja kazi nyingine ilifanywa na Jonas Mkude katika kiungo. Alipambana sana hadi pale Himid Mao alipokuja kumsaidia ndio maana zile dakika za lala salama Burundi waliutafuta sana.

Sina shaka na Kocha Etiene mwalimu wa kiwango kikubwa. Tunakwenda Group Stage tunakwenda kupambana. Kama tulivyopambana leo dhidi ya Burundi ukiskia Burundi unaweza kuwadharau lakini wana timu imara. tuliwaona Afcon hawa.

Nimekaa Nimewatazama Kelvin Yondani na Erasto Nyoni. Wanaume hawa katika ukuta wa Tanzania. Sijui siku wakiuacha wengine kuvaa viatu vyao haitakuwa rahisi. haitakuwa rahisi kabisaa wamecheza na wanaendelea kucheza kwa kiwango kikubwa mno. Respect sana kwao.

Burundi wanamfahamu Samatta waliweka ulinzi mara dufu. walicheza nae kibabe mpira uwapo mguuni kwa Samatta ile Sub ya Samatta wala sikuwa na wasi wasi nayo kabisa.

Leo Nimemuona Gadiel Michael Mbaga mwenye miguu ya Tshabalala. Umenielewa? Amepanda sana kushoto,Amepiga sana kazi,Amezuia sana kushoto. Na alipogundua kwamba Erasto Nyoni kapiga penalti kulia,Na Himid amepiga kulia yeye aliamua kupeleka juu what a penalti?

Baada ya Group Stage kumalizika kuna sehemu Naomuona Simoni Msuva. Kwa sasa amekuwa mtu kweli kweli. Ball Ballance,Ball control,Maamuzi vyote anavitimiza kwa usahihi kabisa Yah Msuva.

Juma Kaseja,Juma Kaseja,Juma Kaseja nimelitaja mara tatu. Nafikiri Beno Kakolanya,Metacha Mnata wala hawakushangaa kwanini wakaa nje ikiwa Juma Kaseja ameanza mbele yao.Mikono yake bado ina miujiza ile ya mwaka 2003 katika Dimba la Zamaleck.

Hongera sana Tanzania. Tuanzie hapa kuyatafuta mafanikio kamwe huwezi kuanza na 5 bila ya moja. Zamani ziliwahi kuwa ndoto lakini kwa sasa inawezekana Miezi kadhaa iliyopita tulicheza Afcon leo hii tunaenda kucheza hatua ya makundi kuwania kufuzu Kombe la Dunia sio mbaya. Mwanzo hauwezi kuwa mwepesi.
 
Unajua mahana ya NADO uku uswahil alipo tokea uwa tunamwita ronaldo ni shidah sana uyu watot wa Keko wanalijua ilo
jamaa nilimuonaga game ya nusu fainal hapo uwanja wa stakhishari kabila hajatoka wala hatujamsikia ndondo cup nikamwambia washikaji uyu mpira usipokuja kumlipa ajiue tu jamaaa ni blaaa hana utani kabisa kama Cr7 OG
 
Tunakosea wapi Kama Taifa..Kuitoa Burundi tunaandamana?
 
Kweli aiseee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…