Wanataaluma Wakristo watoa waraka wa 'Tafakari' kabla ya kuichagua CCM

Habari Leo
CHAMA cha Wanataaluma Wakristo Tanzania (CPT) kimekiri kutoa waraka ambao wenyewe wameuita ‘tafakari’ ukikishambulia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kukituhumu kuwa ndicho kikwazo cha ukuaji demokrasia nchini.

Nafikiri tuachane na mambo ya udini hapa maneno hayo hapo ndio uliokuwa msingi wa waraka tunachotakiwa ni kutafakari kweli CCM ndicho kikwazo cha demkrasia nchini.
 
Nafikiri baazi yetu tunajadili hii hoja tukiwa na mawazo kwamba wakatoliki ni wa upande mmoja wa kiroho tu, sii hivyo hata kidogo.

Jamaa wako full active kwenye masuala ya kidini, kisiasa na kijamii. Mfano mzuri ni kwamba nchi yetu ni moja ya nchi ambazo yupo balozi wa vatican, na sii hapa tu hata UN wanae balozi. Sasa mnafikiri wale mabalozi wamekubadiwa kama wawakilishi wa dini fulani?

Cha msingi ndani ya huo waraka japo sijausoma ni kujiuliza ni nani atakae mkemea ccm kama sii yale makundi au viongozi ambao kazi zao sii za siasa moja kwa moja? Maana wakizungumza wanasiasa wapinzani ambao kimsingi ndio waasirika wakubwa wa mfumo kandamizi wa ccm tunaaminishwa kwamba ni propaganda za kisiasa.

Binafsi sioni kama kuna udini kwa kundi lolote liwe la kiislam, kikristo au kipagani kupaaza sauti zao dhidi ya unyanyasaji wa aina yeyote iwe ni katika vyama au taasisi yoyote. Walinzi wa katiba yetu ni sisi sote yaani wenye dini na wasio na dini na wala hakuna haki ya wanasiasa pekee kujifanya kwamba mustakabali wa nchii hii upo mikononi mwao.

Pia hatujawa vipofu wa kuweza kufahamu kwamba kama kuna vinara wa kuendesha siasa kwenye nyumba za ibaada ni ccm.
 

waraka wa wakatoliki ulikuwa positive na haukuwa na ubaguzi wowote kwa raia yoyote. Ila walioupokea ndugu zetu waislamu waliupokea na kuandika wao ambao hakuwa na maslahi ya taifa. Issue hapa ni wisdom zaidi ambayo kaka sisi wakristo tunapaswa kuwa nayo. sisi wote tunajua waislamu walivyo, na kuishi na hawa ndugu inahitaji hekima. Tukianza hizi stori za dini na kila mmoja aseme kwa mgongo wa dini, basi tuwe tayari kila kitu kwenda kwa mgongo huo huo.

Kuna mkristo ataanzisha kampuni na kuajiri wakristo watupu na kisingizo chake, ni kuwa hapaswi kuficha identity na imani yake, hali itakuwa the same kwa dini zingine.

Hao wanataaluma wangekaa chini kama kweli ni intellectua na wangefikia tamati huwezi ukataja ubaya wa CCM bila kuwahusisha wakristo na waislamu nchi hii! matatizo ya CCM na serikali yake yanaanzia kwenye hizi dini, ambazo zinakumbatia hawa mafisadi, leo hii unasema CCM ,mbaya, then unasema Nyerere awe baba mtakatifu

Matatizo ya CCM yameanza siku nyingi sana , wakristo na waislamu kuwakumbatia hawa mafisadi hakujaanza leo, free thinking za waumini wa hizi dini mbili haipo!

I will feel good kama leo hii hao wanataaluma wakapambana na wakristo wawe huru katika kuwazaa na kuchallenge(KUANZA MAKANISANI kwenye udiketata wa kila aina, si RC mpaka kwa akina Kakobe). It does not make sense kusema CCM wabovu wakati mafisadi akina EL, ndiyo wanaungwa mkono na akina Malasusa.

CPT should start to clean church mbalo limeoza na ni chafu, na usafi unaanzia makanisani kwenda nje , siyo CCM kwenda makanisani.

We have weak nation because we have weak churches we have weak churches because we have weak families!

Hao hao sio ndio waliosema JK chaguo la Mungu kwani tumesahu, kunzia RC mpaka Pentecost.

Nyerere alisema huwa hatuulizani dini wala makabila, watanzania sisi, dini wekeni kapuni kwanza.

CCM wachafu, tuseme kema watanzania CCM wachafu ondokeni!!! siyo niseme kama mkristo
 

Falesy, mi nafikiri lengo la hoja linazidi kupotea kabisa pale tunapozidi kujadili hili. Sasa katiba, memorandum, registration hivi vyote ni vya nini katika hii hoja waliyoitoa? Na je wana umuhimu wowote wa kuappload hivi hapa? Basi pale utakapovihitaji sio mbaya ukwauliza ili kujua jinsi wanvyoendesha mambo yao lakini kwa sasa hii "tafakari" yao ina mantiki? Hili ndo la kujadiliwa hapa na identity ya mtu isije ikakuathiri katika kumjudge kile anachosema la. Sidhani kama mtoa hoja alikuwa amedhamiria hilo bali ni kiini cha habari yenyewe. Hebu angalia post ya ngapi hii? Je hoja imeguswa hata kidogo?

Kuwepo kwa CPT pia si kosa ni sawa tu kule mashuleni kulipokuwa na TYCS na vinginevyo basi labda tufungue thread nyingine ya kuhoji uhalali wa luwepo kwa hizi organization lakini si katika hii
 

Teh teh teh. Mkuu una mantiki lakini kumbuka ccm ni kisiki cha mpingo, hekima kwao haifai kitu. Hawa jamaa dozi yao ni rungu tu. Tena lele la kiafande lenye minundu.
 
Teh teh teh. Mkuu una mantiki lakini kumbuka ccm ni kisiki cha mpingo, hekima kwao haifai kitu. Hawa jamaa dozi yao ni rungu tu. Tena lele la kiafande lenye minundu.

Nakubaliana na wewe kama unataka rungu basi iwe;

moja

Hilo rungu lingeanzia na kuwatenga kwenye nyumba za ibada!

au

Pili

hao wataaluma ningewaona wazuri kama wangesema, wakristo wote hawatapiga kura wala kujihusisha na lolote lile la kisiasa mpaka

1. Katiba ibadilishwe
2. mafisadi wafunguliwe mashtaka
3. Rais apnguziwe madaraka'
4. Serikali ya mseto

Leo kanisa likisimamia haya na kufanikisha, ndio tumeula, nilitoa ule suahrui kulinga na wao walivyoutoa.
 

Waberoya umenena jambo jema kweli hawa kama wanataka kuwashughulikia wangeanza huko huko ktk nyumba za ibada. Kwani hawa wote ni waumini lakini utashangaa huko wanapapatikiwa. Wangewaweka chini na kuwaambia jamani ninyi ni waumini wenzetu lakino mnatuabisha
 
kama vile chama cha waislamu wenye msimamo mkali, bakwata, hizborallah, hamas au vipi?
 

Nadhani siyo rahisi kwa wakristo hasa wakatoliki kuanzisha chama cha siasa kwani haya mambo yanatenganishwa kabisa na SIASA na DINI kwa wakatoliki.

Mi nadhani unaifahamu dini gani hapa duniani ambayo haitenganishi dini na siasa na nina hakika wewe ni muumini wa dini hiyo. Dalili za dini isiyotenganisha siasa ni kutaka kila utaratibu wanaokuwa nao ndani ya dini yao uingie ndani ya katiba ya nchi. Nadhani pia unazifahamu nchi nyingi hapa duniani ambayo zinatawaliwa kidini na hasa dini isiyohubiri upendo zaidi ya jino kwa jino na lazima wewe utakuwa muumini wa hiyo imani.

Kwa wakatoliki, wanaikosoa serikali yoyote ambayo inaelekea kutokuwa na usawa na kwa hili sidhani kama ni udini kama unavyosema.

Kuhusu upendeleo sijaelewa ni upendeleo upi kwani nadhani hawa wakatoliki/ wakristo wanajitosheleza kielimu na kiuchumi kiasi kwamba wanaweza kuendesha mambo yao bila kutegemea kulipwa mshahara na serikali, nadhani hiyo imani yako unaelewa fika kwa nini mlitaka mambo yenu ya kidini myaingize ndani ya katiba, kubwa lilikuwa ni ajira kwa viongozi wenu. Hawa wakatoliki hawana haja ya kushindwa kukemea kwani siyo wanafiki.

Ni hayo tu ukitaka waweza kwenda kwa mtabiri wenu akueleze ni imani gani inaongoza hapa duniani kwa kuwa na msimamo na mtazamo wa kirafiki kwa watu wote na vinginevyo akueleze ni imani gani imesimama na itabaki imesimama kikamilifu kwa muda wote. Sali sala zako na mimi nitasali nevena!
 

Bahati mbaya sana chama hakiendi ibadani ila tu wafuasi wa hicho chama ndio wanaingia kwenye nyumba za ibada. Sasa wakuu wa dini hawana bifu na mtu binafsi ila wana usongo na hili limfumo kandamizi.
 
Bahati mbaya sana chama hakiendi ibadani ila tu wafuasi wa hicho chama ndio wanaingia kwenye nyumba za ibada. Sasa wakuu wa dini hawana bifu na mtu binafsi ila wana usongo na hili limfumo kandamizi.

Hewaa! hapo ndio pagumu sana ni wakati gani useme chama na ni wakati gani umseme mtu! , CCM ni watu na sio likitu fulani ambalo halieleweki, hao watu tuna makanisani na misikiti, wanatoa mafungu ya kumi na tunawaheshimu sana!

Pagumu hapa mkuu, huwezi kawasema watu pasi kugusa iani na vyama vyao! Makanisa yangekuwa makali, tungejua sehemu ya kuwapata hawa mafisadi ni CCM tu, huku makanisani tukisema tupange strategy ya kuiondoa CCM, mtu wa pembeni yako ni CCM!!
 
naamini kuzaliwa Mkristo ni bahati na baraka, kuzaliwa Mkristo peke yake ni ishara ya mtu mwenye akili timamu, mwenye mapenzi mema, mtu anayeweza kuona mbali tena mbali sana, mwenye kuyaona maisha katika mwanga wa ajabu.
ninaamini hao wanataaluma Wakristo wanamaono sana....wanaiona nnchi hii kwa namna ya kipekee, wanamapenzi ya dhati.
 
kama vyama vya siasa vimefail kuongea na kuonyesha njia, basi vikundi vinavyoshughulika na maswala ya kijamii vikiwemo vya dini ni lazima viseme,

dini zote zinakataza rushwa, uuwaji nk, sasa kama hivyo vitu vinafanyika na serikali hipo kimya kwa nini watu wa dini wasiseme, mimi sioni ni tatizo lolote hapo, ni eleement za udini tu ambazo watu wanazo ni zinawakwaza, ingekuwa hii kauli imetolewa na mtandao wa kijinsia Tanzania nadhani watu wote wangekuwa na kauli moja, lakini kwa sababu ni watu wa dini wamesema basi inakuwa kero
 
well done hii ni njia sahihi kabisa ya kutoa tafakari ya kuuelimisha umma.Elimu imetolewa mwenye kuelewa na aelewe.Mwenye mawazo finyu ya kudhani huu ni udini shauri yake.Au wanaopinga tafakari hii ya wanataaluma wa Kikatoliki walitaka wafanyeje??waanze kujilipua kama watu wa imani fulani????
 

Unachokisema na nilicho kisema ni vitu viwili tofauti.nadhani umemkoti wrong person poleeee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…