Mmea Jr
JF-Expert Member
- May 20, 2016
- 798
- 1,871
NDEFU KIDOGO
Habari zenu wakuu , nadhani wote tunalikumbuka vizuri lile zoezi la urasimishaji liloanza chini ya raisi wa awamu ya tano marehemu jpm . Ukiachilia mbali changamoto zake , moja ya mambo ambayo mimi kama raia nilifurahia ni jinsi ambavyo wananchi tuliweza kujua hatua kwa hatua juu ya mchakato mzima wa urasimishaji wa ardhi na makazi kwa kupitia mikutano mbali mbali ya mitaa ambayo alianzishwa kwa lengo lakumjuza mwananchi nini kinatakiwa .
Nakumbuka vizuri hatua ya kwanza ni ilikuwa ni kuandaa mkutano ambao uliwashirikisha pia maafisa ardhi ambao walitupa elimu nzuri kabisa juu ya faida ya kupimiwa maeneo yetu namna ya upimaji utakavyokuwa lakini pia hata gharama za upimaji , hakika ilikuwa ni mkutano mizuri sana , afisa ardhi alisema kila " mwananchi atatakiwa atoe kiasi cha sh 150, 000/= tu kwani kiasi kingine serikali yetu pendwa ilikuwa imetusaidia katika kukilipa " hakika tulipaga makofi ndelemo na vifijo juu ya taarifa hii nzuri aliyotolewa na bwana àrdhi yule . Baada ya hapo tulipimiwa maeneo yetu ikifatiwa na usimikwaji wa bicon ( bikoni ) na kuna form ambayo ilitakiwa kila mtu ampatie jirani yake aliyepakana naye aiweke sahihi ili kujiridhisha kuwa bicon zilizowekwa mipakani ziwekwa sahihi kabisa . Ikimbukwe michakato hii yote ilihusisha mikutano ya hadhara ambayo mara nyingi ilifanyika kila mtaa kwa uwazi kabisaa .
Hatimaye zoezi lilofuata baada ya hayo yote ilikuwa ni utoaji wa hati kwa wale wotee waliokwisha maliza michakato tajwa hapo juu , kwa mtazamo wangu nilifikiri hili pia lingeanzia kwenye mikutano ya mitaa wananchi tupewe taarifa kuwa hati zipo tayari pia tuelekezwe taratibu zote zin azotakiwa ili kama itawezekana kila mwananchi akajichukulie hati yake kiurahisi kabisa .
Lakini katika hali ya kushangaza jana nimepigiwa simu na mtu aliyejitambulisha yupo ofisi za ardhi , akinitaka leo siku ya jumamosi tarehe 17 , nifike katika ofisi zao ili nikajichukulie hati yangu . Leo nimeitikia wito ila nimeambiwa natakiwa nitoe laki na nusu (tsh 150,000/=) ndipo nipatiwe hatii nikajalibu kuwakumbusha juu ya ile laki na nusu tuliyowapa kipindi zoezi hili limeanza nikajibiwa kuwa ile ilikuwa ni kwa ajili ya upimaji na hii ya sasa ni kwa ajili ya hati hivyo ni vitengo viwili tofauti . Nikajitetea kwa kusema sawa " mimi leo nilikuja kwa ajili ya kuitikia wito tu sikujua kama natakiwa pia kuja na hicho kiasi mlichonitajia , hivyo naombeni muda nikajipange na pindi nitakapo pata basi nitawaleteeni hicho kitita cha laki unusu mnachokiitaji " mmoja akasema sawa lakini jitahidi si unajua tena ma-file ni mengi ukichelewa linaweza kupotea wakaniruhusu nitoke nikiwa na maswahili yafuatayo
- kwanini watu hawa hawaja taka kulitolea ufafanuzi shwala hili la gharama ya hati kama walivyofanya huko nyuma kwa kuhitisha mikutano na kuwajuza wananchi juu ya jambo hili ?..
Nikiwa katika dimbwi hili la maswali kimoyo moyo Nikasema hamna shida kule jamiiforum kuna watu wana- deal na mambo haya wanaufahamu wakutosha sana ngoja nikawaulize ili nipate undani wa swala hili. Je wadau hichi nilichokutana nacho ni sahihi?

- kweli kiasi hiki cha sh 150,000/= walichokitaka ni sahihi au kuna harufu ya upigaji inayoninyemelea hapa?..
- sawa kama kiasi hiki ni sahihi nakilipa kwa njia ipi ya benki au nawapa tu cash mkononi?..