Masi Lambo
JF-Expert Member
- Apr 8, 2020
- 532
- 360
Wanadai wagonjwa wa magonjwa mengine wakipata korona wanakufa na magonjwa hayo siyo korona, kama kisukari, moyo, saratani n.k. Lakini duniani kuna hata watoto walio fit bila magonjwa mengine, wamekufa na korona, kuna watu wazima wenye Afya zao wamekufa na korona.
Kwa madai yao wanatupotosha kufikiri korona haiuwi kama rais alivyodai mwanzo na kuonyesha hana ujuzi wowote wa hili na anaongea pumba tu, maana watu wengi hata TZ wamekufa na korona.
Pia wanatupotosha kwa kutotangaza idadi ya visa vya korona wakati dunia nzima inaona umuhimu wake katika kupambana nayo, hili jambo linatufanya tufikiri korona haipo au haijasambaa.
Namuunga mkono rais kwa ugunduzi wake wa uitilafu wa mashine za kupima, lakini maelezo yake ni finyu yasiyoeleweka kufanya wengi wafikiri korona sio kweli na haipo. Zaidi angalia video hii,-