Wanaume tu viumbe tunaopenda 'changes' muda wote. Hatuwezi kutumia kitu kimoja (ambacho kwa jinsi kilivyokuwa jana, ndivyo kilivyo na leo, na hata kesho unajua kitakuwa vivyo hivyo). Hii ina maana kuwa kama wanawake watakuwa wabunifu katika mahusiano (kwa maana ya kufanya kitu kisizoeleke), basi wanaume hawana haja ya kwenda nje. Kwa nini ukatafute vitu vipya nje, tena mbali ilhali hivyo vipya unavyo ndani?
Wanawake wengi huwa wanakuwa wabunifu siku za kwanza za mahusiano (wanafanya kila kitu kipya). After a while, sijajua ni kwa nini, wanakuwa 'constant'.
Mfano; Upo katika ndoa. Mpangilio wa sebule yako uko vilevile kwa muda wa hadi mwaka (Unaweza hata kuichora sebule yako hata ukiwa mbali na nyumbani). Wanaume wakizoea hali hii, hawatatulia 'home' hata kidogo. Watatoa visingizio ili mradi tu aende hata kwa marafiki zao ili wakaone vitu vipya.
Mwisho: Umbile na uzuri wa nje, vyaweza kuwa sababu ya wanaume kutulia. Lakini si mara zote.
-Tafakari-