Wanaume kuanza kukaguliwa kama wametahiriwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532

Serikali nchini kuanzia leo Jumatatu itaanza kuchunguza nyeti za wanaume ikiwa wametahiriwa, katika kaunti nne za eneo la Nyanza.

Wizara ya Afya nchini humo imesema uchunguzi huo unaoendeshwa na Shirika la Wanaume Kutahiri kwa Hiari (VMMC) unalenga kuimarisha vita dhidi ya maambukizi ya virusi vya ugonjwa hatari wa Ukimwi katika kaunti hizo.

Uchunguzi huo pia unalenga kufahamu idadi ya wanaume waliotahiriwa katika kaunti za Homa Bay, Kisumu, Siaya na Migori. Wakati wa uchunguzi huo wa miezi mitatu, wahudumu waliopokezwa mafunzo watakagua kibinafsi uume wa mwanaume iwapo anayechunguzwa atakubali na akikataa atajibu tu swali iwapo amepitia kisu cha ngariba au la.

Hata hivyo, mila na desturi za jamii huenda zikazuia baadhi ya wanaume kuhojiwa kuhusu iwapo wametahiriwa au la.

Huduma za VMMC zilianza kutolewa katika eneo la Nyanza mwaka wa 2008 kabla ya kueneza huduma hizo hadi maeneo mengine ya nchi.

Jukumu lake lilikuwa kusaidia kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya Ukimwi katika Kaunti za Nyanza ambazo zimekuwa zikisajili zaidi ya asilimia 20 ya maambukizi. Utafiti unaonyesha tohara hupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa asilimia 60.

Kulingana na Dkt Akeche, utafiti wa kuchunguza nyeti za wanaume Nyanza umefadhiliwa na serikali ya Marekani pamoja na Kituo cha Kudhibiti Magonjwa(CDC) na utasaidia kuamua iwapo rasilimali zaidi zitawekezwa katika kupambana na ugonjwa wa Ukimwi maeneo ya Nyanza.

Chanzo: Taifa Leo, Kenya
 
Woyooo middle income ya wasiotahiriwa za asubuhi. 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂 Karibu huku Tarime mpigwe kisu bila Ganzi
 
Mimi sitoi govinda langu kwanza linasifiwa na mamsap

Hehehe!! Ina maana sisi tuliotahiri tulifanya kosa, hebu aje mwanamke humu atuambie utofauti wa haya madude ili nisimpeleke mwanangu kwa ngariba mwezi wa Desemba mwaka huu.
Tatizo kwenye kabila langu, usipotahiri utakosa amani hadi utamani kujitoa uhai, hii desturi wanaichukulia kwa uzito mkubwa sana, hata vijana wanaweza wakakuvizia na kupitisha kisu au mkasi moja kwa moja.
 
Waje na humu tz wamejaa kibao hasa hasa wanaotoka kanda ya ziwa bado sana hata kipindi tunafanya bord check jeshini wale waliokuwa wametoka kanda hizo walikuwa wengi sana kwa bahati nzuri yule doctor aliwapitisha lakini nakumbuka baadae baada mafunzo kuisha ile miezi 6 tuu walianza kutahiriwa kule kule tukawa tunawapa kazi ya kulinda hanga ili wapone haraka[emoji2][emoji2]
 
[emoji23][emoji23][emoji23]kwahiyo na wazungusha mikono wamo
 
Inabidi ukathibitishe kama umetailiwa ulete mrejesho MK255
 
Huwa nachukia sana,kuona mtu mzima anayejitambua anashindwa kutoa mkono wa sweta;hata baadhi ya wazungu tunaowaona wamestaarabika...bado wanakuwa na mkono wa sweta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…