Wanaume kupika na kupakua ni ushamba jamani??


BJ naona wanaume wasiotaka kuingia jikoni walikuwa wa mwaka 47 siku hizi wengi hawaoni kama it is a big deal kumsaidia mwenzao katika kazi mbali mbali za nyumbani ikiwemo kupika. Mchana nilikuwa naongea na jamaa basi akaniambia mama kachoka kalala mimi nakorofisha msosi na kufua pia (wanatumia mashine na wote ni Wabongo) na wala alikuwa haongei kwa kusikitika na mkewe huappreciate sana msaada huo. Sasa mwanamke ukiwa na Mume kama huyo uombe nini tena kwa Mungu!? Naomba sana iwe 0-0 maana nahisi bingwa mwaka huu anaweza kuwa ni kwa tofauti ya magoli, sasa nyinyi na Chelsea mmetuzidi kwa magoli hivyo mkitoa sare ya 0-0 nasi tukimpiga mtu bao nne au zaidi tutaweza kupunguza gap ya magoli iliyokuwepo.
 
hakuna kazi ya mwanamke wala mwanaume. biblia ilisema adamu atakula kwa jasho kuna wanawake wangapi leo ni bread winners? na wewe unayepika wakati wageni hawapo unaficha nini? ushamba tu na kutoendelea
 
Kusema mwanamme kusaidia ni ushamba ndio ushamba wenyewe.

Hawa wanawake wanaosema kusaidiana ni ushamba hawako mbali sana na wale wanaosema "mwanamme asipokupiga hakupendi"
 

Mambo ya kusaidiana kwenye ndoa ni muhimu, inapendeza na kufanya wapenzi waone kila mmoja anamjali mwenzie....BAK na hiyo wish yako ya 0-0, haya wee tusubiri wikend vinginevyo jiandae kunipongeza!..Alamsiki!!
 
hakuna tatizo kumsaidia mamaa mambo ya jikoni....tunachoogopa ni maneno yenu kina mama..hamkawii kutuona mume ***** kisa tu tumewasaidieni kupika...
Nakubaliana nawewe. Wengi tunapenda kuwasaidi ila yakianza maneno inakuwa shida kidogo. mara mchoyo, mara anakaba mpaka penati basi ni fulu matatizo. But inshort kuwasadia ni jambo jema tena sana.
 

Mama mia,

Mwanamume kupika siyo ushamba. Ila kuna mambo mengi sana ya kuangalia. Kubwa kati ya hayo ni mazingira mnayoishi na matajario ya jamii. Kama mnaishi Tandika kwenye room 1, mnapikia mkaa kule uani ambapo mnachangia kama familia 10, basi siyo vizuri mwanamume kukimbia kimbia na misufuria ya ugali huko jikoni. Ila kwa kama mnaishi kwenye apartment yenu wenyewe, jiko lenu la kisasa na mambo yenu private hakuna shida.

Mimi ni mpenzi na mtetezi wa usawa katika ndoa ila sidhani kama ni busara kukimbia kimbia jikoni wakati kuna wageni ambao hamna uhakika na mitizamo yao. Sipendi na wala my wife wangu hataki niwe kichekesho mitaani. Kwa hiyo sitaenda jikoni kama kuna wageni.
 
hakuna kazi ya mwanamke wala mwanaume. biblia ilisema adamu atakula kwa jasho kuna wanawake wangapi leo ni bread winners? na wewe unayepika wakati wageni hawapo unaficha nini? ushamba tu na kutoendelea

Unaweza kuwa sahihi ila ukumbuke kuwa biology yenyewe ilishaleta ubaguzi mkubwa. Mmoja anasukumbwa na testosterone wakati mwingine anacheza na estrogen. Matokeo ya hivyo vitu ni makubwa sana. Ndo maana katika michezo kama riadha wanaume na wanawake hawachanganyiki. Kwa hiyo tofauti katika gender ni natural na zimebebwa hivyo hivyo katika tamaduni zetu. Na pale tunapotaka kufanya mabadiliko hatuna budi kwenda taratibu, vinginevyo tutaonekana vituko tu!
 


Point ya tatu ni sahihi sana
 
m.ume kupika sio ushamba....wala ujinga....
hapo ndiyo mnapokosea nyie w.wake!!!!
waume zenu wakiacha hata kuwafulia kufuli zenu mnasema eti wanaboa, sasa mnataka wafanyeje?
 
Mkubwa, nakubaliana nawewe kabisa. Kupika inakuja naturally kwangu, najikuta ninataka kufanya mautundu flani, and it is funny.

BUT, mwanume hauwezi kuwa unaingia jikoni tuu kila wakati kupika "everyday food" mnaweza kukutaa hoja yangu. lakini, mwanaume unatakiwa kupika vitu ambavyo sio vyakula vya kila siku..............unaweza kukaa chini unakuna nazi ili upike wali nazi na nyama??
Mi naona inakuwa fresh kama unafanya mambo flani ya michemsho, mikaango ya maini hivi, misamaki flani.......week end flani watu wana-look foward kuona baba atafanya nini different na chakula cha kila siku.
 
Mkubwa, umenena vizuri kabisa. Tukisema tunapenda kitu fulani, haimaanishi tufanye tuu hata kama mazingira hayaruhusu kulingana na tunapoishi.
 
ni kweli kabisa kamanda... sidhani mleta mada alitaka tupike kila siku... sasa na mengine tutafanya saa ngapi
 
Mkubwa, umenena vizuri kabisa. Tukisema tunapenda kitu fulani, haimaanishi tufanye tuu hata kama mazingira hayaruhusu kulingana na tunapoishi.
kweli bana yaani we ukae jikoni unapika wakati mkeo anapiga soga na mashostito wake dah hii kali...
 
Mmmmng there's nothing wrong with this....i love to have my bfast done by my swtty....and once in a while we cook together!!!
 
Iko haja ya kubadili ladha ya chakula nyumbani,Mwanaume kupika ni safi sana, nimekuwa napika mara nyingi nyumbani kwangu, Lakini Pia nimejifunza toka kwa baba yangu alikuwa mpishi mzuri sana, Siku alizokuwa akikaanga watoto tulikuwa tunainjoi sana.
Japo si wanaume wengi wanajua kupika kutokana na nature yetu ya waafrika kwamba mwanaume Jikoni si mahali pake familia nyingine ukionekana uko jikoni siku hiyo utasema nini kilikupeleka uko.
 

Ni kweli kabisa, hata mimi baba yangu mzazi alipokuwa hai (kwa sasa ni marehemu) siku moja moja alikuwa anaandaa bonge la msosi halafu tunakula pamoja katika familia. Kweli inapendeza sana. Pia hata mimi mwenyewe mtoto wa kiume kuna wakati wazazi wakitingwa sana na kazi na pengine wakati fulani wanakuwa wamechoka, basi hata mimi naingia jikoni naandaa msosi wa nguvu.

Ila si vema sana mwanamke kukaa sebuleni na mashosti zako halafu mwanaume akawa jikoni anapika. Kwa hapa italeta picha ambayo si nzuri kwa hao mashosti zako ambao mkishaagana tu wanabadilika kuwa Radio Umbea. Ila kama mwanamke ni mgonjwa sana na huna uwezo wa kukaa jikoni kwa wakati huo itakuwa sawa maana hata hao mashosti watakuwa wanaiona hali yako.

Halafu kwenye nyumba za kupanga ambako mara nyingi mnakaa uani kupika mfano familia 5 au zaidi, hata 2 si vema kwa mwanaume kukaa na wanawake kupika. Kwa hapo kama mwanamke hajiwezi ni mgonjwa sana, basi mwanaume afanye utaratibu wa kuiomba familia mojawapo za wapangaji hao kumsaidia kupika.
 
kuasaidiana katika maisha ni jambo la kawaida tu hasa kwa mwanamme muelewa
 

Aisee nimependa hiyo kumbe tuko wengi ambao baba zetu walikuwa wanatupikia, Manake kwa marafiki zangu nilikuwa sioni hiyo halafu nilikuwa naona aibu nikija na rafiki home afu tunakuta baba ndo anapika!!!!
 
endelea kuwa na upendo huo kaka wa kumsaidia mkeo,wewe ni mfano wa mwanaume bora.

Avatar hii unaipendea nini? Aaaaaahh nilikuwa nakubipu tu, haya turudi kwenye mada.

Kuna jamaa yangu mmoja hata kupika ugali hajui. Hivyo ikitokea mke wake kapata safari ya ghafla analazimika kuwaomba majirani wampikie ugali/chakula. Duh haya sasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…