Wanaume kupika na kupakua ni ushamba jamani??


and I will always love you B....!!!!
 
Kakangu kule juu......

tehe tehe lakini ASENI WENGA amefulia mkuu
samahani kama nimekukwaza.

Hapana hujanikwaza mkuu..EPL ya mwaka huu ni ngumu mnoo...Ndo maana mpaka sasa inakuwa ni vigumu kujua ni nani atakuwa the champ..Mfano Jumapili ijayo kuna game ngumu kati ya timu 2 za kileleni Man Utd na Chelsea,akifungwa mmojawapo kati ya hawa na siye tukashinda tunapunguza gap na kuwa na ama tofauti ya point 2 ama 1 kwa aliye mbele yetu....So ni mapema mno kusema Wenger kafulia though alichemsha mbaya Jumamosi kwa kuwaweka benchi Nasri na Arshavin na kuwaingiza dakika za mwisho...Pamojah
 
and I will always love you B....!!!!

Mhh B,

Mi naanza kuogopa. Nikisoma btn lines sipati kitu, kwani wanaume wengi wako tayari kupika ila mara moja moja tu!! Mimi naweza kupika wakati wowote endapo sijabanwa mbavu na kazi za kubeba mabox.

Hata hivyo kama tunaishi uswahilini siwezi hata siku moja kuingia jikoni. Ikibidi nitapikia hata uvunguni, tena mlango umefungwa. Wambeya wanaweza kunigombanisha na wife kwamba amenipa limbwata. Sitaki hicho kitu wakati bila my wife mimi sina life.
 
kwangu mimi mpaka sasa ndio mpishi mkuu wa nyumba yangu,mama yeye ni siku mojamoja,
 

Unaogopa Balantanda kunisaidia kupika? (sijui kama ni kunisaidia au....)

kwetu hilo ni jambo la kawaida sana na nimojawapo ya spice kwenye mapenzi yetu yanayozidi kushamiri......
 
kwangu mimi mpaka sasa ndio mpishi mkuu wa nyumba yangu,mama yeye ni siku mojamoja,
Uwnaume ni kuhakikisha kuna ugali mezani................Mkuu, haimaanishi ununue unga na kupika upike wewe.
tehe tehe!! paoja mkuu
 
Kidume lazima uchome nyama home, misamaki ichomwe,,,,,,,,watu walio kwenye nyumba yako wajue kuwa, hivyo vitu sio vinapatikana bar tu!

Nakubaliana na wewe [bold/U]. Moja ya mambo yanayokamilisha pendo langu kwa mke wangu ni jinsi anavyoandaa maakuli! Nikiingia mwenyewe jikoni najisikia kuwa "abandoned"!
 
Huo ni mfano wa mgawanyo wa kazi ulivyokua huko mwanzoni. Kwa hapa mjini naweza kupiga pasi nguo au kumbembeleza mtoto ili wife awe na muda mzuri jikoni. Kuna shughuli za jikoni mwanaume unaweza kufanya wife akiwepo - kutengeneza juice, kuchoma nyama au kuchinja kuku/mbuzi n.k
 


i salute you,umemaliza yote
kupika mwanaume sio ushamba,sio limbwata,sio option (eti adi mkewe aumwe)nk
ni mwanaume aliyelelewa vyema kwao basi!!
 
Unaogopa Balantanda kunisaidia kupika? (sijui kama ni kunisaidia au....)

kwetu hilo ni jambo la kawaida sana na nimojawapo ya spice kwenye mapenzi yetu yanayozidi kushamiri......

Hapana da B,

Naogopa mnapoanza kwa kusema anatoa msaada, halafu na yeye anasema kuwa hupika mara moja moja tu. Halafu hatujui ni kila baada ya muda gani. Labda ni mara moja kila baada ya ya miaka kama 5? Lakini pia sijui kama utajisikia poa tu mzee akakae kwenye kigoda uani, katikati ya wanawake kama 10 hivi (huko Tandika) akitengeneza ugali au wali wa nazi. Kule kwetu Tanga anaweza pia kukaanga uwono?? Bado nipo nipo tu!
 
Unaogopa Balantanda kunisaidia kupika? (sijui kama ni kunisaidia au....)

kwetu hilo ni jambo la kawaida sana na nimojawapo ya spice kwenye mapenzi yetu yanayozidi kushamiri......
Kwenye swala la ksaidiana nalikataa kabisa!!
Sipiki kwa kumsaidia wifey wangu! napika kwasababu
1) Napenda kupika vitu flani flani.ambavyo ni tofauti (mfano choma nyama)
2) Nataka familia yangu ile vitu ninavyopika siku moja moja
3) Kuna vitu sio wife wala msichana wa kazi anaweza kupika........inakuwa ni usumbufu kuwaelekeza.
4) wote walio nyumbani kwangu wanafurahi sana nikisema leo msipike nitapika (wana-expect mambo ya maana ile mbaya) inaleta furaha.

Sipiki kusaidia.............kusaidiana kupika maana yake nini? mimi napika ijumaa, yeye anapika alhamisi au?
 
Na mimi hapo ndo sikubali kabisaaaaa!
sitoi msaada wa kupika........labda misaada mingine.
Napika mara moja moja, na sio kumsaidia wife
kwanza wake wenyewe hawa.......hawaingii kitchen hata siku moja, utasikia, upike ugali na kitimoto............kachumbari uweke pilipili kidogo....anaita akiwa sebuleni. Msichana wa kazi ndo anafanya yote.

waiiiiii!!!!!!
 
 

brilliant question........ila silijibu mapaa baadae!!!
 
 

Hausaidii,bali mnasaidiana(that's what i said)..Ni sawa na kusaidiana katika matumizi ya home,kusaidiana kufua nguo...Nk...Ndo maana nikasema mimi(maana ishajengeka,hasa Tanzania na Afrika kwamba wababa wao hupikiwa tu ama na mke ama na house maid) so narudia tena mimi mara nyingi weekend huandaa chakula twala mimi,mke wangu na mtoto wetu pia na msaidizi wetu wa kazi za nyumbani...So si vibaya kusaidiana kupika bana(narudia tena kusaidiana kwa maana ya kwamba kila mtu ana wajibu ya kupika,simaanishi kufuata ratiba hapa)
 
"Astaghfirullah-al'azim allazi la ilaha illa huw-al-hayy-al- qayyuma wa atubu ilayh"
Dah! Ndio tumefikia huku?

Ngoja nirudi zangu jikoni sorry I mean kaunta! Mi kupika? Hapana jamani😕
Nisameheni bure.
 
Sawa nimekusoma.............mnasaidiana
tofauti hapa ni kewamba mimi nina passion ya kupika vitu flani flani....for the family na ndo maana kuna wakati nikisema nitapika, ninaulizwa utapika nini? kama unapika nanihiii.(sikisemi hapa) niwashtue na wakina flani waje kushinda huku leo?

(mkuu, 90% ya wakina dada wanaofanya kazi ziwe za kuajiriwa au kujiajiri ambazo zipo tight.........hawaingii jikoni kabisa, wasichana wa kazi ndo wanapika, sasa wewe ukisema mnasaidiana, unakuwa unasaidiana na msichana wa kazi au?)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…