Kumbuka kuoa au kuolewa ni kwamba umeamua huyo ni wa maisha yako yote awe dokozi au kikojozi, lazima uwe makini na mtulivu kufanya maamuzi.
Ukiona mwenzio anataka kutoka mbio, usiingie kichwa kichwa! Lazima uchungulie kulikoni.
Only that na wala si uoga!!
chanzo ni nyinyi wanawake!wapendwa naomba mnisaidie kwa hili, kwanini wanaume ni waoga sana kuingia kwenye ndoa? yani hata kama mmeishi pamoja ikija kwenye suala la ndoa ni kupiga kalenda tu, ni kwanini inakua hivyo? je anakua hana mapenzi na mwenzi wake lakini anaendelea kudanganya kuwa anampenda?
Just a second!:smiling::smiling:na inachukua muda gani mpaka mtu aamue kwa dhati?
na inachukua muda gani mpaka mtu aamue kwa dhati?
Just a second!:smiling::smiling:
very possible....Duuuuh!
ni kweli nyamyao hata mi ningeshauri hivyo lakini kuna wale ambao hawakupata ushauri huo na wako hivyo sasa
Mkiingia ndani ya ndoa unyenyekevu wote unaisha, mwanaume anahitaji kujiridhisha kwamba sasa yupo tayari kumtunza mwanamke, kutunza family na majukumu mengine ya ndoa. kwa miaka ya sasa wanaume wengi hupenda kujikamilisha kielimu, kifedha wengine haoi mpaka apate degree, masters kwa sababu nyie wanawake wa sikuhizi mnapenda sana raha na starehe, usipokuwa na kazi nzuri tabu, huna gari dharau utazipata, wenye magari watasifiwa kila siku. nakumbuka rafiki ya bro wangu alikuwa na wife wake wa ukweli mno acha tu, bro akanunua chaser mayai miaka ya 98-99, bro alikuwa bd hajaoa, wife wa jamaa alikuwa haishi kumtaja bro na alikuwa akija hm kuazima gari, yule rafiki wa bro alipoona hivyo akaamua kuiba kazini kwao, na yeye akanunua corrola lkn mwaka mmoja baadaye jamaa akasimamishwa kazi, kesi ikachukua mwaka mzima jamaa akatemwa job, hivi vitu ndo vinatufanya tuwapige kalenda, ili kesho na keshokutwa usianze kunigeuka tena. na nyie muache kulazimisha acha mtu ajiandae
napend akuwashauri wadada wackubali kuishi na mwanaume bila kutangaza nia inayoeleweka kwanza.
kumbe ndio hivyo! basi labda anaogopa majukumu huyu?
Hiyo SEKTA ina ugumu wake.. Ni lazima kuamua kwa dhati unapoingia, Kwani ina mlango mmoja tu wa kuingilia.. Ukisha ingia, Kutoka hakuna...
na hawa wanaume bwana! sasa una watoto wa 4, unasubiria nini tena? cha ajabu anaweza kuja kutangaza nia kwa mwingine kabisaaaa..hapo ndipo ninapowachoka.