Wanaume na tezi dume

Wanaume na tezi dume

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Tezi dume si ugonjwa bali ni kiungo miongoni mwa viungo katika mfumo wa uzazi wa mwanaume,ipo chini ya kibufo cha mkojo

Ni wakati gani tezi hii huwa ni tatizo? Ni pale ambapo tezi dume inakuwa au inaongezeka kutokana na umri kitaalamu inaitwa benign prostatic hyperplasia,kadri mwanaume anapoongezeka umri ndivyo uwezekano wa tezi hiyo kukua au kuongezeka

Na inapoongezeka basi huuminya mrija wa mkojo na kuleta dalili zifuatazo,kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku,mkojo unatoka taratibu sio kwa kasi ,vile vile mkojo haumaliziki wote katika kibofu na hivyo kumfanya mhusika mara kwa mara kuhisi kwenda haja.

Inasemwa asilimia 50% ya wanaume wenye umri wa miaka 51-60 wana nafasi kubwa ya kupata tatizo hili,na asilimia 70% wanaume wenye umri wa miaka 60, na asilimia 80% ni kwa wanaume wenye umri wa miaka 70 na kuendelea.

Familia yenye historia ya changamoto ya tezi dume huchangia sana uwezekano wa mhusika kupata tatizo hili.

Lakini habari nzuri ni kwamba ugonjwa huu hausababishi kupata cancer ya tezi dume labda kwa wanaume ambao wana umri mkubwa sana kuanzia miaka 75-80 na hii ipo kwa asilimia 80%.

Soma Pia: Je, kumwaga mbegu za kiume mara kwa mara nikinga dhidi ya saratani ya tezi dume?

Ugonjwa huu wataalamu wanasema una tiba za kufanya kibofu kilegee na kufanya tezi dume isinyae na huduma za upasuaji labda kama tatizo limekuwa kubwa sana ndio hapo upasuaji utahusika,na siku hizi kuna namna ya kukata mshipa wa damu usiende kulisha tezi hiyo na hivyo kuifanya isinyae na isikue

Na kibongo kibongo kuna shuhuda nimesikia za kutumia majani ya mstafeli yanasagwa na kisha juisi yake inanywewa na tatizo linaisha

Sasa tuje kwenye point muhimu ambayo ndio lengo la andiko langu hili,,wanaume wenzangu iko hivi,wataalamu wanasema kwamba shughuli ambazo zinafanya mwili utumie nguvu ikiwa ni pamoja na mazoezi zinachangia sana kuepuka tatizo hili.

Kinyume na sedentary life style ambayo mtu haushughulishi mwili wake,yaani mtu huyu hata kutembea mwendo mrefu ni shida,hana movement za hapa na pale,mtu kama huyu ana asilimia kubwa sana kupata tatizo hili katika umri wa 51-60

Hata wale ambao tupo kwenye 40's tusirelux,si unajua life begins at 40's,kwahiyo tuachane na sedentary life style,najua watu wa mandinga mpo humu,kutoka home kwenda job ni ndinga,ukifika ofisini unatumia lift,halafu ukikaa umekaa,na ukitoka kama ulivyokuja

Haya sio maisha mazur kwa ajili ya afya yako,tufanye mazoezi jamani,nasisitiza tufanye mazoezi kwa faida yetu wenyewe,ili tuepuke baadhi ya changamoto za uzeeni.

Ni hayo tu!
 
Back
Top Bottom