Wanaume na vituko vyao.


Haaa haaa ndito watakukaba.
 
Unajua hapa ume-generalize na kutoa conclusion mwenyewe.... ukisahau kuwa wanaume wengi wanaofanya vituko hivyo nyuma yao kuna wanawake. Na siku zote aisifiaye mvua imemnyea, kama una tatizo na mwenzi wako leta jamvini tukusaidie kwa ushauri....:kev:
 

Chauro,

Post yako imejisimamia kiasi cha kutosha.

Naomba tu niongeze kwamba, watu wanahangaika saaaana kutafuta na ku-list makosa ya wenzao. Inafikia mahali hata makosa yao wenyewe wanawatwisha wengine. Hili ni jambo la hatari sana katika mahusiano. Kila mtu ni mtenda dhambi sema hatuwezi kuitisha press conference kuzungumzia dhambi zetu wenyewe. Ni vizuri tukapunguza matope tunayowapaka wenzetu kwani hata sisi tunaweza kuwa tumechafuka kama wao au kuwazidi!
 
Mkuu hiyo picha kwenye avatar yako ilipigiwa kijiji gani? Inanikumbusha mbali sana!
 
wanaume siku zote wako sahihi na ikitokea wamekosea kusamehewa ni haki yao ya msingi
 
ivi kama mngebaki wanawake wenyewe hapa duniani, mngekuwa mnatembea uchi? hayo manywele ya wafu mngekuwa mnavaa? suruali za kubana mngemvalia nani?
Lakini jibu lipo, waangalie wanapoenda kwenye vicheni party, wanavaa vizuri, lakini wakienda kwenye mikusanyiko mingine ambapo wanaume wapo waone nguo zao! kama hawajitambui hawa watu, ona wanavyochezeshwa uchi kwenye makumbi ya starehe huku wanaume wamevaa vizuri,
kweli Mungu alimuumba mwanaume kwa mfano wake na kumfotokopy mwanamke toka kwa mwanaume .
 
wanaume siku zote wako sahihi na ikitokea wamekosea kusamehewa ni haki yao ya msingi

Tena jaribu umfumanie, atakuomba msamaha utamsamehe, yeye akifuma wewe mfano, unajua kinacho fuatia hapo hataulie kama nini ni basi tena hakuna la zaidi ni unaachwa.
 
heee subhana llah... hii topic basi tena...lol..
Tena jaribu umfumanie, atakuomba msamaha utamsamehe, yeye akifuma wewe mfano, unajua kinacho fuatia hapo hataulie kama nini ni basi tena hakuna la zaidi ni unaachwa.
:A S kiss:
 
Ubinaadamu ni mapungufu
jicho la kwanza huona mema
jicho la pili huona kasoro
Moyo nao hutamani
ubongo huyumbayumba na kufanya maamuzi tofauti na yule jicho wa kwanza,zaidi utabias kwa jicho la pili
 
mwanaume huyo huyo akiwa na pesa wanawake wanajipanga kama magari kwenye traffic light...hahaha
mwanaume huyo huyo anawafanya mjifanyie plastic surgery na botox kibao!...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…