Duuh yaani hata kabla sijafafanua hoja, mnaanza kunifokea!?
Anyway, ukweli ni kwamba dunia hapo kale ilimtambua mume kuwa Kichwa Cha familia! Kiukweli kwa uhalisia wa nyakati zile Ilikuwa sahihi kwa 100%
Mwanamume alibeba sifa zote tatu za msingi za kuwa mkuu wa familia, ambazo ni umiliki wa uchumi, umiliki wa akili pevu, na nguvu za mwili.
Nyakati zile haikuwezekana katu mwanamke kumiliki uchumi wowote. Hakumiliki mifugo Wala shamba, hakuruhusiwa kufanya kazi za biashara Wala ufundi, na kamwe hakuruhusiwa kwenda kuwinda nguchiro, swala hata kutega mitego ya kanga Wala kware shambani.
Kwa hali hio mwanamke asingeweza kamwe kutunza familia wala kujitunza mwenyewe!
Wanawake hawa walikuwa wakifiwa na waume wao, huishi maisha magumu Sana na Hadi manabii nyakati zile wakaleta maandiko ya kuhimiza kusaidia wajane, maandiko ambayo kwa Sasa ni outdated!
Kuhusu akili pevu, kwa mwanamke nyakati zile haikuwa Jambo rahisi kutokea!
Akili hujengwa na kuimarishwa kulingana na mfumo wa maisha ambao mwanadamu hupitia!
Maisha ya mwanamke nyakati zile hayakufungamana na Harakati za utatuzi wa changamoto za maisha.
Jamii ilimsuka mume kuwa mpambanaji wa changamoto, hivyo akili yake ikawa inapevuka kila siku.
Mwanamume alikaa kutafakari ufugaji, kilimo, biashara, uwindaji, utawala hadi mapambano ya Vita.
Mwanamke aliwekwa pembeni, na akawa mlezi wa watoto.
Yeye ni kuishi utoto na vitoto nyumbani hivyo akili ya mwanamke ikawe haipevuki.
Hapo nyumbani ikitokea hitilafu yoyote ataitwa baba haraka.
Baba ndio afikiri kupata ufumbuzi wa tatizo. Hii Hali iliendeleza kudumaza ubongo wa mwanamke
Kuhusu nguvu za mwili, pia mifumo ya maisha ilimnyima mke kujiimarisha. Wanawake hawakuruhusiwa kazi za nguvu zilizowapa tija waume kujenga miili yao!
Hata hivyo ingawa hoja hii ipo kibaiolojia zaidi, lakini ukosefu wa majukumu ya nguvu yalizidisha ulegevu kwa mke, ingawa kibaiolojia asingeweza kuwa juu ya mwanaume kwa ulinganifu wa mabavu!
Leo hii dunia imeshahama huko, tupo mbele maili nyingi Sana!
Kichwa Cha familia Leo hii si issue ya jinsia Tena, Bali sifa tatu nilizoainisha, ambazo nyakati zile zilikuwa sifa za kiume na hivyo mume kuwa Kichwa Cha familia bila kupingwa!
Kutunza familia kunahitaji nguvu ya uchumi. Leo hii uchumi unamilikiwa na yeyote.
Mke anaweza kuwa Bora kiuchumi Mara kumi ya mwanaume.
Mke aweza kujenga nyumba, kununua na kuendesha kilimo, kufanya biashara, kuendesha ofisi za serikali ama binafsi.
Katika mazingira hayo mume unapata wapi uhalali wa kujitangaza kuwa Kichwa Cha familia? Huna haya?
Maisha Leo hii yanaibua na kupevusha akili za mwanamke pia. Mtoto wa kike Leo hii anashiriki nyanya mbalimbali za maisha zinazomfanya kuimarisha akili yake. Uwezo wa kufikiri Leo hii ni kwa jinsia zote. Mwanaume Hana hati miliki Tena ya Akili.
Mume upo na mke mwenye uwezo wa kufikiri Mambo zaidi yako, unatoa wapi nguvu ya kujitangaza kuwa wewe ni kichwa Cha familia?
Kuhusu nguvu za mwili, si tena factor ya msingi kwa ujenzi na utunzaji wa familia. Nguvu itabaki kuwa sehemu ya kipaji Cha kazi za shamba, au vibarua barabarani au viwandani
Hivi, jamani, madam wetu president, madam speaker na wanawake wengine wa kaliba yao, mume anapata wapi nguvu za kutangaza ukuu wake hapo ndani?
Kwenye nyumba Kama hio wewe mwanamume ni Nani hasa? Provider, planning officer, family guide, family security officer,? who are you to declare the head of family?
Waume lazima tukubali, status zetu za kiuchumi na intelligence ndizo zitaamua kwenye ndoa zetu tuwe kichwa ktk familia, au mwenza ktk familia.
Kuna wanaotoa ushauri humu ndani kuwa mwanaume asioe mke aliyomzidi uchumi au akili. Ni kweli iwapo objective ya kuoa ni kuwa Kichwa Cha familia.
Ukimuoa mke amekuzidi, uwe submissive tu. Hakuna shida, ilimradi bidada yupo tayari kukufanya mwenza wa maisha.
Shida yetu waume ni kukariri kuwa sisi haki yetu ni uboss kwenye nyumba. Ukitaka uboss oa yule ambaye kweli utaonesha uboss wako kiuchumi na kiakili.
Mwisho wa siku, Mimi niseme kwamba,
1)Dunia ya leo Kichwa Cha familia ni yeyote anayestahili
2) "Mwanaume ni provider" ni outdated philosophy!
Yeyote ni provider wa familia, iwe baba pekeyake, iwe mama pekeyake au kwa ushirikiano wao kwa viwango sawa au visivyosawa kutegemeana na hali zao.
3) Mahari zifutwe! Ndoa iwe muungano wa hiari wa kujenga familia.
Mahari bado inabeba dhana kuwa mume Ni kichwa, na kwamba yeye ndiye anakwenda kuiendesha familia, na mke anawajibika kwake kwa utiifu wote kitu ambacho hakipo.
Wanawake si watiifu Tena, na possibility ya mume kuwa Kichwa Cha familia ni ndogo Sana.
Misingi ya ndoa za kale imevunjika vipande vipande.
4)Mwanaume kwa Sasa oa kwa ajili ya familia na sio kwa ajili ya mke. Jenga ngome ya ukuu wako na si kuamini kuwa umezaliwa kuwa mkuu wa familia.
Hakuna mke anamheshimu mume kwa sababu ya uanaume wake. Bali utaheshimiwa kwa uchumi wako na akili zako.
Uchumi na akili ndio nyenzo ya kuwa Kichwa Cha familia!
5) Zipo familia nyingi tu, mke ndio kichwa Cha familia!!