coder12
JF-Expert Member
- Dec 28, 2016
- 253
- 2,303
Ukishakua mwanaume tu, tayari familua wanakusubiri ukue uwakomboe, jamii inakuangalia wewe. Ukiwa na mwanamke au ukioa unategemewa kwa vitu vingi hata kama huyo mwanamke anajiweza. Wengi wetu tunaishi maisha tusiyoyataka na kufanya kazi tusizozitaka ili mradi tu haya majukumu tuweze kuyatimiza. Baba kwenye familia huwa thamani yake haionekani sana, hakuna anaejua wala kujali ni kiasi gani amejinyima na ndoto zake nyingi ameziua ili tu familia iwe sawa. Watoto wanampenda zaidi mama kwa sababu baba mara nyingi hayupo karibu. Hawajui kuwa ndo ameenda kutafuta. Mtoto wa kiume ukishapata mtoto ndo utaelewa baba yako alikua na mchango gani mpaka umefika hapo ulipo.
Kwa mwanaume, sio mvulana(boychild) asilimia 80 kama sio 90 ya kipato chako ni kwa ajili ya watu wengine, hiyo inayobaki ndo ujibalance usurvive nayo. Halafu wanajiuliza kwanini wanaume tunakufa mapema.
Tunywe bia tutoe stress tu