siyo kila Hoteli ina masink WC kwa taarifa yako mimi nwenyewe nilishuhudia jamaa Pale mnazi mmoja akisukutua na kutema mate wakati wengine tukila chakula.
Hahahahahaaaaaaa! Jamani na wewe Rose una maneno!!!! Hivi ni demu kweli wewe au kanyanga???? Huyo bwana ako kala hasara.kwan tukifutua ndo iwe matangazo? yaaan kikitu kiduchu cha kumwambia ehh bwwana ehh ni ivi stak vile lijitu la kiume utaliona limeleta jf tujadlil..
Kuna Mambo sisi wanaume lazima tuyaache na tujue jinsi ya kuwa wasafi.
1. Mtu soksi zinanuka kwa sababu ya kuvaliwa kwa muda mrefu haoni kama ni tatizo
2. Hotelini mtu anasukutua na kutemea mate au kohozi kwenye sink linalotumiwa na watu wote. raha mustarehe
3. Una Soksi ina bonge la tobo kwenye kisigino na kwenye dole gumba lakini bila ya aibu unaivua mbele za watu.
4. Unaingiza dole lako kwenye pua na kutoa Kamasi au ugando wa kamasi bila ya wasiwasi mbele za watu
5. Unafanya kazi Gereji hufui nguo zako hadi tofauti kati yako na Grease za gereji inakuwa sawasawa na Ziro
6. Unajijua una kikwapa lakini kunyoa nywele zako za kwapani inakuwa ni mgogoro mkubwa.
7. Unakula kitimoto, unakunywa bia na vitu vingine kadha wa kadha,lakini mswaki kwako mwiko!
8. Huwezi kuoga mpaka ujue unakwenda kwenye kideti kipya.
9. Domo lako unajua kwamba linanuka lakini wewe ndiyo kinara wa kutaka kunong'oneza watu.
Hizi ni tabia ambazo baadhi yetu wanaume tunazo ila wengine wanazitetea eti ndiyo "udume" jamani tuwe wasafi kwani usafi nao ni sehemu inayochochea mapenzi.
Mashallah! Bi mkubwa wangu hapo kwa Gozi lako umenikongaMie nna addiction ya harufu ya mume wangu silali mpaka niinuse, akisafiri huwa natafuta Tshirt zake nnalalanazo chini ya kichwa, sizifui makusudi, niipate tu harufu yake. Kumbuka hanuki ananukia kama misk, MashaAllah, Mungu aniwekee Gozi langu.
Usafi ni katika imaan. Mwenye imaan ya kweli awe mwanamme awe mwanamke hanuki hata chembe, kwanza Waislaam wenye imani yakini huswali (kwa uchache) swala tano kila siku na kila swalaat lazima uwe na udhu, huo mnuko utatoka wapi?
Heeheeheeee! Mkuu wa ndimu, hakikisha umebeba ndimu mda wote! Akikulazimisha tena kwenda chumvini unakamulia ndimu kwanza...!!! Heeheee mapenzi ya kuiga yana balaa, yaani ananuka kunako lkn bado anakulazimisha ulambe vitu?????jinsia zote tu kuna haya matatizo! kuna wadada pia makwapa yao yanatema halafu unamkuta kavaa kibrauzi vikwapa viko inje inaboa na wale unakuta hadi kwenye shati kuna ramani!
namidomo jinsia zote wapo wanaonuka midomo!
wanaboa unakuta mtu anakomaa umpe kiss ya mdomo wakati domo linanuka kama choo cha shimo!
wanawake nao kule chini niwachafu pia mtu anakomaa kukuvuta chumvini wakati kunaharufu aaaaaaaggghh!
wote tuwe wasafi naukimuona jamaa/rafiki ananuka domo au sehemu yoyote mwelimishe!
Kufloss ndio nini tena jamani maana ulivyokazania...nahitaji kujua tafadhaliWana floss na nini? Toothpicks?
kweli bwana nilikuwa namaanisha mgahawa ingawa si ule wa mama ntilie bali ni "Restaurant" kwani kwa vigezo vya walioendelea kila kitu huku utakiona ni shaghalabaghala!Kigarama naamini unamaanisha MGAHAWA.
Manake kule kijijini kwetu hata banda la mama lishe twaita HOTEL.
Otherwise nitajipima kupitia list yako nione wapi nachemka, manake mambo haya bila wito ni kazi ngumu kweli.
kusafisha kinywa kwa vifaa maalumu vilivyothibitishwa au kuwa na aina fulani ya madawa yanayoua baadhi ya "wadudu" kinywani. Kinywa ndiyo sehemu yenye wadudu wengi kwenye mwili wa binadamu.Kufloss ndio nini tena jamani maana ulivyokazania...nahitaji kujua tafadhali
Kuna watu kwa asili wana kikwapa na kikwapa ni ugonjwa wa ngozi na wataalamu wa magonjwa ya ngozi dermatologists wanajua jinsi ya kushughulika nalo. Tatizo kuna watu wanajua kabisa wana kikwapa lakini kwa vile wanajidai wako Bize basi kunyoa ni mpaka watu wawe wameshapiga sana chafya kwenye daladala.
Hao wanaume wenye tabia hizo ni wa huko kwenu,.....ambako hakuna maji,sabuni,maduka ya kuuza miswaki na dawa,hakuna leso,...etc,..huku kwetu hayo mambo hayapo_na hao kina Preta na Rose1980 wanao kussuport nafikiri mnaishi nao huko...waambie waje kwetu wataona tofauti
Kuna Mambo sisi wanaume lazima tuyaache na tujue jinsi ya kuwa wasafi.
1. Mtu soksi zinanuka kwa sababu ya kuvaliwa kwa muda mrefu haoni kama ni tatizo
2. Hotelini mtu anasukutua na kutemea mate au kohozi kwenye sink linalotumiwa na watu wote. raha mustarehe
3. Una Soksi ina bonge la tobo kwenye kisigino na kwenye dole gumba lakini bila ya aibu unaivua mbele za watu.
4. Unaingiza dole lako kwenye pua na kutoa Kamasi au ugando wa kamasi bila ya wasiwasi mbele za watu
5. Unafanya kazi Gereji hufui nguo zako hadi tofauti kati yako na Grease za gereji inakuwa sawasawa na Ziro
6. Unajijua una kikwapa lakini kunyoa nywele zako za kwapani inakuwa ni mgogoro mkubwa.
7. Unakula kitimoto, unakunywa bia na vitu vingine kadha wa kadha,lakini mswaki kwako mwiko!
8. Huwezi kuoga mpaka ujue unakwenda kwenye kideti kipya.
9. Domo lako unajua kwamba linanuka lakini wewe ndiyo kinara wa kutaka kunong'oneza watu.
Update:
10. Mtu mkewe akisafiri wiki nzima basi na yeye hatandiki kitanda chake wiki nzima. Huo ni u-smart au ni uchafu?
11. Kila ukikutana na kichochoro au kigiza kidogo, mzee lazima umwage "kojo" tena lenye harufu kali. Jiheshimu!
Hizi ni tabia ambazo baadhi yetu wanaume tunazo ila wengine wanazitetea eti ndiyo "ugumu" jamani tuwe wasafi kwani usafi nao ni sehemu inayochochea mapenzi.