Wanaume wa JF...Ngoma zisizo na mdundo mnazocheza nasi kutwa kucha huko Pm, ipo siku zitapasuka. Wanawake Tumechoka sasa!!!

DaJane

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2012
Posts
223
Reaction score
622
Hodi humu jamani!!!
Msishangae kuja usiku wa manane.
Yamenifika hapaaaa!!!
Kila nikilala usingizi hauji.
Khaaa!!!!

Sasa leo mie ujio wangu nimekuja na jambo moja tu kuhusu baadhi ya wanaume wa humu Jf na hii tabia ya kushinda na msuli na boxer Pm kwetu sisi wadada.
Najua ujumbe huu watausoma kimya kimya shurti na kashda wala chagizo.
Hivi, mliambiwa sifa kubwa ya mwanaume ni kumjia mwanamke Pm?

Jamani wanaume hebu punguzeni majotrooo na tunaomba mtupumzishe, maana nimetumwa na wanawake wenzangu niwaambie kuwa wamechoka kujiwa Pm bila sababu za msingi, TUMECHOKAAAA.
Cha maana mnachojia hakuna,
La maana mnalosema hamna, mnabaki kutoa salamu mwanzo mwisho, aliyesema tunataka salamu zenu za mkono mmoja nani?
Kanisani kwenyewe baada ya misa sadaka, msikitini baada ya swala sadaka...haya nyie yapi yamewakuta?
Tena humu kuna wanaume maarufu kutwa kulala na kuzurura kwenye Pm za akina dada, ndio maana wengine profile zetu ziko private, mana ukichungulia tu ukamuona Jane yuko online, huyoooooo unakimbilia Pm na pua lako pana kama sketi ya solo.

Jamani eeee, mtaula huu na hasara juu....baadhi ya wanaume jiheshimuni, Pm hukatazwi lakini uje na jambo la maana, sio unakurupuka tu mbio kuja Pm, ukikuta nimevua nguo je!!?

Halafu sasa kuna wanaume ni ving'ang'anizi hao, mwenyewe utaomba poo.
24/7 yuko macho juu juu kama mwanamke aliyebandika kope kusubiri kwenda Pm kwa mdada, ukiwasha tu data, huyu hapa mlangoni kwa pm, jamani mbona sina raha na bando langu?
Bando huninunulii
Ila kutwa utataka tushinde tunachat Pm.
Unajua aliyeninunulia bando?
Unajua aliyenunua simu?
Tena wengine utasikia anasisitiza kabisa "mie sitoki pm"
Jamani, mbona mnatuweka roho juu juu kama tumejamba ukweni?
Tunakuwa hatuna amani kama tumevaa vigodoro?
Bando langu na simu ni yangu.
Nikitaka nachat na wewe na nisipotaka usinilazimishe,
Afu kitu ambacho hamjui ni kuwa wengine tuna mababy daddy zetu na ma-sponsor wetu humuhumu Jf, sasa wewe unasema live kuwa twende Pm, danga langu akiona je,

Please tuheshimiane, mjini cha bure salamu
Bando huweki kazi kupiga chapuo tu.
Ndio maana wengine conversation zetu tumefunga kwa tabia yenu hii ya kuja kulala Pm.
Acheni ushubwada.
Acheni kutukosesha amani huko Pm jamani.
Wengine tumetega nyavu huko.
MNATUCHEFUA.
TUNACHEFUKWA NA NYIEEEE!!!

Kuchat na wewe Pm sio sheria.
Hivyo nahitaji uhuru wangu.
Usinifosi tuchat wakati sina mood na wewe.
Tukichat jukwaani inatosha, sio mpaka tukalambane lambane Pm.
Tuacheni, tutachat na hizo fataki zinazolipuka hapo uwanjani maana ziko mpaka Pm...tutachat nazo
Wanaume mnaopenda kutumendea Pm nawapa habari, habari ndo hiyo.
Ujumbe huu uwafikie popote mlipo.
Simu inakuwa nzito kwa kujaziwa mi-pm.
Basi hata siku moja uteleze unirushie kavocha, hakuna.
Acheni kupenda dezo.
Acheni kitonga.
Acheni kutuchefua.
Acheni ukwakwasu.
Acheni kudandia mlenda.
Acheni ushubwada.
Tena wanaume wengine na heshima zao ila kwa screenshot hawajambo, ukijipindua ukachat nae tu ujue utazikuta screenshot zako mtaa wa 7 zimesimama dede kama mwanamke aliye period!!!
Jamani zama zimebadilika sio kila homa ni malaria,
Acheni tule sikukuu kwa amani.
Acheni tufunge mwaka kwa amani jamani.
Mbona wengine wanakuja kistaarabu tu na wakishachat tu wanaenda, nyie mnaojenga kambi na maturubai juu mna matatizo gani, mnataka kutulilia matanga?
Au tuwaingize kwenye vicoba?
Afu cha kushangaza sasa, unaweza kuta mwanaume mmoja kwa siku anatembea zaidi ya kilomita 100 kutoka Pm hii kwenda nyingine, ila jukwaani humuoni, kutwa anamiminika jasho Pm,huchoki?
Mtaja fia njiani mzikwe na Manispaa bila mashada wala pambio.

Mie ya kwangu leo ni hayo tu.
Ujumbe umefika japo mtapinga.
Pingeni kwa hoja.
Mwenye kuelewa aelewe na asiyeelewa acha aelemewe.
Ndio maana wengine tunaweka avatar za matunda maana tukiweka hata za akina Jlo bado tu mtakuja Pm.

Alamsiki.
Narudi kulala.
Povu lenu nalikusanya nifulie mashuka asubuhi.
 
Mkuu wanawake wangapi wamekutuma uwaongelee??
Mbona kuna maada hapa mwanamke mmoja alilalamika hatuwatongozi PM?
Kama watu wanakufwata pm jiongelee mwenyewe uwakataze lakini usiwaongelee wanawake wote as if wewe ndio matron wao..

Mbona wengine tumeng'oa mizigo ya maana pm kama unafwatwa na watu usiowataka labda ndio hadhi zako aiseeh
 
Uzuri ni kuwa wenzio huko pm wanatuma picha zao kibao kwa wanaume tofauti wengi humu wapo kutafuta mabwana. Mtu kaolewa lakini mpaka saa 7 usiku unamuona yupo humu unadhani anahangahika na nini?. Pm hamna mwanamke mwenye bwana mmoja humu
 
Mleta mada, aka DaJane pole kwa yalokusibu.

Nje ya mada, naweza kupata wapi hiyo mishumaa kwenye avatars yako. Nataka niitumie kwenye keki ya Valentine 2019.

Kurudi kwenye mada, ujue kati ya ID zinazokufata za kiume nyingine za kike. Uzoefu wangu mie, wamwkuja wengi tuu na kule nawapa ukweli wangu wote na kama wana screenshot shauri lao sababu wote wanaokuja jibu ni lilelile..... Euro 900 na kuendelea....

Hiyo mishumaa tafadhalinaihitaji sana, napenda sana kuchezea zile goroli.... Hehehehhee.
 
Pumbavu kweli..! wewe nae kuna mtu atakuwa ameoa au anapanga akuoe aweke ndani kama mke, kweli wanaume tumeumbwa kwa mateso..!
 

Binafsi nakereka sana na hii tabia
Halafu ID zenu mnazificha mnakuja na mpya

Mtu kuwa straight ueleweke ni unajaza inbox na salamu!?? Wtf
 

Kuna dada anatengeneza mishumaa labda unaweza kumpa order ya shape unayotaka
 
Tafadhari lipia tangazo lako, Na hongera sana kwa ubunifu wako huu wa kufikisha ujumbe kwa njia ya kuwapondea, lazima uwapate wa kuwapiga za sikukuu hizi mbili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…