Wanaume wanalalamika sana kuhusu makeup zetu: Mwanamke pitia tips hizi muhimu kwenye swala zima la urembo

Wanaume wanalalamika sana kuhusu makeup zetu: Mwanamke pitia tips hizi muhimu kwenye swala zima la urembo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Wanaume wanalalamika sana kuhusu jinsi wanawake tunavyopaka makeups zetu. Na hizi colour combo ndio kabisaaa...Maybe huwa tunafanya makosa bila kujua. Jaribu kuzingatia yafatayo ukiwa unajiandaa na swala zima la kujipamba.

Kwanza kabisa unatakiwa ujue shape ya sura yako.
Hii itakusaidia kujua aina gani ya nyusi zinaendana na uso wako.
Ukiangalia kwenye hii picha utaona shape ya uso, inaendana na nyusi aina fulani.

brows-for-your-face-shape-530x168.jpg


Unapoenda kununua foundation yako, ijaribu sehemu ya chini karibu na kidevu, na si mkononi ili uweze kujua kama inaenda na uso wako au la.

article-2120193-125591E3000005DC-699_634x582.jpg


Unapopaka wanja kwenye macho, inabidi ujue una aina gani ya jicho. Jinsi unavyopaka wanja, ndivyo utakavyobadilisha muonekano wako.Kama jicho lako ni dogo,inabidi upake wanja ambao utafungua jicho lako na kulifanya lionekane kubwa zaidi. Ukitazama picha itakusaidia kujua wanja upi unasaidia vipi muonekano wa jicho lako.

how-to-put-on-eyeliner.gif


Ile style ya kupaka wanja mweusi kwenye lips imeshapitwa na wakati. Paka lipstic au lipshine yako vizuri basi, muhimu kuchagua lipstic inayoendana na wewe.

Angalizo.
Usinunue au kujipaka kitu kwasababu umemuona mtu mwingine amepaka. Siku zote hakikisha umejipaka kitu kwa sababu kinaendana na ngozi yako.



abarawonsstyle.blogspot
 
Wape somo maana kuna watu wapiga make up kwa mazoea tu.
 
wapanda daladala na makeup ni shughuli labda lipstick na wanja kwa mbaliiiii
 
Huu urembo unipite kushoto maana makeup nyingine mmh. Scrub, powder, wanja, lipshiner. vinatosha.
 
Fake eyelashes zile ukiziangalia unaona kama matawi ya miti iliyopandwa na Makonda halafu ikasahauliwa kumwagiliwa zinatuua.

Inakuwa ukimuangalia mtu kama unaangalia horror movie.

Fake eyelashes inatakiwa ukiangalia hata hujui hizi fake au real.

Halafu applying makeup in a public place just spoils the magic of it all.

Leave something to the imagination please.
 
A black woman was never mean to wear makeups, you are a natural beauty and an amazing creation that God has created. Acheni hizo stupid make ups. Watu wa jamii zingine wanawaonea wivu hiyo ngozi yenu they wished they had it ila nyinyi mnajidharau, why?
 
Back
Top Bottom