naomba unisaidia kuani umhimu wa kuvaa pete...
Pete zinamaana kubwa sana katika mahusiano ya wawili wapendanao unapo amua kuiweka pembeni inaashilia nini?
Pete zinamaana kubwa sana katika mahusiano ya wawili wapendanao unapo amua kuiweka pembeni inaashilia nini?
Ukiangalia kwa makini kwenye vidole vya wanandoa utagundua kuwa wanaume wengi hawapendelei kuvaa pete za ndoa, huku wanawake wengi wanapendelea kuvaa pete hizo unakuta anazo mbili ya uchumba na ile ya siku yenyewe ya ndoa kwenye kidole.
Je kwa nini wanaume hawapendi kuvaa pete za ndoa?
Ndoa ya wawili wapendanao,
ipo moyoni mwao na Mungu Mwenyezi,
pete ni ishara tu mkuu!!!!
Kuvaa pete ni ujinga! Babu yangu na Bibi yangu mpaka wanatangulia mbele ya haki ndoa yao ilikuwa na miaka 70 (sabini), lakini sikuwahi kuwaona wakiwa na pete kwenye vidole vyao!
mie automatically toka utoto wangu huwa sipendi kuvaa vitu mwilini kama bangili,heleni,pete au kubadilisha nywele kama mtoto wa kiume huwa naona sipo huru nikifanya mambo hayo kikubwa ninahisi wengi wanavua kutokana na either sio waaminifu kwa ndoa zao au hawapendi tu kwasababu wanaona mzigo mwilini
Kwa hiyo hakuna umuhimu wa kuvaa pete?
sisemi watu waache kuvaa pete,
watu waendelee tu kwa amani kuzivaa hizo pete,
kwani ni ishara kuwa yupo kwenye ndoa, (ingawa siku hizi kuna wengine wanavaa pasipo ndoa)
lakini hata wale wasiovaa na wako kwenye ndoa,
mimi binafsi siwezi kuwashangaa, kwani
ndoa ipo moyoni mwa mtu na wala si kwenye pete!!!!!!
Bacha wewe umevaa pete ya ndoa?? Kama hujavaa ulipokea ya nini pale kanisani/Kwa RC.
Si ungeiacha hapo kwa padri/mchungaji
Nimeivaa moyoni mwangu!!!!