Wanaume wanatuchosha lakini hatusikii na wala hatuoni.


Ndo shida ya kutaka kuolewa tu kwa sababu marafiki zako karibu wote wanaokuzunguka wameolewa. Kwa hiyo jamaa alivyomwonyesha upendo ule wa kitapeli na kumwahaidi atamwoa, masikini my shost akamwamini.
 

Aksante kwa ushauri huu. Nipo nae na tunajaribu kumpa moyo sana, mashosti tunataka tumchangie hata kidogo kumrudisha katika hali ya kawaida, maana ukimwona amechanganyikiwa kabisa, lile penzi alilokuwa anapewa halipo, pesa pia hazipo, vyote viwili ni kwa wakati mmoja na jamaa huyo huyo, inauma kwa kweli.
 
mkome na nyie..ndo maana hata JK anawaambia mna viherehere...

Jamani Chezo mbona una roho ngumu kiasi hiki? Tuna viherehere wakati mnatuonyesha upendo, na sisi tukishajiingiza kichwa kichwa mnatutenda. Huyo niliempigia mstari kama si kiherehere anavyokiita yeye angezaliwa.
 
wangechukua hamsini ingekuwa vizuri,millioni sita?? Wanaume wengine jamani!!! kweli wanatisha....nafurahi haya maneno yanapotoka kwa mwanaume....Bwana Yesu Rudi tu!!!

Yaani alimwonyesha mdada mapenzi hasa kumbe hayakuwa mapenzi bali utapeli, alimpa mdada milioni moja ya kufanya shopping. Baada ya muda ndo yeye akaja na gia ya kusema mzigo umekwama na hahui afanye nini? Eti dada tu ndo mtu wake anamhesabu kama mama wa watoto wake, halafu anavyoongeaga kwa upole kaka yule, hata sisi marafiki hatukutegemea. Kweli tumepata somo.
 

Jamani!!!!!!!!!!! Yaani hata huyu shoga yetu amechanganyikiwa sana. Halafu mimi ninavyomwona hajachanganyikiwa kuhusu pesa kama kumpoteza jamaa. Yaani tumeshajitahidi kuongea nae mwisho wa siku ukimuuliza jamaa akikuomba msamaha utamsamehe, hatoi jibu la moja kwa moja lakini kwa mtu mzima ninaelewa tu kwamba jamaa ndo anamuumiza kuliko pesa. Jamani lakini yuke kaka anajua kuigiza, si mchezo.
 
Hayo mapenzi motomoto ndo yapi,mpaka utoe milioni sita....Mungu pitisha mbali,hata kama ni matamu namna gani sitaki kitu cha kuniondolea uwezo wa kufikiri....khaaaaaaaaaaaaaa!

Muulize mleta habari Michelle! hahahahah lol! Njemba katika muda wa miezi mitatu ilionyesha penzi la hali ya juu mpaka marafiki wakaanza kusifia...kumbe alikuwa ana mpango wake mkubwa. Huyu ni wa kumkomesha tu asirudie tena kumfanyia mwanamke mwingine utapeli kama huu. Ni kumkwida shati barabara arudishe pesa za watu haraka sana au apandishwe kizimbani, lakini si ajabu mdada hana ushahidi wa kuonyesha kama kweli alimpa huyo tapeli hizo million 6.
 

Yaani we acha tu. Mapenzi, mapenzi mapenzi na siku hizi naona kama hayapo zaidi tu ya utapeli, lakini wadada hatusikii, ila hili somo tumejifunza, jamani jamani usiombe umwone huyu dada sasa hivi maana hajitaki kama sio kutokujipenda, tumeshabembeleza weeeeeee mpaka.
 
Hivi ndio maana wengine wanarogwa kabisa embu ona huyu alivofanya, halafu bila haya anaruka namna hiyo, mtu kama huyo kumkomesha wewe unakaa kimya tu, yeye ndio aaanze kujiuliza, au unaokota mizoga kila siku ofauti leo wa paka, unaenda tupa mlangoni, kesho wa mbwa , kesho yake wa bundi hapo hakuna uganga lakini ataipata fresh
 
Mwaka huu tutakoma,maana tutaitwa kila jina,sawa bana.

Bishanga ndugu yangu, naomba tu uniambie huyu ni mwanaume mwenzio hivi kitendo alichofanya ni sawa kweli? Tutamwombea tu na maombi yatajibiwa.
 
Mpelekee pole zake ila isijekuwa ni wewe unatumia kigezo cha "rafiki yangu" si ndio style ya kuripoti matukio hapa JF? Pole sana

Wala hata jamani, ingekuwa mimi ningesema tu kwamba ni mimi kwani kuna tatizo gani. Sidhani kama huyu shoga yangu anatamani hata ku-chit chat kwa sasa ukimwona utamwonea huruma.
 

Bila kumfagilia huyu mwizi, huyo dada kachemka sana. Miezi mitatu tuu tayari anaenda kumkopeshea pesa bila hata maandishi? Ndio maana labda wanasema ukitaka kumwibia mwanamke mpe mapenzi ya uhakika. Kuweni makini. Miezi mitatu tuu? Khaaa! Buyers be aware. Wezi wako kila kona.
 


Tapeli wa level nyingine hiyo....mpe pole sana mdada!!
 
Kabla ya kupewa pesa huyo mdada alikolezwa kwa KATERERO kumbe tusemeje, miezi mitatu huwezi kumwani mtu hivyo


Jamaa anajua kuona mbali kweli, yeye alimpa mdada milioni moja naona ndo ilikuwa gia ya kuvutia kasi
 
Kuna watu wana roho ngumu hapa duniani hawana hata chembe ya huruma
Maskini dada wa watu namuhurumia usawa huu ni kumwamini mtu ndani ya miezi mitatu..lol
nakumbuka dada mmoja alikuja na sredi hapa mmewe kamdhulumu 5m sembuse huyu mpenzi wa miezi mitatu.
Pole dada hapa hili janga lako malizia kulipa mkopo wako uendelee na maisha mengine
ingawa inaumiza....
hilo jamaa natamani nilimwagie Acid
 
Laiti angelikuwa dada yangu angekipata cha mtema kuni,mwanamke umetoa u... na bado unatema faranga namna hyo,hivi siku hizi akina dada mnaumwa nini?miezi3?...mie mchumba wangu tuna mwaka sasa na bado anawaza sana kunikopesha laki moja iweje miezi3 upate ujasiri wa kutoa mamilioni hayo yote?

kuna mipango maalum ya kutoa pesa kiasi hicho na siyo tu kwa vile mnavuliana nguo na kuitana sijuhi honey,sijuhi dear,sijuhi shosti...umeona sasa?
 
Tapeli wa level nyingine hiyo....mpe pole sana mdada!!

Lizzy mimi simpi pole. Sorry. Hata-learn chochote kwenye hizo pole. Let be realistic here! Yaani Lizzy tumekutana nikakutongoza ukaingia line, within 3 months nikakuomba mkopo wa milioni 6, huna, ukaenda kukopea kazini, halafu ukaanipa hata bila maandishi kwa vile tuu nakuwewesa kwenye mapenzi? I don't think so. Tena nita-ku-underrate sana. Siku hizi mpaka mume na mke wanaandikiana wanapokopeshana, ndio sembuse iwe boyfriend and girlfriend wa miezi mitatu? Angesema labda kabla kuanza uhusiano wao walikuwa marafiki wa kaiwada, then ningeelewa. Lakini hata hivyo, no. Angekuwa sister angekiona.
 
Huyo dada wa wapi? Anaweza weka rehani hata nyumba ya familia huyo. Miezi mitatu hata mtu humfahamu! Siyo kawaida huyo, au ndo jamaa alivunja ukuta akaona mapenzi ndo haya?
 

Safina hapo kwenye red mnataka kumchangia kimapenzi au kifedha? Kwa sababu amepoteza vitu viwili hapo. Whatever, the case, mumpe somo pia. Msije mkamchangia, halafu akipata mwanaume mwingine yanakuwa yale yale.
 


Mmmmh! Hivi hao wadada wanaoweza kumpa pesa nyingi hivyo mwanaume, tena mpenzi wake tu wa miezi kadhaa wanapatikana wapi? maana wengine sisi kila siku kutakiwa kufanya shopping tu na kabla hujakaa vizuri unarushiwa INVOICE ya ada ya Chuo....Tehetehetehetehe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…