Wanaume wanatuchosha lakini hatusikii na wala hatuoni.

So sad jaman! Its up to us kinadada kuwa makini na watu wa namna hii, wanaume wengine ni hatari na kama wasemavyo "moyo ni giza nene huwezi jua yupi mkweli yupi tapeli" so ni vizuri kuwa alerted especially mwanaume anapotaka financial favours kutoka kwako, ni afadhali kufikiria kwa makini na kuchukua muda kutafakari au hata kutafuta ushauri kwa watu wengine. Inauma sana kwa kweli, so sorry kwa huyo mdada she did it out of love, hakujua kama jamaa angemtenda, 6 million debt na maisha yalivyo tight?Lord have mercy
 
Maisha ndo yalivyo, poleni sana kwa wale ambao yamewakuta kama hayo, lakini mtambue hata wanaume hutendwa sana na akina dada japokua ni wagumu wa kusema tu. Ni bora upoteze pesa kuliko kudhulumiwa penzi
 
Babu hutujui wanawake tukipenda
tunatoa kila kitu hata roho ikiwezekana pasi na kuandika ,tunaawaamini na tunaendelea kutendwa kila kukichaaaa,hii ni mpaka tutakapoanza kufanya maamuzi kutumia akili badala ya moyoooooo
ILA IKIFIKIA HATUA HIYO DUNIA ITAKUWA NI MAHALA PAGUMU PA KUISHI HASA KWA WANAUME
 

EMT acha hasira bana, si ndo maana nikasema mnatuchosha lakini hatusikii wala hatuoni, jamaa alingia na gia ya kumwambia mwenzie mzigo wake umekwama na hamna mtu wa kuweza kumkopesha kiasi hicho cha pesa zaidi yake, ila pindi tu atakapokamilisha mambo yake atarudisha kiasi hicho cha pesa na pia wife to be angefurahi zaidi, yaani angepewa zaidi ya hiyo m6.
 
mpelekee pole zake ila isijekuwa ni wewe unatumia kigezo cha "rafiki yangu" si ndio style ya kuripoti matukio hapa jf? Pole sana

au ndio wale wanawake wanahonga mameniiii!!!!! Maana mie laki moja unajuta kuzaliwa!!!!!!!!!! Haya hizo biashara uliziona??? Haya makubaliano ya kulipa muliandikiana au ndio maloveeeeeeee hothot!!! Kweli kinyagoi cha mpapure mweeeeee
 
Embu dada zetu muache kukomalia tu wanaume wana tabia mbaya,ooh wanaume matapeli..Ukweli ni kwamba matapeli wapo wengi hata wanawake pia wapo...mimi namuona huyu dada kama mlemavu wa mapenzi,aidha anapenda sana na vibaya, ama ni mgeni katika mapenzi na alikolea kama moto wa kifuu..Kukopa mil 6 kwa ajili ya mpenzi mpya wa miezi 3,hata ingekuwa mwaka ni kumwamini mtu asilimia 99.9 wakati ndio kwanza umeanza nae mapenzi...Angekuwa mume ni sahihi kukopa kwa ajili yake mil 6...Kwa mpenzi mpya NO dada amepotea step..Sikatai hilo li jamaa ni tapeli na inaonekana huo ndio mchezo wake na huyo dada imekula kwake kamuazima kama mpenzi wake hakuna kusainishana wala nini hapo na ushahidi hakuna hivyo hakuna kesi...Dada zangu kuweni makini,ila kama hilo li huni linasoma haya ma post hapa lita twist hiyo technique,kwa hiyo kuweni makini zaidi...
 
Hii hatari sana mtu hamjafunga hata ndoa tayari unampatia 6m?sijui lkn nilishasema mwl wenu kipofu

Unafikiri umekosea baba, kipofu kweli kweli na sijui tumpeleke wapi angalau awe kengeza anaweza akajaribu kutuongoza. Yaani naona kosa letu ni kumuamini mtu jumla jumla, miezi mitatu unamkopea mtu mil 6, wakati ukiangalia angeweza kujikopea mwenyewe ili afungue hata kimradi uchwara!
 


Sijui ni akili ya namna gani unazozizungumzia wewe, maana mdada ni msomi tena msomi haswa au ni akili za kujua mambo, nasikia kwenye mapenzi akili huwa zinahama, mtu unakuwa hujihelewi, labda na shosti wetu akili zilihama.
 

EMT ndugu yangu wewe onyesha hata huruma kidogo, michango yako ni mizuri lakini mbona haujaniambia nimsaidieje huyu my shost we umebaki kumlaumu tuuuuuuuuuu. Tunajua kabisa uamuzi aliouchukua wa kumkopesha jamaa hela ni mgumu, lakini sasa ndo kesha fanya tukiendelea kumlaumu uoni kwamba tutazidi kumchoma roho, hapa tunataka kumsaidia na ndo maana mashosti tumeamua kumchangia angalau basi apate hata kimoja kati ya hivyo viwili alivyopoteza, maana kuhusu mapenzi hatuwezi kumsaidia zaidi ya kumshauri kwamba amtoe huyo bwana akilini, aangalie vitu gani vizuri vinavyoweza kumsahaulisha jamaa, kama kujinunulia vitu vizuri, kuhama alipokuwa anakaa kama ni nyumba ya kupanga, kujisahaulisha yale mazuri yote aliyokuwa akitendewa na jamaa, na kukumbuka mabaya ya jamaa likiwemo hili la kumtapeli.
 
Binafsi sidhani kama ingeniingia akilini!Kwanza akianza tu kunihonga sijui million ya shopping naanza kumwogopa!

Mpenzi jamaa anapenda mambo makubwa kama nini? Kuanzia mavazi, usafiri, mahoteli ni makubwa makubwa t.
 
Galz....galz....galz.... come on, tutalia mpaka lini???Mapenzi mengine ni upumbavu tu!! How can u trust a guy ambae umekuwa nae only for 3months. Wake up dears, let us learn jaman hii mijanaume hii itatumaliza!!!

Kipipi mpenzi, naona wameshatumaliza kabisa.
 
Hii ni tuition kali sana kwa mhusika na wengine wa humu JF.....!
 
hayo ndo madhara ya kavu... yaani utamu unakukolea mpaka unajaza form kuchukua loan ofisini kudadadeki...huyu jamaa atakuwa anajituma sana maana amefast track sana hii kitu na imekuwa positive...

ha ha ha ha ha ha jamaa atakua fundi!
 

Huu sasa uongo! Unachukuaje hela nyingi kiasi hicho bank kwa kutumia kadi ya mtu mwingine? Ingekuwa kwenye ATM sawa, ila hapo inaonekana aliingia ndani kabisa. Haiwezekani ndugu
 
Huu sasa uongo! Unachukuaje hela nyingi kiasi hicho bank kwa kutumia kadi ya mtu mwingine? Ingekuwa kwenye ATM sawa, ila hapo inaonekana aliingia ndani kabisa. Haiwezekani ndugu
Jamani,hata ATM haiwezi to all that amount per day.The highest amount per day ninayoijua mm ni laki 5 NMB na hizi limits zimewekwa kwasababu za kiusalama upande wa hela za mteja incase mtu kaiba pword na card yake.Na kama ni ndani,je hawakumuidentify kwenye kitambulisho?na signature je?
 

Hapo kwenye red ni wizi mtupu. Kadri unavyoandika ndivyo unavyoonyesha jinsi shosti alivyokuwa amechemka. Angekuwa makini hapo kwneye red nako angefikiria mara mbili.

Sijui ni akili ya namna gani unazozizungumzia wewe, maana mdada ni msomi tena msomi haswa au ni akili za kujua mambo, nasikia kwenye mapenzi akili huwa zinahama, mtu unakuwa hujihelewi, labda na shosti wetu akili zilihama.

Akili ya kawaida. Huitaji wala kwenda shule. Kwenye mapenzi akili zinaweza kuhama lakini sio ndani ya miezi mitatu.



Sasa hapo utamsaidia nini? kweli jamaa kamtapeli lakini naye katapeliwa kirahisi mno. Mchango wangu ajifunze kutokana na kosa alilofanya. Sidhani kama kuna kingine cha kumsadia, unless mna mpango wa kutafutia mwanaume mwingine. Kama walikuwa wameandikishana huo mkopo ungesema labda achukue hatua za kisheria. Lakini kama alinogewa penzi hivyo sifhani kama atakuwa nao.
 
Hawa wanaume hawaaaaaaa!! Dah, bora hii dunia tungeumbwa peke yetu. Mpe pole mdada, mwambie hizo ni changamoto tu za kumuweka imara na maisha lazima yasonge mbele.
 
Mbona wako wengi wanaume wa hivyo.mjini hapa ila tu tuwe makini jamani.
 
hamuwezi kusikia coz mpo kifedha zaidi, hamna mapendo ya dhati zaidi wa wizi through mapenz!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…