Ni kweli huyo mwanaume ni tapeli hasa. Lakini inashangaza wadada hapa wanapoimba wanaume wanaume! Au kwa sababu huyo kachukua nyingi kwa mara moja? Wasichana wengi wanakula na kufuja hela za wanaume huku wakijua mioyoni mwao hawana mpango na wanaume hao, ukiwauliza utasikia 'si kanipa mwenyewe? Kwani nimemlazimisha?' si zinamuwasha, nk. Hapa kila mdada ni malaika hajawahi kutumia hela ya mwanaume huku akijua hana feelings zozote za mapenzi naye! Wote tunaujua ukweli, wadada wengi ni matapeli sawa na huyo jamaa, labda tofauti tu ni amount. Wangapi wanagarimiwa masomo, nyumba/vyumba, gari, mavazi, misosi, vinywaji na vitu kibao lakini mwisho wa siku wanawatema wanaume tena kwa kejeli kibao?! Huyo jamaa ni mwizi kamili, lkn hiyo isitumike kutuita wanaume wote majina ya kila namna. Wasichana wanatumia hela za wanaume kwa udanganyifu zaidi ya wanaume wanavyotumia za wanawake! Vumilieni hadi usawa utimie!!