Wanaume wasio na wapenzi Wana furaha na amani

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Nimefanya uchunguzi nimegundua wanaume ambao hawajihusishi na maswala ya mahusiano Wana furaha Sana ndani ya mioyo yao.hawana mawazo Sana na Wala hawana magonjwa ya moyo na pia hawana stress.hata Kuna ma braza zangu wakubwa ambao nilikuwa nikikutana nao kitaani tunacheka Sana stori nyingi ila baada ya kuoa wamebadilika hawacheki Tena wamekuwa na uso wa simanzi na ukauzu fulani mpaka nawaogopa Kuongea nao wamekuwa wakimya sana hawaongei kama zamani. nikatamani kufanya uchunguzi kwanini walioamua kuvaa wajibu wa ndoa na kuishi na wanawake hawana faraja mioyoni mwao,nikagundua wanawake huwa wanapenda Sana uteseke juu yao yaani wakiona huna furaha au unaumia na kukwazika juu ya Jambo fulani wenyewe ndo wanaridhika ndo maana hatahangaika Ili urudi Kwenye Hali ya kawaida ya kufurahi ye atataka muda wote unune mwisho ukumbwe na matatizo ya moyo ufe mapema.Kwa hiyo atakupeleka mbio mpaka ushangae.wanachojiamini Hawa wanawake zetu Ni kwamba Wana soko hata Kama ukimuacha Leo hii hawazi kesho ye anapata mwingine.ila wewe mpaka upate mwingine lazima ukae hata mwezi mmoja au miwili ya kujitafakari ndo ufanikiwe kuanza kuishi na mwingine.
 
Sio kwa wanaume tu hata kwa dada zetu hali ipo hivyo, kutokua na mwenza mtu ana kuwa na uhuru fulani hivi, hakuna ugomvi hakuna lawama yani stress free zone na maisha yanasonga tu bila bughudha , ila faida ni nyingi kuliko hasara

Super hero daddy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…