Thuwaiba Habibu
Member
- Oct 8, 2024
- 8
- 5
Wanaume watoe ruhusa kwa wanawake kuingia katika uongozi
Na Thuwaiba habibu
Sheha wa michamvi Khadija hassani haji amewaomba wanaume watoe ruhusa kwa wanawake kushiriki katika uongozi
Ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na muandishi wa habari hizi huko michamvi mkoa wa kusini Unguja amesema wanaume waache tabia ya kutowapa uhuru wake zao katika kugombania nafasi za uongozi
Alisema baadhi ya wanaume wanapoowa wanatumia mamlaka hiyo kuwazuia kushiriki katika shughuli mbali mbali ikiwemo suala la uongozi kufanya hivyo kuna wakosesha fursa muhimu wanawake
Nae katibu wa kikundi cha kaya maskini shehiya ya michamvi Zawadi Sudi Ame alisema lazima iandalie kampeni ndani ya vikundi vya ushirika kuhamasisha wanawake kugombea nafasi hizo
Alisema wanawake wengi hujihusisha na vikundi vya ushirika huku vijijini kwenye sehemu hizo ndiko kunako hitajika kampeni na hamasa ya nguvu kuhakikisha wanawake wanagombania nafasi za uongozi ifikapo mwaka 2025 ili kupigania maendeleo ya taifa.
Nao mwanakijiji wa michamvi wamesema wanawake ni watu wenye huruma sana wakati wanapopatiwa nafasi hizo hutaka maendeleo yaonekane na hawajivutii faida wao na familia zao.
Pia walisema kwanza wanawake wanatakiwa kujirekebisha katika suala la kuvunja moyo na kudharauliana wenyewe kitendo hicho huwapa mwanya mwanaume kuwakandamiza.
Walisema wanawake hawaoneshani ushirikiano na wanabaguwa endapo ikitokea nafasi ya uongozi huchangua mwanaume kuliko mwanamke mwenzao na hapo wanaume huwaona hawana uwezo lakini wakiamua kuacha kudharauliana na kuoneana wivu na wakawa na mashirikiano watafikia asilimia hamsini kwa hamsini na wanaume kwani kuongoza wanaweza