Tausi Mzalendo
JF-Expert Member
- May 23, 2010
- 1,470
- 722
Nilibahatika kusikiliza mazungumzo ya wadada fulani wakisema ati wanaume wazuri ni wale waliopata malezi ya karibu ya mama zao.
Wakatoa mifano ya ni vipi waliliona hilo:
Wanaume hao wanajua kupika, kulea watoto, wana huruma zaidi, wanaheshimu wanawake, wana upendo, wanajali, etc.
Mwanakijiji lazima kuna watu watasema hivyo...Naamini kuna ukweli lakini wengine wanasema ni watu waliodekezwa sana na kuharibiwa! Ndio huwa wanaitwa "watoto wa mama" a.k.a 'mama's boy'
Hahahaha!!! Mwanakijiji umeona nilijua tu lazima watasema hivyo...Hao wamedekezwa sana hawajui kujishughulisha mtaani tunawaita watoto wa mama wao ni kudeka deka na kuona wanaonewa kwa kila kitu
Nilibahatika kusikiliza mazungumzo ya wadada fulani wakisema ati wanaume wazuri ni wale waliopata malezi ya karibu ya mama zao.
Wakatoa mifano ya ni vipi waliliona hilo:
Wanaume hao wanajua kupika, kulea watoto, wana huruma zaidi, wanaheshimu wanawake, wana upendo, wanajali, etc.
Hili likanifanya nifikirie na kwa kiasi nikaona lina ukweli.Nimeliona hilo kwa ndugu zangu wa kiume waliolelewa na mama zao bila kuwepo baba, au wale waliokuwa na baba lakini wakatii sana mafundisho ya mama zao.Wako independent zaidi, hawanaga makeke sana kwa wake zao, nk...
Hebu tupate mawazo zaidi kwa wale wenye uzoefu.
Mwanamme kujua kupika ni quality ya kusema ni mwanamme mzuri?
Hata mimi sijui, ila nadhani kama mwanaume anajua kupika hawezi kuwa fussy kama wale wasiojua.Mwenye kujua kupika most probably hatazinguka sana na "mapishi" ya nje maana hata yeye ajua kupika!Ngoja tusikie watakaojibu wanasemaje.Mwanamme kujua kupika ni quality ya kusema ni mwanamme mzuri?
That was my biggest issue,
Huku uswahilini hiyo ni disqualification!!
Tausi,
Hapo kwenye blue...hivyo navyo ni vigezo vya mwanamume mzuri???
Na hapo kwenye red, hiyo list in exhaustive??
Hata mimi sijui, ila nadhani kama mwanaume anajua kupika hawezi kuwa fussy kama wale wasiojua.Mwenye kujua kupika most probably hatazinguka sana na "mapishi" ya nje maana hata yeye ajua kupika!Ngoja tusikie watakaojibu wanasemaje.
Sidhani hata kuwa hicho kigezo kinakubalika kwa wanawake wengi...at least wale wengi nnao wajua sijawahi kuwasikia kutaja hicho kuwa ni moja ya vigezo vya mwanamme mzuri.
Na kwa vile kimetajwa awali zaidi ya vyote, jee inamaanisha kuwa kinabeba uzito mkubwa zaidi a vyengine?
Mwanamme asiyejua kupika mbona ni hatari sana; ndio mwanzo wa unyanyasaji.. nadhani hata kwa mwanamke ni to her own interests to have a man who can cook. Matokeo yake mama akiugua au kusafiri utaletewa msaidizi wa kupika.. (vyote viwili)..
nadhani mtoa mada ametoa with a light touch bila kujali sana uzito wanini kilichotajwa, vipi kimetajwa au nini kimeachwa. The point is simple kwamba wanaume waliolelewa na mama zao na kupewa yale mapenzi ya mama wanakuwa very sensitive, loving na kwa ujumla "wazuri" yaani "good". Ninavyoelewa ni kulinganisha na wanaume ambao hawakupewa mapenzi ya karibu ya mama zao.
MSINIULIZE MIYE JAMANI... mimi nimewanukuu tu hao waliosema.Hii sredi inataka kudadavua kujua "uzuri wa wanaume waliolelewa na mama kwa karibu ukilinganisha na wale waliojikita zaidi kwa baba zao" .