Habari wana jf, poleni kwa shughuli za ujenzi wa taifa.
Huku mkiendelea kupokea matokeo ya uchaguzi, naomba niongelee jambo moja la msingi ambalo nimekuwa nkilishuhudia katika jamii zetu na hata humu jf ni very common.Wanaume mmekuwa kama mmepatwa sijui na pepo gani! Yaani ni kama nanyi mnataka kuolewa, mmekuwa watu wa kulalamika tuuuuuuu, kazi hamtaki na hata wenye kazi akili zimekuwa mgando anategemea mshahara mdogooo hata hajitanui kimawazo kusaka hela zaidi, au kazi yenyewe anafanya kivivuuuu muda mwingi yupo kwenye mitandao ya kijamii kujibizana na kutukanana na watu asiowafahamu na wivu usio na mpango kwa waliomzidi kipato.
Imefikia hatua mwanaume anamuonea wivu binti mdogo aliyeolewa na mwanaume (wa makamo) mwenye pesa, utakuta wamekaa wakimjadili binti na hata kumtukana na kuwachanganya wanawake woote kuwa wanapenda pesa (who doesnt), badala wakae wajiulize ni kwa namna gani huyo mwanaume mwenzao amefanikiwa kiasi hicho nao wajitahidi wamfikie au hata kumpita wamekalia majungu tuuuuuuu!! Utasikia mara free manson,mara pesa za madawa (maneno ya wakosaji).
Ni kweli kwamba maisha magumu and so on, ila isiwe excuse ya kuwafanya muwe marioo bila kujijua, wanaume wengi ni marios ila hawajijui tu, sasa si bora mijitanabaishe tuolewe wote tu na sio kuwa walalamishi that much, ni aibu sana tena sana kwakweli.Msije kujifanya hapa sijui wanawake tunapenda mteremko ndio maana tukaitwa wanawake nanyi wanaume, sisi ni jukumu lenu, sasa mambo yamebadilika siku hizi nasi tunafanya kazi ili tusaidieane ila sasa isiwe ndio chance ya nyie kubweteka na kuwa marioo, mwanaume lazima uwe "MWANAUME" hii itakupa heshima bila hataaa kutumia nguvu kuidai.
You have to man up na mchukue nafasi zenu kama wanaume, kulalamika hakutokufanya uwe Bakhressa au Mengi, wivu pekee unaotakiwa kuwa nao ni wa kupiga hatua na sio kumuonea wivu K'lyn kwa kuolewa na Mengi (vipi wataka kuwa mke mwenzie?)
Nawasilisha, likikugusa waruhusiwa kutukana si ndicho mkijuacho zaidi.