Wanavyotumia interview ya zamani kufanya Diamond aonekane ana kiburi

Singida ndio home

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
3,188
Reaction score
3,370
Kumekuwa na video ya miezi 9 iliyopita ya interview ya Diamond yenye lengo la kumchafua, Huyu dogo hajafikisha hata miaka 30 ila kaka zake na dada zake wanavyomtungia vitimbwi siku unaweza kumwonea huruma,

lengo la hawa wanga kuisambaza hii video clip ni kuchochea upuuzi, hawajaweka wazi kwamba hii interview ni ya miezi tisa iliyopita wakati ambao dogo kachoka kunyonywa na ile radio iliyopiga pini nyimbo zake zisipigwe, hii kauli aliitoa endapo ile radio itamfanyia figisu figisu nyimbo zake zikifungiwa,

Hawa wanga wanasambaza huu utumbo ili ionekane Diamond katoa hii kauli baada ya kufungiwa na basata, Niwafumbue tu macho kwamba hii interview ilifanywa zamani sana na kijana alitoa hii kauli baada ya kuwapa kisogo ile redio na akaweka wazi endapo ile radio itamfanyia figisu ili nyimbo zake zifungwe basi atahama hii nchi.

MALIPO NI HAPAHAPA DUNIANI!!!!!!
 

Mmh mmh umeandika ujinga
 
Diamond alihitaji muda kujipambanua na kupambana na medias nyingine kunalevo flan ingefika diamond angetoa makucha yake bila kudhuriwa alianza mapema Sana kwa watu wenye mizizi kwenye industry....

Mawingu siwapendi ila ukweli na uwe ukweli wanna kitu Cha ziada na wanaijua vyema siasa ya bongo wanaijua michezo yote michafu ambayo mondi ilimuhitaji kajifunza kwanza

Alikiba anaweza kuwa na madhaifu yake Kama ilivyo kwa binadamu wengine but he knows to play fair somehow.
 
Dogo hapo alikuwa anawajibu basata na naibu waziri kuna nyimbo zake mbili zilikuwa zimefungiwa kipindi hizo tena aliyetangaza ni Naibu waziri,zilikuwa nyimbo zaidi ya kumi.Nikweli interview ni ya zamani ila hapo hakuwa na mausiona na redio furan nenda kwenye account ya lil omy YouTube..
 
Dai hana miaka 30? Una uhakika mkuu maana tangu aanze mziki miaka 9 tayari
 
Nilichoona hapa si kwamba ni kujadili hali halisi, bali ni chuki na wivu wa kike uliyowajaa baadhi ya watu(ukikasirika utajijua mwenyewe)

Diamond nyimbo zote anazotajwa hazina maadili, hakuna hata moja ambayo ni yake. Hiyo Mwanza hadi Kwangaru, zote kashirikishwa. Ila sioni watu wakimsema mwenye wimbo, wakimtaja Rayvan au Harmonize waliyoweza kumshikirisha kwenye nyimbo zao.

Watu ni Diamond kuimba matusi, husikii akiambiwa mwenye wimbo kaimba hivyo. Hapa ndiyo utajua kabisa, wengi humu wapo kumponda huyo jamaa kisa chuki zao na wivu wa kijinga. Yaani mnatumia nyimbo zisizo zake kumsema vibaya, huku mkiacha wamiliki wao hata kuwakosoa kwa kufikiria idea za namna hiyo.

Hakuna cha maadili wala nini, humu mmeendekeza chuki zenu. Hapo kisa ni Diamond na si kisa ni maadili.
 
Siku Fiesta inazuiliwa kuna clip za kucheka za Diamond, akionesha kuwacheka jamaa.

Unaikumbuka kauli mbiu ya "Cheza Usichezewe Wewe", naye kachezewa, ausome mchezo kimya kimya.
 
Kwenye wimbo wa Kwangwaru verse ya Kondeboy iko clean kabisa, verse ya 'kaka' ndo imejaa mitusi, Kwenye wimbo wa Mwanza verse ni Diamond aliyeimba 'Nyege nyegezi', 'Michezo ya Amberruty', 'Pitisha kwa chini',,, kwa Rayvanny hakuna shida sana. Labda Mbosso ndo wa kumtahadharisha sana maana naye anapita mulemule kwa boss wake, sijui anafukua mitaro,nipitishe boda la huko,...n.k
 
Siku Fiesta inazuiliwa kuna clip za kucheka za Diamond, akionesha kuwacheka jamaa.

Unaikumbuka kauli mbiu ya "Cheza Usichezewe Wewe", naye kachezewa, ausome mchezo kimya kimya.
Yupo Kenya tayari anajiandaa kuperform Mombasa na Nairobi
 
Hujui unachokisema, hayo maneno yakikuwa hayahusiani na Clouds, ilikuwa ni baada ya kufungiwa 'wakawaka' na 'aleluya', hapo alikuwa anawajibu Basata na Shonza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…