Kuna hili sakata la wanavyuo kushindwa kupiga kura kutokana na vyuo kuchelewa kufunguliwa, mpaka sasa sijapata habari zaidi ya ile walipokwenda kwa waziri mkuu, je kuna kinachoendelea? na kama ikishindikana itakuwaje?, je suala hili kuna mkono wa siasa au ni bahati mbaya?
Tanzania full uoga, kama wahadhili walishindwa je wanavyuo wataweza, hio ndio imetoka bwana, ila shame on Tz Gvt.Mambo haya huwezi fanya nchi kama Ug, SA na kwingineko ambako wananchi wake wanatambua haki yao ya kidemokrasia.
Wengi ingawa sio wote nimewasikia wakijitayarisha baada ya wiki hii kwisha kwenda kupiga kura. Hasa wa UDSM wamejitolea kutopoteza haki yao.