Wanawake acheni kuwaroga waume zenu kwa tamaa ya mali

Wanawake acheni kuwaroga waume zenu kwa tamaa ya mali

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
5,715
Reaction score
13,739
Hii kitu imezoeleka sana kwenye familia zetu lakini watu wengi wanashindwa kuiongelea, wanawake wamekosa huruma kabisa mwisho wa siku wanauwa bila kujuwa kuwa wanauwa, kuna familia moja huko kanda ya ziwa jamaa alienda kuowa huko dodoma kondoa kwa warangi.

Lakini jamaa alikuwa ameishapata watoto watatu kutoka kwa mke mwingine ambae waliachana na kipindi anamuowa huyo dada wa kirangi alikuwa vizuri kiuchumi, inaaminika kuwa waislamu huruhusiwa kuowa wake wawili mpaka wanne. Na jamaa nae alikuwa ni muislamu basi maisha yamekwenda ndani ya miaka 9 jamaa akajenga nyumba mbili lakini pia walibahatika kupata watoto watatu wengine na mwanamke huyo wa kirangi.

Sasa shida inaanza jamaa akasema anataka aongeze mke wa pili mama wa kirangi kusikia hivyo amani ikavurugika ndani ya nyumba lakini jamaa akasisitiza kuwa lazima aowe mke wa pili, mama wa kirangi naona aliona solution ni kwenda kwa karumanzila akapewa kwa kigezo cha kumfunga jamaa asiwe na mawazo ya kuowa mke wa pili, mama kazidisha dozi jamaa akawa zezeta matokeo yake akawa anashinda ndani tu amejificha anaogopa mpaka watu.

Mwisho wa siku akafariki baada ya kufariki jamaa uchumi wa familia ukayumba mbaya, mpaka chakula kikakosa ndani ya nyumba, kwa sasa mama wa kirangi anahaha na maisha amefikia mpaka kugawa mzigo hovyo ili apate riziki ya kuendesha maisha.
 
Nimeona utaombwa picha

IMG_20221116_201101.jpg
 
Tahadhari " kabla ya kuongeza mke" Au ni uongo ndugu zangu..!
 
Mimi nilileta thread humu wanawake jamani wanatisha akina mama wa leo ndio wakukaa nao mbali mno Siri ya maendeleo na itawale la sivyo?
 
Title haiendani na habari kamili. Maana mke alimroga mume wake ili asiongeze mke mwingine. Ilipaswa iwe wanaume acheni tamaa za kuoa mke zaidi ya mmoja
 
Ni bora mlogwe na wanawake zenu wahalali kushinda kulogwa na mchepuko mzoeee hii hali tu hii ndio nynja zakulinda Mali za watoto wako wa baadae wewe sema tu wasiwe wanawaumiza kiafya waume zao maana Sasa hii ni mbaya watakufa naakose mapenzi ya kudumu.
 
Back
Top Bottom