Wanawake Dar mmeamua haya na mi sijui, kuna watu wana siri...nimelia sana
=====
Your browser is not able to display this video.
Wanawake wa jijini Dar es Salaam, kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wanatarajia kuandaa tukio maalum la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa mafanikio yake katika nyanja mbalimbali za maendeleo. Tukio hilo linatarajiwa kufanyika katika siku zijazo, likilenga kuonyesha mshikamano na kuunga mkono juhudi za Rais katika kuleta maendeleo nchini.
Katika hafla hiyo, wanawake hao wataelezea furaha yao na kutambua juhudi za Rais Samia, ambaye hivi karibuni alichaguliwa tena na chama tawala cha CCM kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu2025. Wanawake hao wamesema kuwa Rais Samia amekuwa kielelezo cha uongozi bora na amekuwa akifanya kazi kwa karibu na jamii katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Tukio hili linakuja wakati ambapo nchi inajiandaa kwa uchaguzi mkuu, na wanawake wa Dar es Salaam wanatarajia kuwa sehemu ya mabadiliko chanya yanayoletwa na uongozi wa Rais Samia. Wanawake hao wanatumai kuwa tukio hili litakuwa fursa ya kuimarisha umoja na kuhamasisha wanawake wengine kushiriki katika siasa na maendeleo ya nchi.
Hivi huu ujinga wa uchawa aliuleta nani. Kwa nini wananchi wa Watanganyka kila kinachofanywa na viongozi waliowachagua wanaona ni hisani kwao kutoka kwa viongozi na siyo wajibu wao. Najiuliza sana,
Je ugumu wa maisha ndiyo umeleta ujinga huu?
Je ukosefu wa ajira ndo umeleta ujinga huu?
Je ukosefu wa elimu ndiyo umeleta ujinga huu?
Je wanaofamya ujinga huu ni kwa manufaa binafsi au taifa?
Je Taifa limegawanyika? Wasiopenda huu ujinga na wanaopenda huu ujinga?
Ni ujinga sababu km ni jambo jema kwa nini wasiwe wanawafanyia wazazi wao kwa kuwashukuru kuwaleta duniani, kuwalea na kuwasomesha?
"Illiteracy and ignorance are eating Africa". With regard to the above descriptions discuss this contention with reference to Tanzanian citizens (50 marks). ππ