Wanawake hatari wa kuwakwepa 2025

Wanawake hatari wa kuwakwepa 2025

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2022
Posts
276
Reaction score
460
Wewe ni mwanaume umehangaika sana kutafuta mwanamke wa ndoto zako na haujampata au pengine umewahi kumpata lakini mkashindwana?
Kama unapitia kwenye hatua hii basi tambua kuwa hakuna mwanamke mzuri na mkamilifu kwa asilimia zote ila unaweza kumpata ambaye unaweza kumjenga kulingana na mahitaji yako.

Hata hivyo kuna aina ya wanawake ambao unatakiwa kuwakwepa kwa namna yoyote kwa sababu ni hatari kuwa nao kwenye uhusiano au ndoa.

Mwanamke anafuja mali. aina hii ya wanawake hawana aibu kabisa kwenye maisha Wana tamaa hupenda kutumia zaidi kuliko kutafuta. Wao hutegemea kila kitu kutoka kwa mwanaume na wakipewa hawaridhiki.

Mwanamke alie na makundi ya marafiki kila kona. mwanamke wa namna hii hawezi kuwa furaha yako kila kukicha atajifunza mbinu mpya ya kukuumiza. Wanawake wengi wanapokuwa kwenye makundi ya urafiki ajenda yao kubwa ni kupeana mbinu namna ya kuwashinda na kuwadhibiti wanaume wao.

Mwanamke mbinafsi asiyejali ndugu zako. Ukigundua hilo mwanamke wa hivyo mkwepe kwa sababu ukiingia nae kwenye ndoa nyumba yako itapoteza uhusiano na ndugu zako na baraka zao utazikosa kabisa.

Jarida la Nairland Forum kutoka nchini Nigeria linatahadharisha kuwa miongoni mwa mwanawake wa kumkwepa kwa gharama yoyote ni mwanamke aliye na wanaume wengi mtaani anaowaita rafiki linasema inawezekana asilimia 80 ya wanaume hao anaweza kuwa nao kwenye uhusiano na wanaweza kuwa mbadala wako.

Mwanamke anaetaka kuombwa msamaha wakati wote hata kwa makosa yake mwenyewe ni miongoni mwa wanawake waliotajwa kuwa hatari na jarida la Nairland. Wanawake wa namna hii hujiona wakamilifu wakati wana kasoro nyingi za kujirekebisha.

© Peter Mwaihola
 
Bado kuna wanaume wanaopelekeshwa na wanawake kwa sababu hawana akili ya kuishi nao

Watawakwepa wanawake wasiofaa ila ipo siku watanasa tu katika mtego...

Pep aliishia kugawana mali na mwanamke aliyeishi naye kwa miaka 30.
 
Kila mwanamke ana tabia njema na mbovu kutegea na hisia zake kwako.

Ukipata mwanamke utakayemuona ni Decent;lakini hajakupenda, nakuhakikishia kuwa lazima atakushangaza.

The goal is, hakikisha anakufeel... Utaepusha kuwa shuhuda wa maovu yake.
 
Back
Top Bottom