Wanawake huwa mna tatizo gani mnapokuwa kwenye biashara?

RGforever

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2011
Posts
6,878
Reaction score
5,432
Juzi nilikuwa napita pita maeneo ya mjini kama unavyojua Mkulu kesharuhusu wamachinga kupanga vitu, nikawa napita kutafuta saa moja hivi ya mkononi kwa ajili ya mdogo wangu.

Nikapita eneo wamepanga saa nikaiona saa moja nikaipenda nikasema nikirudi nitaipitia. Nilipomaliza shughuli zangu nikapita lile eneo nikasimama akaja mdada mmoja nikamuuliza hiyo saa ni sh ngapi? Akanijibu ni elfu 10 daaah nikamwambia saa elfu kumi wakati sa hizi za kawaida ni elfu 5 nachukua, akakomaa pale pale eti haishuki hiyo kaka ni Elfu 10 nikamwambia haya dada poa haina shida.Yaani hata bila kubembeleza akaniambia haya, nikasepa zangu.

Nimefika mbele kidogo nikakutana na mshikaji mmoja kwa bahat nzuri nikaikuta saa ile ile nayo jamaa anayo nikasema ngoja niicheck. Jamaa akaniambia buku 8 hiyo boss, nikasema mimi nina tano hapa mfukoni kama inalipa nikutoe akasema ongezea kama nipe 7 nikuachie. Nikasimamia pale pale nina 5 mkuu, akasema toa hiyo pesa, nikatoa nikasepa zangu.

Sasa swali ninalojiuliza ni;

Hivi kwanini wanawake mkiwa kwenye biashara mara nyingi hampendi kushuka bei au mkiona mwanaume basi mnajua atatoa tu hela kizembe, maana huyu mwanamke si mmoja nishakutana nao wengi tu na kwenye nguo pia wanasimamia kucha, yani bora ampoteze mteja kuliko kupunguza hata mia.
 
Hao wengi itakuwa biashara wameachiwa hivyo aliepanga bei ambae ndie anajuwa gharama za Manunuzi hayupo, alieachiwa kuuza kaachiwa na bei na hujui hata faida inayopatikana ni kiasi hivyo atakomaa na bei elekezi tu, ila kwa Mwenye biashara ambae anjuwa bei ya Manunuzi hata faida buku anachukuwa mana anajuwa hana chakupoteza ikizingatiwa halipii leseni ya Biashara, Kodi ya Mapato wala Kodi ya Pango.
Mbinu hii huwa inatumiwa sana na Wafanyabiashara kwakuwa wanajuwa kuwa wateja wengi wanaamini Wanawake hawawezi wapiga kumbe ndo Nyoka wa Makengeza!!!
 
Hawa wadudu wanakwenda na MOOD wakiwa kwenye siku zao hawaeleweki kabisa. Rangi hata iwe njano watakuambia ni nyekundu.
 
Sasa mkuu mwanamke mmoja tu ndo umekuja kupondea wanawake wote??
 
wako friendly sana mkuu, pia wengi wao wana kastama kea nzuri
 
Huyo aliekuuzia 5k labda ashauza nyingi kwa 10k hio moja anarudisha hela yake tu akachukue design nyingine. Hamna mtu anakataa hela bila sababu ya msingi.
Paul how nakufatilia sana. Una upeo mkubwa sana. Michango yako humu Yani Ni peculiar. Kweli huna jiwe lolote Cambridge ama Oxford? Najua lazima mlimani unayo
 
Huyo aliyekuuzia 5000, halipi kodi, halipi frem, pengine huyo uliyemkuta dukani ni mfanyakaz anaitaji mshahara hata Akili ya kujiongeza huna, uko shule ulienda kusomea ujinga?
 
mwanamke anajua kuuza t,ila mwanaume anajiongeza na mengi,muda agni yuko kwenye biashara,cost ngapi anapata kwa kuchelewa sokoni nk,na wanawake wengi wanakuwa wameachiwa biashara
 
Huyo aliyekuuzia 5000, halipi kodi, halipi frem, pengine huyo uliyemkuta dukani ni mfanyakaz anaitaji mshahara hata Akili ya kujiongeza huna, uko shule ulienda kusomea ujinga?
Wote ni machinga hawalipi kodi.. Na wote walikuwa wamepanga Kwenye msitari mmoja niliokuwa ninapita
 
Tatatizo hawa watu hawalipi hata senti ya kodi na kwa dar pekee wapo over 1,000,000 Sijui wenye leseni halali wataponea wapi! Kuruhusu biashara holela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…