Pre GE2025 Wanawake kushiriki kwenye nafasi za uongozi ni chachu ya wengine kufuata nyayo

Pre GE2025 Wanawake kushiriki kwenye nafasi za uongozi ni chachu ya wengine kufuata nyayo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Katika ukanda wa Afrika Mashariki, Tanzania inaongoza katika kuimarisha ushiriki wa wanawake kwenye uongozi. Wanawake wanaochukua nafasi za uongozi wanatoa mfano bora kwa wenzao, wakionesha kuwa uongozi si wa wanaume pekee, bali ni haki ya kila mtu mwenye uwezo na dhamira ya kuleta mabadiliko.

Wanawake viongozi wanawatia moyo wanawake wengine kwa kuwapa matumaini na kuonyesha uwezo wao wa kushinda changamoto kama ubaguzi wa kijinsia na ukosefu wa fursa sawa. Viongozi kama Anna Tibaijuka, Halima Mdee na Dorothy Gwajima wakiwa kwenye nyadhifa muhimu, wametoa mfano wa jinsi wanawake wanavyoweza kufikia malengo yao na kuwa na sauti katika maamuzi ya kitaifa. Uongozi wao unawatia nguvu wasichana na wanawake katika jamii, na pia huchangia kutunga sera zinazoboresha maisha ya wanawake, kama kuongeza fursa za elimu na afya bora.

Katika Uchaguzi Mkuu na Serikali za Mitaa, unaona wanawake wakijitokeza kwa wingi kuwania nafasi za Urais, Ubunge, Udiwani na hata nafasi za uongozi wa Mitaa?

Soma:

==> Kwa Wanawake: Una mipango ya kugombea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa au Uchaguzi Mkuu? Kwanini?
==> Dkt. Mzuri (TAMWA – Zanzibar): Wanahabari kuweni wajasiri na wabunifu katika kuibua Wanawake kushika nafasi ya Uongozi
 
Naona wanaogopa kuchangia lakini ukweli ndo huo hakuna siku izo hoja zao zitakua na mashiko
HAO NI WASAIDIZI BY NATURE
 
Back
Top Bottom