Kwa mawazo yangu na mtizamo wangu, ni afadhali mtoto akaujua ukweli tu, kwamba fulani ndo baba yake,
pale apatapo akili za kujua mema na mabaya, na akili ya kujua kwamba kuna baba.
Upendo huwa unajengwa na ukaribu na uwepo wa mtu mwenyewe, haijalishi hata kama baba amekuzaa mara tatu, kama hana mapenzi na mtoto,
hawajibiki kwa mtoto, hapatejengeka upendo kati ya baba na mtoto. Mtoto mwenyewe ataona tu huyu ni baba kwa sababu alishiriki kunizaa lakini,
yule ambaye anamlea, na kumtunza pengine na kumsomesha na kumuonesha upendo huyo ndio atakuwa baba maishani mwake.
Tena usishangae mtoto akakutaa wewe mwenyewe kwa midomo yake, kwamba na mtambua huyu baba/mama/babu/mjomba nk nk, aliyenilea,
anakuuliza sasa wewe unasema we ni baba yangu kwa mpango gani?
Tukumbuke tu kwamba watoto, kuna wakati watakua wakubwa na wenye akili ya kujua mema na mabaya, na watajua kuchuja ipi ngano na ipi pumba. Kwa hiyo ni vema kuwa huru nafsini mwako, nakutojenga hatia nyingine kwa mtoto ako hasa pale atakapogundua kwamba ulimdanganya baba yake hayupo au ameariki.
Dah mi naona hakuna haja ya kubishana na ujinga wa mtu hapa duniani, kama anaikataa damu yake, namuacha itamtafuta/ataitafuta mwenyewe siku moja. Na mbaya zaidi wakati anaitafuta unakuta na yenyewe inamkataaa........
Mungu atusaidie tuponywe na hasira na majereha tuyapatayo katika mapito ya kukataliwa na watoto wetu, atupe neema ya kusamehe,
ili watoto wetu wawe na furaha na amani, na ikiwezekana kujijengea heshima nzuri mbele ya mtoto wako.
Sio vizuri mtoto anakua na kidonda moyoni, eti mama alisema baba yangu amekufa kumbe hajafa......
Atakudai kaburi lake na ndugu zake sijui utampeleka wapi......
Tujifunze tu kuushusha moyo na kurahisisha maisha......
Na huyo anayekataa watoto/mtoto malipo yake ni hapa hapa duniani wala hayasubiri siku ya hukumu.