Inatokea mwanaume uliyezaa naye alikutosa na kukutenda vibaya enzi za uhusiano wenu.Mwisho wa yote mnaachana na anakuacha na ujauzito.unamlea mtoto peke yako na anakua vizuri.Tatizo linakuja ukubwani,mtoto anataka kumjua baba yake,kwa nini wanawake mnakuwa mnabana sana,mnaweka password kwa mtoto hata ikibidi kumdanganya babako kafa,why this?
Inatokea mwanaume uliyezaa naye alikutosa na kukutenda vibaya enzi za uhusiano wenu.Mwisho wa yote mnaachana na anakuacha na ujauzito.unamlea mtoto peke yako na anakua vizuri.Tatizo linakuja ukubwani,mtoto anataka kumjua baba yake,kwa nini wanawake mnakuwa mnabana sana,mnaweka password kwa mtoto hata ikibidi kumdanganya babako kafa,why this?
But huo ugomvi ni kati ya baba na mama tu,mtoto yeyote lazima ateswe na duku duku la kumjua baba,hawezi ku take for granted easily.
Mungu akubariki na akuzidishie busara ulizonazoKwa mawazo yangu na mtizamo wangu, ni afadhali mtoto akaujua ukweli tu, kwamba fulani ndo baba yake,
pale apatapo akili za kujua mema na mabaya, na akili ya kujua kwamba kuna baba.
Upendo huwa unajengwa na ukaribu na uwepo wa mtu mwenyewe, haijalishi hata kama baba amekuzaa mara tatu, kama hana mapenzi na mtoto,
hawajibiki kwa mtoto, hapatejengeka upendo kati ya baba na mtoto. Mtoto mwenyewe ataona tu huyu ni baba kwa sababu alishiriki kunizaa lakini,
yule ambaye anamlea, na kumtunza pengine na kumsomesha na kumuonesha upendo huyo ndio atakuwa baba maishani mwake.
Tena usishangae mtoto akakutaa wewe mwenyewe kwa midomo yake, kwamba na mtambua huyu baba/mama/babu/mjomba nk nk, aliyenilea,
anakuuliza sasa wewe unasema we ni baba yangu kwa mpango gani?
Tukumbuke tu kwamba watoto, kuna wakati watakua wakubwa na wenye akili ya kujua mema na mabaya, na watajua kuchuja ipi ngano na ipi pumba. Kwa hiyo ni vema kuwa huru nafsini mwako, nakutojenga hatia nyingine kwa mtoto ako hasa pale atakapogundua kwamba ulimdanganya baba yake hayupo au ameariki.
Dah mi naona hakuna haja ya kubishana na ujinga wa mtu hapa duniani, kama anaikataa damu yake, namuacha itamtafuta/ataitafuta mwenyewe siku moja. Na mbaya zaidi wakati anaitafuta unakuta na yenyewe inamkataaa........
Mungu atusaidie tuponywe na hasira na majereha tuyapatayo katika mapito ya kukataliwa na watoto wetu, atupe neema ya kusamehe,
ili watoto wetu wawe na furaha na amani, na ikiwezekana kujijengea heshima nzuri mbele ya mtoto wako.
Sio vizuri mtoto anakua na kidonda moyoni, eti mama alisema baba yangu amekufa kumbe hajafa......
Atakudai kaburi lake na ndugu zake sijui utampeleka wapi......
Tujifunze tu kuushusha moyo na kurahisisha maisha......
Na huyo anayekataa watoto/mtoto malipo yake ni hapa hapa duniani wala hayasubiri siku ya hukumu.
Mungu akubariki na akuzidishie busara ulizonazo
Mungu akubariki na akuzidishie busara ulizonazo
Mkuu Mbu kuna mambo yanahitaji busara ya hali ya juu kweli na hizo busara ndio mke anatakiwa awe nazo...haki ya mungu tena, ana busara kweli huyu LD jamani.
Mimi mzima niko napiga stori na mende na mbu kabla ya kulalaAmina TF,
Hamjambo huko?
Muwe mnalala kwa afya ya akili bwana mzee................
...haki ya mungu tena, ana busara kweli huyu LD jamani.
Jamani tuangalie kwa nini wanaume wanakataa watoto au ujauzito.
1. wanawake tujaribu kuwa fair, kwamba mwanaume akilala na wewe siyo tija akuoe au uishi nae.
2. Kubeba ujauzito haukupi guarantee ya wewe kuishi na huyo bwana au kumfanya mwanaume abadili msimamo wake kuhusu wewe.
3. Mwenzako alihitaji muda wa kukujua vizuri, wewe umeenda kutumbukiza hiyo mimba na yeye hayuko tayari, akisema ukweli wake unalalama eti amekataa mtoto.
Nafikiri wanaume wabadilike kulinda matamshi yao nyakati kama hizi. Kama umeambiwa mwenzako ana ujauzito mwambie ukweli sitakuoa ila mama jifungue tu kwanza mambo mengine yafuate. Ukisema wewe hiyo mimba ni yako, na mtoto lea mwenyewe usinipe hata taarifa za kuzaliwa kwake. Hapo ndiyo wanawake wanakuwa na ghadhabu. (wanaume linda midomo inaumba).
Wanawake: Kumbuka kwamba wewe uligombana na baba, mtoto ana haki ya kujua nani babake. Inapotokea hiyo lazima huyo mtoto umpe jibu sahihi acha kupindisha maneno. Unapodanganya mtoto ujue kwamba anatake note, akigundua hatakuamini tena.
Kama kweli mzazi kafariki mpe ushirikiano, mpleke hata kwa bibi yake au ndugu wa mume akakutane naye. Mambo mengine ni ya kusamehe. Ila chanzo cha wanaume kukataa watoto vyanzo ni wanawake kuwa luba wa kuolewa wakidhani eti kuzaa ndiyo mwanaume ananasa.
Watch out gils ambao hamjaingia kwenye ndoa mwanaume hashikwi kwa mimba ni matendo yako na vile unavyobehave, wanawake nyenyekea hizo NGO za uongo na kweli eti GENDER ni ujinga mtupu. Hata kwenye biblia imeandikwa, Sara hakuwahi kumuita mumewe Ibrahim (BWANA). wanaume ni viumbe dhaifu sana, kuna jinsi ukitune tu anaoa bila hata kumlazimisha wala kushika fimbo. I wish ningerudi usichana leo, NI NOMA wadada. Ebu tubadilike.
CD