LGE2024 Wanawake Mshajiandaa kugombea nafasi za Uongozi Serikali za mitaa?

LGE2024 Wanawake Mshajiandaa kugombea nafasi za Uongozi Serikali za mitaa?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Wanawake, Umeshajiandaa kugombea nafasi za uongozi au mnasubiri mseme ningekuwa mimi ningefanya hivi, au haya mawazo yanatuumiza Wanawake au haya maamuzi hayawagusi wanawake?

Huu ndio muda muafaka wa Wewe Mwanamke kugombea ili yale maoni au fikra chanya ambazo umekuwa ukizitamni kuziona zikifanyika upate wasaa wa kuzitekeleza na si kubaki kulaumu tu ooo Wanawake tuko nyuma ooo wanawake hapa tumesahauliwa sasa ukumbukwe na nani na Wanawake mnakuwa wazito kujitokeza kwenye nafasi za uongozi.

Mtasema mazingira yanawanyima fursa lakini kwa nini msijipe ujasiri mkaonesha nia na kugombea, najua wanawake mna mawazo mazuri ya kujenga, mna mawazo mazuri ya kutengeneza sera kwa ajili ya watoto na Taifa kwa ujumla, haya huu ndio wakati, Jitokezeni kwa wingi mkagombee wakati ndio huu.
 
Back
Top Bottom