R-K-O
JF-Expert Member
- Jun 27, 2023
- 482
- 2,178
Miaka ya hapo zamani niliwahi kuwa urafiki wa kawaida na jamaa fulani aliehamia mtaani kwetu, mara kadhaa tulikuwa tunatembeleana kujuliana hali.
Kumbe hapa mama na dada yangu wakawa wanampa madebe ya mchele na maharage mara kwa mara, wao walidhani wanasaidia urafiki wetu, haya yalifanyika kimya bila mimi kujua.
Rafiki huyo akaanza kuwa kama chawa kabisa kila muda mtu wa kunicheki, kuulizia nyumbani narudi muda gani, n.k. hadi nikawa naona hii ni too much.
Kuja kufatilia naona kwamba jamaa anapewa madebe kila mara, mama na dada yangu wakawa wanasema wanampa kwasababu aliawaambia chakula kwake ni ugali tu basi wakaona kwa vile tupo karibu basi nae wakataka kumfanya mwanafamilia, kosa kubwa sana.
Niliwapiga marufuku, nikawaambia urafiki wa wanaume ni tofauti na urafiki wa wanawake, wasichanganye mambo.
Baada ya mwezi hivi naona jamaa kapunguza ari ya kunitafuta, muda ukaenda story ni kawaida tu. Sasa jamaa kuna siku namkuta sehemu anabeti, nikawa namwambia aache huo mchezo ataliwa.
Jamaa akaanza kunitania ila ile kwa maudhi kwamba hata yeye alitumia urafiki kupewa madebe ya mchele na maharage kwa udhamini wangu. Ni jibu lililoniudhi sana, almanusura nimkate kidevu, ila kwa heshima niliyonayo pale mtaani nikachill tu.
Urafiki wa wanaume sio wa wazi sana kama urafiki wa wanawake, wanaume tunasaidiana sana ila si hivi.