Wanawake: Mume ghafla anaanza kukosoa chakula chako………!

heheheheheheh Mtambuzi, waambie wenye wakwe na mawifi watata wasijaribu zoezi hilo....

Mie niliwataarifu ndugu zangu mapemaaa kabla sijaoa kwamba sitaki majungu wala ushirikina nyumbani kwangu.......
Kwa taarifa yako mie hata NAZI ninaikuna vizuri sana, na kama nikipika mboga mama Ngina anasonga ugali au vaisi vesa.......
 
safi sana, halafu hiyo inaongeza mapenzi mno, na mna-bond vizuri na mamsap....

ila ndugu uwiiiiiiiiii, heri ulivyowapiga biti mapema.......

maana hawachelewi kumwesabia mkeo makosa...hahahah maisha haya, very funny




Mie niliwataarifu ndugu zangu mapemaaa kabla sijaoa kwamba sitaki majungu wala ushirikina nyumbani kwangu.......
Kwa taarifa yako mie hata NAZI ninaikuna vizuri sana, na kama nikipika mboga mama Ngina anasonga ugali au vaisi vesa.......
 
safi sana, halafu hiyo inaongeza mapenzi mno, na mna-bond vizuri na mamsap....

ila ndugu uwiiiiiiiiii, heri ulivyowapiga biti mapema.......

maana hawachelewi kumwesabia mkeo makosa...hahahah maisha haya, very funny
BADILI TABIA Ukiona ndoa ninayumbishwa na ndugu, basi ujue huyo mume hana msimamo.
Mwanaume ni lazima uwe na mamlaka kwenye TERRITORY yako, yaani aje ndugu sijui katoka wapi huko eti ananibania pua...."Mkeo yuko hivi au yuko vile.." Thubutuuu, nitamuonyesha njia aliyojia ili achape mwendo. mke wangu sio wa shirika wala wa ubia, na kwa kulijua hilo, mimi sikutaka kuchangiwa sijui mahari wala kitchen Party wala harusi..... Nilichanga hela zangu nikawaalika tu kuja kula kisha wakatambaa, walibaki wakilalamika eti sikuwashirikisha.... ha ha ha haaa ili iweje? ili kesho waje waseme eti ndio walioniozesha mke....! Wengine eti walilalamika kwamba wamechangia sana harusi za wenzao, sasa kama ningewashirikisha wangechangiwa na wao hivyo ningepata michango mingi na hivyo ningefanya harusi kuuubwa.... Mimi siamini katika kuchangiwa, nilikomaa mwenyewe, na ndio maana sitaki na kamwe sitamchangia mtu harusi wala send off.......
 
Last edited by a moderator:
bora wewe una msimao na ulidhibiti mapema, kuna watu wako kweny ndoa mpaka unashangaa, zinakuwa controlled na remote...

ila ndugu wengine hata ukichimb mkwara watakuchimba tu....tena unakuta undugu wenyewe wa treni behewa la mwisho huko anataka kupanga masharti nyumbani kwako.....

loh kwa kweli mie nawaambia kwangu utakaa kwa sheria na kanuni zangu, hutaki timka...

ila unajua Mtambuzi ndoa inayosimama imara ni ile ambayo mwanaume hayumbishwi?
na unajua kuwa wazazi especially mama wa mwanaume ana uwezo mkubwa wa kuvunja ndoa? kama mwanaume hajasimama imara na kama mama ni mtata?

ila baba mkwe wengi wanakuwa hawana noma, sijui sisi wanawake tukoje, naombea nitakapozeeka nisije kuzeeka vibaya na kusababisha migogoro kwenye ndoa za vijana wangu loh......



 
Last edited by a moderator:

4. kama kuna mahali amepata anakula huko asema na mie nitafute pa kula {yes, najiua kuna watu watapinga hili...lakini sometimes usipokuwa bandidu, mwanaume atakutia presha, sometimes you have to learn your lesson a hard way...}

Hiyo no.4 umenikumbusha ule usemi ambao huwa siupendi kwamba dawa ya moto ni moto ....wakati kumbe dawa ya moto ni maji
 
Kuna kitu kingine pia... Hupendezwi na chakula lakini hujapata namna nzuri ya kufikisha ujumbe.. Wakati mwingine House girl anapika vizuri na unaona tofauti na kile anachopika Mkeo... Unabaki dillemma huku ukiogopa kusababisha tafrani si unajua kina mama wengine, atanuna wiki zima
 
gfsonwin njoo kitandani sasa...okay?
 
Last edited by a moderator:
waswahili husema 'ukiona manyoya jua kaliwa huyooo' kwa kweli uzoefu wangu wa miaka 20 ya ndoa najua ukiona mwanamume ameanza kukosoa chochote (si chakula tu) ambacho awali alikuwa anakiona sawa ujue anakulinganisha na mwingine ! kama ni chakula jua wazi kuna mahali anapikiwa msosi mzuri kuliko wa kwako, tena mahali hapo si hotelini ni kwa hawara tu, kuna vitu kama kukosoa mavazi yako, style za nywele, unaona anakuwa hayuko comfortable na wewe kuwa karibu nae hasa mnapokuwa nje ya nyumbani, anaanza kuona hata maongezi yako kama yanambore hivi, jua tu kuna mwenzako anaemfurahisha zaidi. na wewe ukilijua hili, mrahisishie kazi mueleze ukweli ajue kuwa umemgundua!
 
Comment kama hizo zinaondoa hata hamu ya kukaa mezani! Wanaume inabidi kubadilika, at least kuvumilia na kuyasema yaliyo moyoni baada ya mlo.Kwanza, kuandaa chakula siyo kazi nyepesi hata kidogo, hili lipo dhahiri. Mara kitunguu kiingie machoni nk. Hivyo aliyekiandaa anajisikia vibaya saaaaaaaaaaaaaaaaaana!!!!!!!!!! Subira ni nzuri.
 

Binadamu hatujaweza kukubali ukweli!
 
......hiyo ni dalili kuwa anaterezaaaa
so utaamua mwenyewe cha kufanya inategemea na mahusiano yenu yapo veepee....
Mtambuzi una vijimambo weyeeee...........
 
Lakini pia sio vibaya kama mkijaribu kuwashirikisha kupika waume zenu kwani mchuzi ukichachuka, hakuna lawama hapo.....




Hivi hizi picture wana act au inakuwaje? Tatizo la picture kama hizi zinaharibu sana vijana, wakiangalia hivi wanataka maisha kama haya, kumbe ni maisha ya picha tu... inabidi wawe wanasema jamani ni picha tu....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…