Wanawake na hofu ya kusaidiwa na nyumba ndogo

Yeye kuna kazi ni mvivu kufanya lakini kuna kazi anafanya na ambazo mimi siwezi kufanya. Hiyo ya kufua nimeshajipangia ni kazi yangu. Kwa mfano ananishave wakati mimi siwezi kumfanyia the same!

mnh kwani kimada na nyumba kubwa ni mtu mmoja?
 
Kwa kweli ni ngumu ila inabidi wakati mwingine umfanyie kumwonyesha upendo tu, na wakati mwingine anafanya na yeye pia, ila kuhusu pichu huwa zinatia uvivu kama unaweza unanunua washing machie ili urahisishe kazi bana
 
With time utajua kuwa huyo unayeishi naye ni mume au mwanaume wa kukuridhisha kimwili, only then will you know whether ur altitude is right or wrong.
 
ukiingia jf kila siku unaweza usioe au kuolewa

ndoa humu zoinaonekana nguuumu mno
Watu siku zote huwa nawaambia matatizo kwenye ndoa yanatofautiana mtu akiishasikia fulani ana tatizo kwenye ndoa yake basi unaanza kusikia anasema "Kama ndio hivyo mimi kuolewa sitaki kusikia" watu hawataki kujifunza wanataka mambo easy na mteremko ndoa sio gereza kama ukijua ni nini unapaswa kufanya kwenye ndoa yako basi hautaanza kuwa na wasiwasi kuoa/kuolewa cha msingi ni kumuomba Mungu tu lolote litakalotokea mbele yako kabiliana nalo na mshirikishe Mungu kwenye kila jambo mkiwa kama wanandoa.
 

.........................Paulune ni kweli usemayo lakini wengi tunasahau kuwa ndoa hujengwa na upendo, heshima na trust. Kumpenda, kumheshimu na kumtrust si utumwa hata kidogo. Wengi tunasahau kuwa kama ni wa kucheat atacheat tu hata ukiwa unambeba mgongoni kila siku........but kuna sababu zinazomsaidia kuongeza hamu yake ya kucheat..ukimpatia hizo sababu ah nyumba ndogo unaikaribisha mwenyewe.

Mumeo ukimpenda..........utamfulia kwa kuwa unampenda na si kwa kuwa u mtumwa au unaogopa nyumba ndogo!
Utamnyooshea kwa kuwa unampenda na usingependa asiwe smart huko barabarani, maofisini na mtaani kwa ujumla
Ukimpenda mumeo hutoona karaha kumfanyia kile ambacho unahisi unajisikia kumfanyia.

lakini kubwa zaidi ni kwa wewe kumtrust na kujijengea kujiamini kwa kuwa unajijua kuwa unaplay role yako kama mke mwema na bora bila kusahau kumkabidhi kwa sala kila siku iitwayo leo.
 
Samahani dada,kwani boxers na chupi hazifuliwi na mashine?...au mapenzi?
 
Kwa kweli mwanajamiione nakupongeza sana kwa ujumbe mzuri na wenye kujenga. Kwa wanawake wote walio ktk maisha ya ndoa na wenye kujua maana ya familia ujumbe huu ni ufunuo kwenu. Mmeelezwa vizuri ipasavyo kuenenda kimwili na kiroho. God Bless you Mwanajamiione
 
Mi sioni shida kumuhudumia atakaekuwa mume wangu, ili mradi ananipenda na kunithamini, ananitunza tunatunzana, tena nitamfanyia kwa moyo mmoja kama navoona wakubwa zangu wameolewa na wanawafanyia waume zao kama maagizo yanavosema......mwanaume abaki kuwa mwanaume tu, na sitafanya haya kwa hofu ya kuibiwa mume bali kwa mapenzi ya dhati nitakayokuw nayo kwake
 

Uporoto,
Akakufanyia hayo yote halfu ukamuacha...mhhhh!!!

Mzima lakini wewe? Nakutakia weekend njema!
 
Naona nimeparamia post ya watu si unajua ugeni tena. Ila na sisi vimada tunafua Paulina . Ndicho nilichotaka kukwambia sasa sijujajua kutumia JF vizuri.

mnh kwani kimada na nyumba kubwa ni mtu mmoja?
 
Naona nimeparamia post ya watu si unajua ugeni tena. Ila na sisi vimada tunafua Paulina . Ndicho nilichotaka kukwambia sasa sijujajua kutumia JF vizuri.
Kazi kweli kweli
 
Good point sister,
Nakumbuka nilipotoka chuo mwaka wa kwanza,marehem mzee wangu alikuwa anaona aibu kuniomba nimfulie nguo zake
Ingawa utotoni nilikuwa namuona mkoloni,I grew up and got the point.
Nilikuwa namwambia mama anitolee nguo zake,he really respected that and I felt blessed.
Thanx for reminding me,nimewahi kumfulia nguo mtu mzima na sometimes namwoshea mke wangu nguo zake,as long as she is there and the cycle is not full.
 

Haya ni mawazo pevu, mawazo ya kikubwa, nakushukuru sana. Mazingira ya west na hapa kwetu tofauti kabisa. West mama hana nafasi ya kufanya kazi za nyumbani amebanwa kama alivyobanwa baba, kwa hiyo kusaidiana ktk kazi ndogondogo ya home ni sawa. Hapa kwetu hatujabanwa kihivyo, sisemi eti baba asifue, mbona tunafua jamani. westernization tusipoangalia itatufikisha pabaya.
 

Wewe ni mpotoshaji, kama umekosa mtu wa kukuoa au kama umeamua kuwa single usiwavurugie wenye ndoa zao, yaani wanaopendana. Haya mawazo pauline, yanafanana na ya 'LESBIANS'. Labda na wewe ni LESBIAN. LESBIANS hawataki kusikia mahusiano kati ya mwanamke na mwanaume, watatoa hoja zao nyingi zinafanana na za kwako. Sisi ni wanaume wake zetu wanatufulia na sisi tunawafulia mara moja moja si mara nyingi sana kama wao wanavyotufanyia.
 
Na naomba ucthubutu kuolewa na mtanzania. Utanipa hasira...
 
Hutakiwi kufua nguo,kumnyooshea nk kwa hofu ya kusaidiwa na nyumba ndogo ila inatakiwa ufanye toka moyoni mwako.
wapo kinadada wanapenda kweli na wala hawahitaji kuombwa kufanya yote hayo na pia inategemea na imani yako kwani wapo wasichana wanaoamini kuwa mwanaume anatakiwa kufuliwa nguo zote,kunyooshewa kupikiwa nk.ukitaka kumsaidia anaona kama unataka kwenda kinyume na utaratibu na anaweza kuwa hata mkali ukitaka kulazimisha.
sasa wapo wasichana wa aina yako Pauline ambao ukimfanyia hayo mumeo waona ni kama favour tu na sio lazima ufanye.
aina yako siitaki itanipasua kichwa tu...ukimpata msichana alie na attitude kama ya Lizzy umeula.
bottom line,wapo wanaume wanaopenda kufanya kazi za ndani na wapo wasiotaka hata kusikia.so,ukilamba garasa pole zako.
 

hapo nilipobold mwanajamii huoni na wewe umeingia kny huu mtego wa kuwa mtumwa kwa kuogopa nyumba ndogo?sijakataa usimfulie mumeo ninachopinga in return mbona mume hajishughulisha na yeye kukufulia siku moja moja???hayo mapenzi mapenzi gani ya upande mmoja???kwani yeye ndio hapendi akuone unavutia mitaani?mbona asijishughulishe????mie ningependa kuconduct survey kuona wanaume wenye nyumba ndogo kama hawafuliwi na kunyooshewa nyumnbani?lol:lol:
 

i think nyie mnaotaka tuamini,ndoa ni mume kuwa kama mfalme na kutunzwa kama mtoto na sio kutunzana wote mke na mume ndio wapotoshaji wakubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…