Wanawake na kaburi la mapema....


Nimewahi kuzungumza na baadhi ya wanawake wanaoishi kwenye ndoa ngumu, wengi sababu wanazozitoa, ni kichekesho......
Kuna mmoja alidai kwamba, aliwahi kuonywa na wazazi pamoja na ndugu zake juu ya huyo mumewe kwamba sio mume mzuri, nadhani waligundua kasoro zake mapema, lakini yeye aling'ang'ania hadi akaolewa, ni kweli hata yeye aliziona hizo kasoro, lakini alijipa moyo kwamba huenda atabadilika (wenyewe husema akikua ataacha) lakini alipoolewa na mume yule hali ilizidi kuwa mbaya. Sasa anajiuliza, Je akienda kuwaeleza wazazi na ndugu zake kwamba ndoa imemshinda watamuonaje, anahisi watamshambulia na kumdhihaki

Mwingine naye alinieleza kwamba, alipompata huyo mumewe, alijikweza sana kwa marafiki zake kwa sababu mumewe alikuwa na hali nzuri sana kifedha, alidekezwa sana na alijiweka mbali na rafiki zake akihofia kuporwa mumewe, lakini baada ya kufunga ndoa, alifurahia ndoa yake kwa miaka mitano tu, baada ya hapo hali ilibadilika. Mume amekuwa malaya, amekuwa mlevi, na kila akirudi nyumbani lazima wagombane na kuishia kupigwa.............kwa ujumla ndoa yake imekuwa ni ya vurugu kila siku.
Na yeye anadai hawezi kudai talaka kwa sababu anaogopa kujidhalilisha, Je ndugu na marafiki zake watamuonaje?

Kwa hiyo kama ulivyosema, wapo wanawake wanakubali kufa huku wakiona kwa kuogopa kwamba jamii iliyo wazunguka itawaonaje pale watakapoachana na waume zao...................!

Kwa kweli zipo sababu nyingi sana na nyingine ni za kijinga kabisa.................
 
kwa sasa sijajua umri wako
naweza sema haya tu
kuishi kwingi kuona mengi

 
@Mtambuzi:Baba basi basi nimefuta usemi jaman lol!nipe mda nitakuletea mkweo soon nipe miezi kadhaa utapewa chako kwa kunizaa,kunisomesha na kunipa malezi bora!
 

Nimegundua kuwa woote walimaanisha ki2 kimoja ila kila moja wao aliielezea kwa namna tofaut! lol nimekupata nw mtambuz!
 
hivi adha yote hii ni ya nini! kwanini watu walioko kwenye mahusiano kila mtu kwa nafasi yake wasiamue kuwa waaminifu (a.k.a Kuacha mipango ya kando) coz to me nafikiri hii ndo challenge kubwa ktk mahusiano mengi. Mzee Mtambuzi umesahau wale wanaokasirika kufikia kiasi cha kujiua au wakati mwingine kuteketeza familia nzima kwa sababu ya haya maradhi yaliko kwenye ndoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…