Wanawake na kupenda wanaume wenye hela...

jamani,am grateful......ukitaka niona utaniona tu Elia niko kawaida kabisa......Big up yourself as well.....

Thanks, hope to see you and the rest of jf one day!
 

Samahani Michelle,
Kama hutojali unaweza kunijibu hapa hapa upenuni, ukiona noma fanya ze needful, Umeolewa dada yangu?
 

Asante kwa mawazo yako.....naona ume-generalize sana kuwa ni mazungumzo yote ya wadada yanaelekea kuchuna tu....labda unaozungumza nao....wengi siku hizi wameamka,ni wachache sana wanakalisha makalio kusubiri wanaume wa kuchuna na hata kupata mwenye hela ni matokeo pia....anaweza asije ukapata asiye nazo..... ni vizuri kujitegemea na kufanya kazi kwa bidii kwa wale ambao hawafanyi hivyo......

Wanaume wanapaswa kujua si kila mwanamke anawapendea hela zako,wengi wamejiwekea kuwa wanapendewa hela zao hata kama ninachopenda ni utu wako na ulivyo...wajiamini,wachukue muda kuangalia kama mapenzi ni genuine si kukaa na kusema tunawapendea hela...na wao pia wawe na bidii hakuna anayetaka mzigo wa mume na baba watoto....
 
Samahani Michelle,
Kama hutojali unaweza kunijibu hapa hapa upenuni, ukiona noma fanya ze needful, Umeolewa dada yangu?

ha ha ha ha, bado sijampata mume wa kunioa.....Mungu akipenda!!!
 
no comment for 2day...ila nahisi kuanza kuku-fuatilia kujua "UMEPATA WAPI" uwezo huu adimu sana kwa wanawake wengi hasa wa dunia ya tatu kama tanzania kuja na hoja +ve na ya-kujenga jamii kama hii... be blezd

AMEN, Be blessed too my brother!!!
 
sio wote ndio maana hata wewe umeweza kuleta hii post hapa lakini bado kuna kundi kubwa la kina dada wanaishi maisha ya kuchuna ,wengine ni wake wa ndoa kabisa lakini pesa yake yake ya mume ya wote na huo tunaita nini mume akikosa balaa kubwa huoni kama wanaume wantuona wachunaji hasa wale waliobahatika kuwa na kipato kikubwa hembu tusubiri mawazo yao.


 
no comment for 2day...ila nahisi kuanza kuku-fuatilia kujua "UMEPATA WAPI" uwezo huu adimu sana kwa wanawake wengi hasa wa dunia ya tatu kama tanzania kuja na hoja +ve na ya-kujenga jamii kama hii... be blezd
Mzeiya u are lost bana tokea mwaka huu uanze sijakuona hapa au ndio tunapishana otherwise hope u are good
 
Embu nielekeze namna ya kutoa thanks si unajua mambo ya technologia kule kwetu yamekaa kushoto nikupe shukrani zako za dhati
I think you have to log in first. Once you do it, below every post there are links of "Reply, Reply with Quote" on the right and "Thanks, Posted via Mobile" on the left.
Hope you find it useful.
 
Kuna msemo kutoka dini nyingi na kwa wanafalsafa unaosema hivi: "Tajiri si yule aliye na vingi bali yule anayetosheka na vichache". Wako wanaume wenye uwezo mkubwa na wametulia na familia zao, pia wapo wanaume masikini ambao ni viwembe. Zipo ndoa za masikini watupu lakini wameridhika na hali zao. Zipo ndoa za wanawake walioolewa na wenye uwezo na bado wanatoka nje. Kwa ufupi, dunia ina watu wa kila aina.
Ushauri wako dada Michelle ni mzuri sana - Turidhike na tulichonacho, mali usiyoitokea jasho haina baraka. Tujitume, tusali, tuombe, tulee ili tuwe mfano mzuri kwa watoto wetu. Tukumbuke, "Mtoto hufuata kisogo cha mzazi (mlezi) wake".
 

Ni kweli kwa sababu moja au nyingine simlaumu mwanamume anaposema wanawake ni wachunaji kwa kuwa wapo wanaofanya hivyo na wapo ambao hata elimu waliyonayo haijawasaidia kuondokana na fikra kuwa anapaswa kujitegemea na kuacha kutegemea wanaume.....ninayo imani maisha yanaendelea kubadilika na hali tu inavyozidi kuwa ngumu watabadilika,manake itafika wakati lazima nawe ufanye kazi ili familia isogee.....kwa kuwa wote si wachunaji,ni wajibu wa mwanaume kumchunguza yule anayempenda akiona anachunwa akimbie au azidi kumpenda ni uamuzi wake....lakini si wote tunachuna,na kwa kweli kuna wakati tunahitaji msaada wa hapa na pale,wasiache kutusaidia kwa fikra kuwa tunawachuna....thanks Chauro,i got your point.
 
ha ha ha ha, bado sijampata mume wa kunioa.....Mungu akipenda!!!

Una mawazo very constructive, kama wadada mkiendelea kuwa na mawazo ya namna hii basi huko mbele ya safari hakutakuwa na mambo ya kutuumiza vichwa.
Manake siku hizi ukitafuta gf au mke unaumiza kichwa, utampataje mkweli, manake wengi siku hizi wako kikazi zaidi.

Muombe Mungu aliyehai akupatie mume bora ili akusaidie kutimiza ndoto zako, manake unaonekana unajua unachokitaka.
 
Ha ha ha kule ambapo tulikuwa tunaongea mimi na H dah wewe mkali aisee, kama vile ulikuwa kwenye vichwa vyetu

ha ha ha ha ha ha....naona kaenda sali,ngoja arudi hapa......!!!:coffee:
 
hi akina MICHELLE,HASHYCOOL,THE FINEST,BIGIRITA EMT, BACHA and PAULINA!!!

ntarudi baadae kwa hii sred.
 

Asante sana dada yangu,mawazo mazuri sana na yenye hekima....
 

Tatizo kubwa linalotukabili wanaume wengi ni kumtambua mwanamke anayekupenda kwa dhati ya moyo wake.

Kuna wanawake wamefuzu chuo cha sanaa, yaani wanajua kujivika ngozi za kondoo huwezi amini, anakuwa mpoleee lakini akitaka kuvuna anajua tu atakukamatia wapi. wanawake wako tayari kuficha tabia zao halisi hata kwa miaka kadhaa ilimuradi watimize malengo. mwingine atakupeleka mpaka utamuoa akijua kwamba kwakuwa umemuoa basi utakuwa umeridhika kwamba anakupenda. Akishatimiza malengo yake hapo sasa anaanza kuchomoa makucha yake.
 

Ni kweli kabisa,najua si rahisi Mwita na tunafanya maamuzi bila kujua ukweli kuhusu wenzi wetu kwakuwa wanaficha makucha au ni wasanii....ni kujitahidi tu,kuchukua muda wa kutosha kuwafahamu na zaidi kumuomba Mungu aonaye sirini....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…