IBRAHIM ROJALA
Member
- Jul 16, 2021
- 25
- 25
Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara zinazofanya vizuri katika matumizi ya mitandao ya kijamii.
Ripoti ya takwimu za robo ya pili ya mwaka 2020 za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilionesha watumiaji wa intaneti wameongezeka hadi kufikia milioni 27.1 mwezi Juni kutoka milioni 26.8 Machi mwaka huu.
Lilikuwa ni ongezeko la watumiaji 268,057 katika kipindi cha miezi mitatu au sawa na asilimia 56.3 ya watumiaji wa simu za mkononi Tanzania ambao katika robo ya pili ya mwaka 2020 wamefikia milioni 48.2.
Taarifa rasmi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonesha kwamba watumiaji wa mtandao hadi kufikia Juni mwaka 2021 walikuwa milioni 29 ikiwa ni sawa na asilimia 49 ya watanzania wote.
Licha ya ongezeko hilo bado wanawake wako nyuma katika matumizi ya Mtandao ambapo Mobile Gender Ripoti ya mwaka 2019 inaeleza kwamba nchini Tanzania asilimia 17% pekee ya wanawake nchini ndio waliokuwa wakitumia mtandao kwa wakati huo.
Kundi hilo dogo la wanawake pia limekuwa likikabiliwa na matukio kadhaa yanayolifanya kuwa na hofu ya matumizi ya mitandao ya Kijamii ikiwa ni pamoja na ukatili wa mitandaoni.
Takwimu za hivi karibuni zilizotolewa Machi 31 mwaka huu jijini Dodoma na katibu Mkuu wizara ya maendeleo ya jamii Dkt. Zainab Chaula, alisema asilimia nne kati ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaokadiriwa kufikia Milioni 54 kwa sasa wanakabiliwa na ukatili mitandaoni.
Ukatili wa mitandaoni dhidi ya Wanawake ukoje Duniani?
Mwaka 2021 zaidi ya wanawake 200 wenye hadhi ya juu duniani walitia saini barua ya wazi iliyokuwa na lengo la kutaka hatua zichukuliwe dhidi ya unyanyasaji dhidi ya wanawake mitandaoni.
Miongoni ni pamoja na waziri mkuu wa zamani wa Australia Bi. Julia Gillard, mchezaji wa zamani wa tennis wa Marekani Billie Jean King na amuigizaji wa filamu wa Uingereza Thandiwe Newton,barua hiyo ilichapishwa katika Baraza la usawa la kizazi cha Umoja wa Mataifa.
Barua hiyo pia iliangazia utafiti wa mwaka 2020 uliofanywa na kitengo cha upelelezi cha intelijensia ya uchumi ukijumuisha wanawake zaidi ya 4,000.
Upelelezi huo uligundua kuwa asilimia 38 ya wanawake katika nchi 51 wamekumbana na unyanyasaji wa moja kwa mitandaoni(Chanzo,BBC Swahili Julai2,2021).
Nini maana ya ukatili wa kijinsia na Ukatili Mitandaoni dhidi ya Wanawake?
Kwa mujibu wa (TAMWA, 2017) ukatili wa kijinsia ni kitendo chochote kile ambacho anafanyiwa mwanamke au mwanamume ambacho kinalenga kumsababishia madhara ya kimwili, kiafya, kingono na kisaikolojia .
Ukatili wa kijinsia kwa njia ya mtandao ni vitendo vyovyote vile ambavyoanafanyiwa mtu anapokuwa anatumia mitandao kama sehemu yamawasiliano.
Matukio ya Ukatili Mitandaoni dhidi ya Wanawake nchini
Matukio ya ukatili dhidi ya wanawake mitandaoni ambayo yamekuwa yakiteka vyombo vya habari ni yale yanayowahusisha watu maarufu ingawa kuna wengine wengi ambao picha zao au video zao husambazwa na kutumika vibaya wakati mwingine bila ya wao kuwaa na taarifa.
Miongoni mwa matukio ya ukatili dhidi ya wanawake mitandaoni yaliyowahi kuripotiwa ni pamoja na tukio la mwaka 2018 lililomhusisha Amber Rutty aliyetiwa hatiani na kuhukumiwa kwenda jela kabla ya kutoka baada ya kulipa faini.
Video ya msanii wa muziki wa kizazi kipya Faustine Charles Mfinanga(Nandy) iliyovuja mwaka huo huo wa 2018 iliufanya mwaka huo kuwa na pilika pilika nyingi na mijadala kuhusiana na mienendo ya wasanii wanaoelezwa kuwa ni vioo vya jamii.
Mitandao ya kijamii haikumuacha salama Mshereheshaji,Mwanamuziki na Muigizaji maarufu nchini Menina Attick mwaka 2019 alikumbwa na kadhia ya video zinazoelezwa kuwa ni zake kuvuja mitandanoni.
Haya ni baadhi tu ya matukio lukuki ya ukatili dhidi ya wanawake mitandaoni ambayo yamewahi kuwa gumzo hapa nchini.
Kipi hupelekea ukatili dhidi ya Wanawake Mitandaoni?
Kupotea kwa maana halisi ya faragha ni miongoni mwa mambo yanayopelekea ukatili dhidi ya wanawake mitandaoni kukichangizwa na mabadiliko ya mitindo ya maisha.
Baadhi ya maswali ya kujiuliza katika hili ni kuwa mtu akiwa faragha anapata wapi muda wa kurekodi au kumrekodi mpenzi wake?Je walio wapenzi wanajua kipi kinapaswa kufanywa au kutofanywa wanapokwa faragha na huwa wanarekodi ili iweje?
Pili, kasi ya teknolojia dhidi ya mmomonyoko wa maadili,walio wengi kutokana na kukosa maadili huthubutu kujirekodi wenyewe na kuwatumia wanaume ambao wamefikia hatua ya kuwaita waume zao ilhali hawafahamiki kwa ndugu hata mmoja wa baina yao(kiumeni na kwa ndugu wa mwanamke).
Sababu ya tatu ni tama ikiwemo ya fedha kama ilivyotokea katika wakati ambao zilisambazwa video za msichana na chupa,wengi wao kwa kuongozwa na tamaa ya fedha na vitu vya thamani hujikuta wakiangukia kudhalilishwa mitandaoni mara baada ya kurekodi video za aina hii.
Matokeo ya ukatili huu ni yapi kama hautodhibitiwa?
Kutokana na fedheha itokanayo na uzalilishaji waliofanyiwa baadhi ya wanawake hulazimika kufanya maamuzi magumu na wengine hufikia hata hatua ya kujitoa uhai kutokana na kuvuliwa utu kupitia mitandao.
Ukatili mitandaoni unatesa,unaumiza hisia na hata kuharibu saikolojia ya aliyetendewa na wakati mwingine hugharimu maisha ya yule aliyetendewa hali inayotishia ustawi wa jamii ya baadae kwani wengi wanaofanya na kufanyiwa ni vijana ambao ni taifa la kesho.
Pia wanawake kutokana na hofu ya kudhalilishwa wanashindwa kutumia fursa za kujikwamua kiuchumi kupitia mitandao ya kijamii na hivyo kutonufaika na mabadiliko ya teknoloji.
Matahalani wanawake wanaojihusisha na shughuli za urembo hukabiliwa na hofu ya picha na video zao kutumika vibaya mitandaoni.
Kipi kifanyike ili Kukomesha Ukatili huu?
Elimu kwa jamii inapaswa kutolewa ili wananchi wafahamu juu ya uwepo wa sheria ya makosa ya jinai mitandaoni ya mwaka 2015 kama inavyoelekeza katika kifungu cha 14 na adhabu zake kama zilivyoainishwa katika kifungu cha 14(2).
Mamlaka za kiserikali TCRA na COSTECH kwa kutumia wataalamu wa tehama zinapaswa kutoa msaada wa kuziondoa mitandaoni video za wahanga wa matukio haya ili kupunguza athari za muda mrefu kwao.
Kwa makundi ya vijana wataalam wa kusaka na kusambaza kvideo hizi na ni wakati wa kuamua kusema imetosha nakuchukua hatua za dhati katika ujenzi wa jamii iliyostaarabika.
Aidha wanawake na wasichana wanapaswa kulinda thamani ya miili yao,mwanaume anayekupenda kweli hili linapaswa kuwa kipimo endapo akiomba picha za aina hii.
Ni muhimu kuthamini utu wa kila mmoja ndani ya jamii kama leo imetokea kwa yule unayefurahia kumtazama huku ukitabasamu na kumsambaza basi kesho inaweza kuwa kwa mpenzi wako au kwa dada yako au Ndugu yeyote.

Upvote
3