Wanawake na Simu ya mkononi?

simu shingoni inawezekana nyumbani, sasa hapa Bongo kwetu na vibaka wotee hawa mtaani tutoke tumevaa simu shingoni? siku moja si tutarudi nyumbani bila simu wajameni??, na pengine turudi bila shingo kabisa...


Unaweka shingoni,ukiwa nyumbani,sio kariakoo...ukijaribu kariakoo na manzese utakufa siku si zako..
Mbinu nyingine ambayo si salama sana,ni kuweka simu kwenye blazia au skintight/ch*P*...hapo ikilia utaipata tu.

Otherwise tabia hii ni kero sana...na ukitaka kujua ni kero we mama mpigie mmeo asipokee..na una issue ya msingi. utapima ni namna gani inakera.
 

ha haa umenichekesha kweli...bora kwenye bra, huko kwingine kuitoa nikiwa ndani ya daladala si itakuwa kazi!

mume wangu akipiga nikichelewa kupokea huwa ananiuliza kama niliiweka kwenye c**pi ndio maana ikabidi mpaka nitafute choo cha hoteli kabla ya kupolea simu LOL!
 

Hata kwenye bra ni hatari tupu.Kifua ni sehemu sensitive sana.Ukiyapitisha mamionzi direct unaweza kufa siku si zako ni bora hata vibaka wakukwapue.
 

Nadhani inabidi wanaume tubadilike kidogo. Binafsi nikimpigia mwanamke (iwe mke, dada, mama etc) simu sitegemei quick response kama vile ninapompigia mwanaume. Kwa kifupi najitahidi kumanage expectation na hivyo inapunguza disappointment kama simu haipokelewi.

Mimi kinachonikera kwa wanawake ni nini wanafanya baada ya kutopokea simu. Wengi wao they will never return the call, and even when they do, hata kuappologise wanashindwa! Hili pia najaribu kulifanyia kazi ili angalau nilizoee!
 
Shukrani kwa mtoa mada hii, itatusaidia wengi nahisi...
kwangu mimi kwa suala la nyumbani ntafuata ushauri wa Idimi wa kuvaa shingoni
kwa wakati wa kutoka bado kuna utata...simu yenye kelele? ...kuweka sidiriani?
 


huko ni kutesana sasa, wacha apige tu mpaka achoke nitakapoickia ndipo nitaijibu.
 

hahaha kwenye Bra wanadai zinaleta kansa
 

du pole sana kweli unakereheka
tutajirekebisha kama ni hivyo
 
tuna-solve vipi hii problem is long overdue.
kama wamo humu, waelewe kuwa wanatuboa, wabadilike, maana wao wanadai kuwa ukimuelimisha mwanamke mmoja, unaelimisha jamii nzima.
 
duh! kwanza hii mikoba ya kisasa XXXX large tunayoibeba ...mmmnh simu inaita ushaitafuta kwenye mkoba huipati ng'o mpaka mwenye kupiga anakata!
 

siku laumu kwa sababu umesha sema kuwa wewe bado upo upo sana.
Sidhani kama wanandoa wanaweza kuwa na simu hadi iwe kero kwa mwenzie hadi aamue kutokupokea simu au kuzima hivyo unavyopiga na isipokelewe kwa muda muafaka ni jambo la kueleweshana.
Lakini kuna jamaa mmoja aliniambia kuwa ukiona unapiga simu na kupokelewa haraka weka alama ya kuuliza.,huenda yupo na mwingi hivyo anaona kama akichelewa kupokea,aliyenaye anaweza akaipokea na kusababisha mambo kuharibika.
So try to think and make reference to previous days on how did she act on your calls. if any changes has been shown act upon those.
 
Jamani mwalia simu simu simu....wakati hakukuwepo na simu za mkononi hizo emergencies mlikuwa mnazi handle kivipi???
 
Shukrani kwa mtoa mada hii, itatusaidia wengi nahisi...
kwangu mimi kwa suala la nyumbani ntafuata ushauri wa Idimi wa kuvaa shingoni
kwa wakati wa kutoka bado kuna utata...simu yenye kelele? ...kuweka sidiriani?

It seems you like vibrations,......oh
 
Tatizo litakuja pale ambapo kwa bahati mbaya mwanadada anapiga simu ya kiganjani ya mwanakaka mara kadhaa afu simu iwe haijapokelewa....atapindiwa midomo na kununiwa mpaka akome ubishi! Mkuki mtamu kwa nguruwe hahaha

Wanawake mara nyingi vitu vyao huvihifadhi kwenye mikoba yao.Hawajazoea kushika mikononi.Wanaume kwa vile hamtembei na mikoba hamjajijengea kawaida hii na mara nyingi simu mnazishika au kuziweka kwenye vipochi na kutundika kwenye mikanda yenu ya suruali.Ukiona mwanamke kashika simu mkononi ujue basi ni mpya anajishaua nayo au hajawahi kuwa na simu ya kiganjani ni mara ya kwanza na hivyo bado ana mchecheto nayo.
Mkitaka kujua ni kweli basi oneni jinsi wanaume wengi wanavyolalamika hapa kuhusu wanawake na simu hizi.Mwanamke akishaiweke juu ya meza kama ni chumbani au sebuleni akiondoka huisahau hapohapo.Mtapata tabu sana kulizungumzia hili na ni vigumu kubadilika.Utashangaa kuwa mwanamke awapo mbali na nyumbani anapatikana kwa urahisi kwenye simu yake kuliko nyumbani - ni kwa vile huko yuko na pochi yake na humo ndimo anamoweka simu yake.
 
Very true.....
Wanawake hawajui
maana ya simu ya mkononi....
Baadhi yao.
Wengi utakuta simu iko jikoni yeye
yuko kibarazani...
Wanatia hasira hadi basi...

Kaka punguza ukali ndivyo walivyo tuwachukulie walivyo kama vipi mnunulie kale kamfuko cha kuning'iniza shingoni
 
Ngoja utakapokuwa maiwaifu wa mtu...uje utuambie inavyokuwa .Wakati mwingine wanawake hujionea kero kila saa kuwa na simu maana inaweza kuwa chanzo cha mitafaruku isiyokuwa na maana.
 
duh! kwanza hii mikoba ya kisasa XXXX large tunayoibeba ...mmmnh simu inaita ushaitafuta kwenye mkoba huipati ng'o mpaka mwenye kupiga anakata!


umenchekesha kweli mana mie ninakuwaga na kazi ya kumwambia naomba ni beep nijue fone ipo kona gani ya handbag, mweh.
 


Nakushauri uweke landline nyumbani au hata ile ttcl mobile na uiweke sebuleni au jikoni. Nilikuwa na tatizo hili na mke wangu, tuligombana sana mwisho nikaona isiwe tabu, nikaja na hiyo solution, nikaweka landline! akiwa nyumbani nikapiga mobile mara 1 bila kupokea, napiga landline (si unajua linavyolia) basi hata sekunde haipiti nasikia ''hallow'', akiwa ofisini natumia ya ofisini, akiwa ametoka, nimeweka ttcl mobile kwenye gari lake..... basi full covered nampata muda wowote. Hili ni tatizo la wanawake wengi, so usikasirike, tafuta solution!
 

Mnaona sasa mwingine huyu.

Isipopokelewa tabu, bibi yuko na bwana mwingine.

Ikipokelewa haraka nayo tabu, bibi yuko na bwana mwingine kwa hiyo hakutaka bwana mwingine apokee.

Sasa mnataka hawa wanawake wafanyeje?
 
Thanks ndugu, you made my day..duh JF kiboko asante...this is one of the options ambazo sikuwaza kabisaa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…