Wanawake ni viumbe maalum

Wanawake ni viumbe maalum

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,298
Reaction score
7,612
1. Mwanamke anapokasirika, zaidi ya nusu ya mambo anayoongea anakuwa hajamaanisha.



2. Wakati mgumu kabisa kwa mwanamke ni pale anapokuwa mbali na mwanaume anayempenda kwa dhati au anapogundua kuwa mumewe ana mahusiano na mwanamke mwingine.



3. Mwanamke sio kama 'tangazo la Omo', usipomjali na kumtunza... wengine wataifanya hiyo kazi badala yako.



4. Inamchukua muda mwanamke kumuamini mwanaume, na akikuamini ni ngumu kumbadilisha, lakini ukijichanganya, sahau kabisa kama atakuamini tena.



5. Mwanamke ni shule ambayo huwezi kuhitimu.



6. Cheti unachopewa unapomuoa mwanamke sio "leseni ya udereva" bali ni kama "kibali cha mwanafunzi".

7. Anaweza kuwa mchungu sasa hivi, lakini baadaye akawa malaika mtamu.. Itategemea namna utakavyoongea naye.



8. Ni ngumu mwanamke kusahau vitu, anakumbuka zaidi yale yanayomuumiza zaidi, hivyo epuka kumuumiza.

9. Mwanamke anaweza kuwa msiri sana... muda mwingi anapokwazwa na jambo anaenda kwa mtu wake wa karibu, analia.



10. Wanawake wote wanapenda kuombwa. Mara nyingi wanaume wanalisahau hili.



11. Wanawake wote wana tabia ya kipekee kama chumvi, unaweza usitambue uwepo wake lakini akikosekana vitu vyote vinakosa ladha.



12. Akikupenda kwa dhati anaweza kufanya chochote unachotaka afanye madamu kinakufurahisha, hivyo usimlazimishe kukupenda.



13. Mwanamke akikupenda kwa dhati, hata kukuomba pesa ataona aibu, na hasa kama anakupenda hawezi kuvumilia matumizi yako mabovu ya pesa...
 
Kuna dogo analelewa na shuga Mami, Hilo shuga Mami linaibiwa sana hela na huyo dogo, kesho yake asubuhi Mama stimu za gambe zikimwisha utasikia anasema chuma ulete kila siku wananiibia
[emoji1787]
 
Baada ya kuhimizana kutafuta hela tunahimizana kuwa busy kufurahisha watu ambao hata uwape nini bado watatafuta sababu ya kukuzingua.

Tafuta pesa zako, jiwekeze vizuri. Umiza kichwa utazeekea mji gani na kuishi kwa pensheni.
 
255752897029_status_1cbe1534431a41568bcb56ab19056c66.jpg
 
Baada ya kuhimizana kutafuta hela tunahimizana kuwa busy kufurahisha watu ambao hata uwape nini bado watatafuta sababu ya kukuzingua.

Tafuta pesa zako, jiwekeze vizuri. Umiza kichwa utazeekea mji gani na kuishi kwa pensheni.
Hata uwe nazo za kujaza dunia bado sisi ni kama maji. So zitafuteni sana maana tunazihitaji.
 
Namba 13.

Edit plz

"Hata kukuomba pesa ataona aibu"


Sio kweli!!!!

Tunaomba...tunaomba...na tunaomba tena!!!
Eti nione aibu kukuomba pesa kisa nakupenda[emoji2297][emoji2297]
Weeeeh naomba vizuuuri labda unipe mwenyewe kabla sijakuomba.
 
1. Mwanamke anapokasirika, zaidi ya nusu ya mambo anayoongea anakuwa hajamaanisha.



2. Wakati mgumu kabisa kwa mwanamke ni pale anapokuwa mbali na mwanaume anayempenda kwa dhati au anapogundua kuwa mumewe ana mahusiano na mwanamke mwingine.
We ondoa uongo wako kwenye point namba 13.

Hawa watu ni watu wetu tunawajua wengi ni makupe na gold diggers.

Ni wanawake kutoka royal families ndo wanaweza kuwa na mapenzi ya kweli maana hawamtazami mwanaume kama fursa wanamtazama kimapenzi..
Hawa wetu kitaa ni wasaka fursa, mdada anamaliza chuo akiwa hajapata ajira anahaha anafuta angalau bwana aolewe apate uhakika wa kula na pa kulala plus kuvaa.

Huyo useme ana mapenzi? Mmekutana umemtongoza kakubali, hayo mapenzi aliyapata wapi wakati alikuwa hakujui before? Sema anazoea kuwa nawewe
 
Back
Top Bottom