Elections 2010 Wanawake Pingamizi kwa mabadiliko ya uchumi wa Tanzania

Counterpunch,
Duh mkuu wangu unanipeleka darasani sasa!. Lakini mimi nadhani sisi wanaume ndio hufanya maamuzi kwa mioyo kuliko akili kwa sababu nijuavyo kmimi mwanamke hawezi kumpenda au kumchagua mtu bila mapenzi ya haki wakati sisi wanaume huchagua vitu random yaani with ego ya kujaribu tu hata iwe ktk mapenzi.

Wahenga wanasema mwanamke hawezi kutembea na mwanamme pasipo kuwa na maepnzi na huyo bwana lakini wanaume wanaweza kujaribu tu..Kitu pekee ambacho kinaweza kumshawishi mwanamke nje ya mapenzi ya dhati ni ushawishi wa fedha au Umaarufu wa mwanamme hali wanaume hujiweka mbali kimapenzi na wanawake wenye sifa kama hizo. Ukiona mwanamme anamfuata sana mwanamke mwenye fedha basi watu humsema kuwa na tabia za kike!

Hivyo basi nadhani hapa ktk swala la kuchagua viongozi wetu pengine wnawake wanvutiwa kimapenzi na hao wagombea au wanavutiwa na sifa za ambazo wewe mwanamme huzikimbia. na nadhani ingekuwa bora zaidi kama tungeorodhesha ushahidi wakuonyesha wanawake wako mbele ktk maamuzi mabaya kuliko wanaume kwani ktk misafara mingi ya viongozi wetu wabovu mimi huona wanaume wengi zaidi wakimsindikiza Fisadi kuliko wanawake.

na mwisho, nadhani pia mila na desturi zetu ambazo zinadumaza wanawake ktk kufikia maamuzi ya kimaisha inaweza pia kuchagia sana. wanawake wengi sana hawana nia wala mapenzi na siasa. kwao hii ni kazi na majukumu ya wanaume kinyume cha mitazamo ya haki na uhuru wanaotakiwa kuwa nao. Na hakika mara nyingi wanawake wetu hawapendi kazi nzito kwa pato kidogo - Wa Spanish wanasema Puche trabaho poko dereno...
 

Mkuu hujanipata nahisi.

Nilichomaanisha ni kuwa ili kumkomboa mwanamke ni lazima mwanamme akubali hilo kwanza au zowezi zima litafeli.

Mfumo dume umetawala katika jamii yetu kwa kutumia sababu za kimila, tamaduni, na dini..

Ikiwa mwanamke haruhusiwi kutoka ( haruhusiwi na mwanamme ) au kwenda katika mikutano na mikusanyiko ya kijamii, ujumbe utamfikiaje?

Ndio nikasema iwapo wanaume wataelimika basi wanaweza kuwaachia wanawake nafasi za kufikiri na kujiamulia mambo kwa mujibu wa wanavyofikiri wao na sio matakwa ya wanaume.

Note: hadi Leo hii kuna wanawake ambao wanaambiwa na waume zao kura wapigie chama gani.

Ukiwauliza kwa nini hawabadili kura wakati wanaume hawaingii nao kwenye chumba cha kura wanasema mungu anawaona kuwa anampinga mumewe hivyo hawezi na anaogopa akiulizwa na mumewe hataweza kumdanganya
 

Hapa hebu njoo utoe ufafanuzi...... Kwa vipimo gani umeona kuwa mwanamke hawezi kuongoza Kama mwanamme?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…