mimi nimelelewa na mama wa kambo karibia maisha yangu yote maana mama yangu alifariki tangu nikiwa darasa la kwanza lakini sijawahi kunyayasika kwa njia yoyote ile huyu mama amekuwa mtu mwenye upendo sana na nimejifunza mengi kutoka kwake na nitaendelea kumshukuru sana maisha yangu yote.
SIO MAMA WA KAMBO WOTE WANA ROHO MBAYA .
Ingawa sio wote wenye ukatili ila wapo na ni wengi kuliko wenye wema kwa watoto wa wenzao.
Mimi ni mhanga so najua ubaya wa hawa watu dingi akirudi huwa anajikomba ili tusianike maovu yake dingi akiwa hayupo.
Mbaya zaidi wengine ni waumini wa mstari wa mbele wa madhehu tena ni viongozi
Inategema na wanawake sio wote, kuna mwanamke mimi namjua analea mtoto wa mme wake kwa mapenzi zaidi, kuliko watoto zake wenyewe wa kuzaa na huyo mme wake.
Sio wanawake wote wana roho mbaya, matatizo sisi wanaume tunatazama upande mmoja tu, hatutazami upande wetu pia.
Usisahau kuna parcentage kubwa ya wanaume wana roho mbaya kuliko wanawake :cool2:
mimi nimelelewa na mama wa kambo karibia maisha yangu yote maana mama yangu alifariki tangu nikiwa darasa la kwanza lakini sijawahi kunyayasika kwa njia yoyote ile huyu mama amekuwa mtu mwenye upendo sana na nimejifunza mengi kutoka kwake na nitaendelea kumshukuru sana maisha yangu yote.
SIO MAMA WA KAMBO WOTE WANA ROHO MBAYA .
kwakweli msitukumbushe sie tulioteseka jamani,huwa sielewi ni nn hasa inakua ivo mana hatukuwa wakorofi wala nini
ila Mungu hulipa hapahapa duniani,now tuko ngangari kama "skype avosema"
je baba wa mtoto nae ana nafasi gani katika hili sekeseke?
Baba wa mtoto akiwa karibu na mtoto wake na kumpenda kwa dhati atahakikisha huyo mama wa kambo hamnyanyasi mwanae.
Kwangu mtoto anatangulia kabla hata ya maslahi yangu. Asilani siwezi kuruhusu mtoto wangu kukosa furaha na amani kisa mama yake wa kambo.
Ndiyo maana ni vyema wazazi wakawafundisha watoto wao kutokukubali kunyanyaswa na yeyote yule. Mimi sioni ubaya wowote ule kumfundisha mtoto wako kuwa hakuna mwenye haki ya kumpiga, kwa mfano.
Na ikitokea kapigwa basi naye apigane. Heshima wakati mwingine ni lazima mtu uitafute la sivyo utafanywa mkeka.
Ni kweli NN, ukaribu wa baba kwa mtoto ndio kinga pekee inayoweza kumwepusha mtoto na manyanyaso/vipigo kutoka kwa mama wa kambo...Baba wa mtoto akiwa karibu na mtoto wake na kumpenda kwa dhati atahakikisha huyo mama wa kambo hamnyanyasi mwanae.
Kwangu mtoto anatangulia kabla hata ya maslahi yangu. Asilani siwezi kuruhusu mtoto wangu kukosa furaha na amani kisa mama yake wa kambo.
Ndiyo maana ni vyema wazazi wakawafundisha watoto wao kutokukubali kunyanyaswa na yeyote yule. Mimi sioni ubaya wowote ule kumfundisha mtoto wako kuwa hakuna mwenye haki ya kumpiga, kwa mfano.
Na ikitokea kapigwa basi naye apigane. Heshima wakati mwingine ni lazima mtu uitafute la sivyo utafanywa mkeka.
Ni kweli NN, ukaribu wa baba kwa mtoto ndio kinga pekee inayoweza kumwepusha mtoto na manyanyaso/vipigo kutoka kwa mama wa kambo...
Ila cha kushangaza kuna wanaume wajinga sana, eti libaba linahama upande wa mwanae na kuwa upande wa mkewe, kila anachoambiwa na mtoto ni uongo na kila anachoambiwa na mkewe ni ukweli, mtoto anabaki peke yake, hana wa kumsapoti wala kumweleza shida zake...hapa atanyanyasika mpaka apate akili ya kiutu uzima aweze kujiokoa peke yake.
Mama wa kambo huwa wanapima upepo wa baba akikuta libaba lege lege basi huyo mtoto cha moto atakiona, ila kama baba anamsimamo na yuko upande wa mtoto kamwe hatathubutu kumnyanyasa... Mtoto anajenga kujiamini na ataishi kwa amani...