Wanawake tu, ndio wajibu swali hili

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Hebu tuchukulie kwamba, kuna mwanaume amekutongoza kwa muda mrefu sana, na baada ya kujiridhisha kwamba yuko serious ukaamua kuwa na uhusiano naye ukiwa na matarajio makubwa juu yake.

Lakini, kumbe siku mlipokutana kimwili alikupiga picha kadhaa bila wewe kujua mkifanya mapenzi, na picha nyingine ukionekana kitandani kama ulivyozaliwa. Baadae unagundua kuwa jamaa huyo ni kicheche, yaani hajatulia. Unapomwambia waziwazi kuwa hupo tayari kuendeea kuwa na uhusiano naye kutokana na tabia yake hiyo, anakuonesha hizo picha na kukutishia kwamba atazisambaza mitaani na kwenye mitandao ya kijamiii ili kukudhalilisha. Anachotaka ni kukufanya mtumwa wake, ufanye vile anavyotaka na usithubutu kutaka kuachana naye.

Hebu niambie, kama ni wewe ungefanyaje?
 
Hee!Samahani kumbe hiki choo ni cha kike!!
 
Namkodishia wahuni qa ku m cameroon na kumpiga picha,then tuone nani mshindi

Kama akifanyiwa hivyo na akadai msimamo wake ni huo huo, na hatojali kusambazwa kwa hizo picha zake, itakuwaje?
 
Kama akifanyiwa hivyo na akadai msimamo wake ni huo huo, na hatojali kusambazwa kwa hizo picha zake, itakuwaje?

Hili picha lazima stelingi wake awe mbwa,maana mastelingi wanawake huwa wanakufa picha ikiwa haijaisha halafu inamaliziwa na mbwa!
 
Unakubali kuwa mtumwa, in a month (silence killing) sikwambii namuuaje?. Hivi kweli kunakitu kinachomshinda mwanamke katika ulimwengu huu? Utanifanyaje mimi mtumwa wako.
 
Kama akifanyiwa hivyo na akadai msimamo wake ni huo huo, na hatojali kusambazwa kwa hizo picha zake, itakuwaje?

Hiyo ikishindikana polisi moja kwa moja,but am sure haiwezi kushindikana labda kama ni gay na anataka kubakwa daily
 
Unakubali kuwa mtumwa, in a month (silence killing) sikwambii namuuaje?. Hivi kweli kunakitu kinachomshinda mwanamke katika ulimwengu huu? Utanifanyaje mimi mtumwa wako.

Na kama kweli yeye ni gay na haoni hatari yoyote zaidi ya kumsaidia kutangaza tu biashara utafanyaje?!!..
 
Hiyo ikishindikana polisi moja kwa moja,but am sure haiwezi kushindikana labda kama ni gay na anataka kubakwa daily

Na kama kweli yeye ni gay na haoni hatari yoyote zaidi ya kuona tu unamtangazia biashara,utafanyaje?!,.
 
Polisi moja kwa moja ......ahsante

Gaijin kwanza jiulize maswali haya:
Je, ushahidi unao?
Je, rushwa unayo?
Je, unaweza kuvumilia kejeli za Mapolisi pale kituoni, kumbuka huyo kijana ataonekana ni kidume na wewe utaonekana ni malaya..
 
Unakubali kuwa mtumwa, in a month (silence killing) sikwambii namuuaje?. Hivi kweli kunakitu kinachomshinda mwanamke katika ulimwengu huu? Utanifanyaje mimi mtumwa wako.

Wewe Jela inakuita kabisaaa...........sio rahisi hivyo!
 
Gaijin kwanza jiulize maswali haya:
Je, ushahidi unao?
Je, rushwa unayo?
Je, unaweza kuvumilia kejeli za Mapolisi pale kituoni, kumbuka huyo kijana ataonekana ni kidume na wewe utaonekana ni malaya..

Ushahidi kuwa anazo picha sina (unless awe kama amenionyesha), lakini ninaweza kufungua mashitaka kuwa "amenitishia". Ni sawa na kufungua mashitaka pale mtu anapokutishia kukuuwa japo ikiwa alikutishia mkiwa wawili tu peke yenu.

Sihitaji rushwa kwa sababu ni haki yangu ya msingi. Hakuna means nifike polisi kisha wasiandike kesi wanidai rushwa

Kejeli za mapolisi hazinihusu wala sizijali hata kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…