Da , inasikitisha sana pole wanaume wote mnaopitia hayo, na kwa asili mwanamme siyo mwepesi kuelezea matatizo ya ndani ya nyumba yake hadharani ukiona wanaume wanaeleza matatizo ya wake zao jf basi fahamu yamewafika shingoni.
Lakin baadhi ya mwanawake mwenye tabia hizo, unajisikiaje
usipoihudumia familia yako japo unawezeshwa na mumeo??
Unapowachukia ndugu wa mumeo hata kama wao wanakupenda??
Na kibaya zaidi unawachukia wazazi wa mumeo, waliomlea vizuri na kumpa elimu na mwelekeo mzuri wa maisha.
Hivi wazazi wako wakinyanyaswa na mumeo kama unavyowanyanyasa wewe wakwe zako utajisikiaje???
Mwanamke unapoolewa ondoa mtazamo kuwa ndugu wa mume ni wabaya siku zote,bali wachukulie kama hao ni sehemu ya familia yako. Hata wanapokukosea wasamehe kama wewe unavyosamehewa pindi unapokosea.lililo muhimu ni kufahamu kuwa unapoolewa unaenda kuungana na familia mpya,jaribu kuwasoma pia fahamu hao siyo malaika ni binadamu kama wewe wenye mapungufu na mazuri yao,tupendane na tuvumiliane.
Wanawake tukosoane,tusahihishane,tufundishane, pindi mwanamke mwenzetu anapoonesha tabia mbaya kwa mume,familia zao ,pia hata kwa familia ya mume, ili tuoneshe kwa vitendo kuwa sisi ni watu wenye hurumu na upendo.
Kabla haujamfanyia mtu mwingine kitendo kibaya jaribu kujiuliza je ukifanyiwa wewe hicho kitendo kibaya utajisikiaje??.
Ndoa kitu cha thamani sana ukijua na kufahamu thamani ya ndoa, pia fahamu siyo kila mtu anatimiza ndoto ya ndoa ,wewe uliyekifikia mtukuze /mshukuru mungu kwa kumtunza mumeo na familia yako kwa ujumla. Wengine mpaka mauti inawafikia pasipo kupata heshima ya ndoa japo sifa zoooote za kuolewa wanazo lakin wanapungukiwa na bahati ya kuolewa...mwanamke iombee ndoa yako kwa imani yako,iheshimu,ithamini,itunze,ilinde ili mumeo na familia yako wafurahi na kumshukuru mungu kwa kuwa na mama mwema.