Wanawake uvimbe mji wa mimba, maumivu na dalili zake

Wanawake uvimbe mji wa mimba, maumivu na dalili zake

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,925

attachment.php


Kuna pia magonjwa ndani ya mji wa uzazi ambayo pengine huweza kusababisha harufu licha ya mchanganyiko wa kawaida katika taratibu za utungaji mimba.

Wengi hupatwa na uvimbe au vimbe mbalimbali ambazo huweza kusababisha kutokwa na uchafu, harufu na pia kusababisha kuharibika kwa mimba au kukosa kushika mimba kabisa.

Fibroid
Aina ya fibroid (s ), yaani uvimbe kwenye mji wa mimba.

Dalili:
Dalili zake ni hedhi nzito kupita kiasi, utokwaji wa uchafu ukeni, mimba kuharibika, maumivu chini ya kitovu kwa katikati, kuongezeka kwa tumbo kadiri uvimbe huu unavyoongezeka, n.k.

Ovarian Cyst
Hii ni aina ya uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke. Hutokea kwenye vifuko vya mayai ya uzazi, kwa ndani au kwa nje, na yaweza ikawa kwenye kifuko kimoja cha mayai au vyote viwili.


Dalili

Dalili kubwa ya uvimbe wa aina hii ni kichomi chini ya kitovu na sehemu moja. Kichomi huzidi sana mgonjwa anapocheka kwa nguvu au kuinama au anapobeba vitu vizito.

Dalili nyingine kubwa ni kuwa na tatizo la hedhi inayokoma kwa zaidi ya miezi mitatu, tatizo ambalo kitaalamu huitwa Amenorrhea, maumivu wakati wa kutoa haja ndogo na kutoa haja ndogo mara kwa mara, maumivu ya kiuno kwa nyuma, maumivu wakati wa kujamiiana, maumivu makali wakati wa hedhi, kupoteza hamu ya kula, kuongezeka uzito na unene kwa kiasi.


Mwanamke anapoona dalili zaidi ya moja kati ya hizi awahi kwenda hospitali.

 

Attachments

  • 1uterinefibroids.jpg
    1uterinefibroids.jpg
    36.8 KB · Views: 1,430
ma viungo yanatisha hayo, bora hata yangekuwa na rangi ya bluu mpauko.

Ila kuna umuhimu wa akina mama kwenda kwa gyno hata 2 kwa mwaka
 
ma viungo yanatisha hayo, bora hata yangekuwa na rangi ya bluu mpauko.

Ila kuna umuhimu wa akina mama kwenda kwa gyno hata 2 kwa mwaka

Hiyo ndio rangi yake, mwili wa binadamu umejaa damu ndio rangi ya ndani ya mwili awe mzungu au mweusi rangi ndio hiyo.
 
Back
Top Bottom