Duh! mjadala wa tamaduni bado upo tu?
Tutapiga sana kelele... lakini tukumbuke Mila, tamaduni, Values..tumeshachakachua . Hatuna cha kujivunia tena ..tumeviuza vyote kwa mazingira, utandawazi, ukoloni.. n.k
By the way... tusijali sana ..naona mamlaka zinachukua hatua madhubuti kurudi tulikotoka kwa spidi kali.....mfano zamani hawakuwa na umeme waliishi kwa viginga vya moto..nadhani Mgawo wa Tanesco ni matayarisho kurudi kwenye giza totoro kwani iko siku tutaona Tanesco wanatoa minara ya umeme kufanya kuni..... Huduma za afya ..zamani waliishi kwa mizizi....Mambo ya vikombe vya loliondo ni dalili tosha hatuitaji dawa za mdhungu.... Mafuta ya magari hakuna tena..baada ya miezi michache tutatupa mikweche yetu na kuanza kutembea kwa miguu.. Maji ya Nuwa yanatoka kwa kubahatisha...ni mafundisho ya kujifunza kuchimba visima na kujisadia porini...
Tanzania = Back to square one!